Tuesday, June 4, 2013

ENEO KUBWA KWA AJILI UFUFUAJI WA VIWANDA LATENGWA JIJINI TANGA

Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma.

Serikali kupitia Mamlaka ya EPZ imetenga eneo lenye ukubwa wa Hekta 1,363 katika Mkoa wa Tanga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na uthamini wa eneo husika umekamilika.

Hayo yamesemwa Bungeni Jijini Dodoma wakati Waziri wa Uwekezaji, Mhe. Mary Nagu akijibu swali la Mhe. Omari Rashidi Nundu kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara aliyetaka kujua ni matayarisho na utekelezaji upi unafanywa na Serikali  uweza kutekeleza azma hiyo katika kipindi cha mwaka 2010-2015 na ni nini hatma ya Viwanda vya zamani ambavyo kwa muda mrefu havifanyi kazi.
 Mhe. Nagu amesema kuwa mkakati wa kuufanya Mkoa wa Tanga kuwa jiji la viwanda upo katika hatua nzuri na kuongeza kuwa kwa hivi sasa viwanda vipya vilivyojengwa na vinavyojengwa ni pamoja na kiwanda cha NILCANT cha kutengeza chokaa, kiwanda cha Rhino Cement pamoja na kiwanda cha Sungura Cement ambacho kinatarajiwa kujengwa.
“Jiji la Tanga limeingia ubia na kampuni ya Korea (GoodPM) kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa kujenga viwanda 15 katika eneo la ekari 73 huko Pongwe unaotarajiwa kuanza mwezi Mei mwaka huu chini ya utaratibu wa Tanga Economic Corridor”. Alisema Waziri Nagu.
Akijibu swali la nyongeza toka kwa Mhe. Nundu lililotaka kujua kama Serikali iko tayari kufanya tathmini kufufua viwanda vya zamani, Waziri Nagu amesema kuwa Serikali inakubaliana na hilo na iko tayari kuhakikisha viwanda hivyo vinafufuliwa.
 Aidha Mhe. Nagu aliongeza kuwa Serikali ni moja hivyo itashirikiana na Wizara ya Viwanda kupitia Waziri wa Viwanda kuhakikisha kuwa viwanda vya zamani vinafufuliwa.

Tuesday, April 2, 2013

Kikwete: Sibagui dini yoyote nchini

 http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1736606/highRes/484917/-/maxw/600/-/elgirl/-/jk.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Rais Kikwete alisema hayo juzi katika hotuba yake ya ambayo huisoma kila mwishoni mwa mwezi, kauli ambayo imekuja wakati kukiwa na malalamiko kwamba Serikali imekuwa ikifumbia macho matukio ya uhalifu wenye sura ya uhasama wa kidini.

“Mimi binafsi sibagui, hushiriki shughuli za Waislamu na Wakristo kila ninapoalikwa labda nikose nafasi kwa sababu nyinginezo,” aliongeza Rais Kikwete.

Alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakisema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa Kikristo na kwamba amekuwa akipendelea kushiriki zaidi katika shughuli za Kikristo kuliko za Waislamu.
“Naambiwa kuwa niko mwepesi kushiriki maziko ya maaskofu kuliko ya masheikh wanapofariki.

“Kuna misikiti mitatu ya Jijini Dar es Salaam ambayo iliwahi kunisomea itikafu ili nife kwa sababu za kubagua dini yao.
“Katika itikafu hiyo waliwajumuisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova,” alieleza Kikwete.
“Nimeshashiriki mazishi ya Masheikh kama nifanyavyo kwa maaskofu na watu mbalimbali Waislamu na Wakristo,” alisema.

Alifafanua pale ambapo hakushiriki mazishi ya sheikh au askofu itakuwa ni kwa sababu ya kubanwa na shughuli nyingine ambazo ni lazima zifanywe na yeye au taarifa ilikuwa ya muda mfupi.
“Waislamu desturi yetu ni kuzika mara mtu anapofariki, hicho ni kikwazo kwangu kushiriki mazishi ya masheikh hasa ikiwa ni nje ya Dar es Salaam kwa sababu ya taratibu za kumsafirisha Rais kutoka mahali pamoja kwenda pengine siyo nyepesi,” alisema Kikwete.

Alisema pia Waislamu wanadai kuwa kitabu chao kitakatifu, yaani Quran Tukufu, kinadhalilishwa kwa kuchanwa, kuchomwa moto na kukojolewa na Wakristo na Serikali haichukui hatua yoyote ya maana. Alisema imefika mahali viongozi na waumini wa dini hizo kubwa mbili kama hawatakubali kubadili mwelekeo wa sasa basi tunakoelekea ni kubaya
“Nchi yetu tutaivuruga na sifa yake ya miaka mingi ya Waislamu na Wakristo kuishi pamoja kama ndugu itatoweka. Tanzania itaacha kuwa kisiwa cha amani na kuingia katika orodha ya nchi zenye migogoro na hata vita ya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kikwete.

Alisema Serikali haifurahishwi na kitendo cha mtu kudhalilisha dini ya mwenzake ndiyo maana wapo wahadhiri wa dini ya Kiislamu na wahubiri wa dini ya Kikristo ambao wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka katika matukio tofauti.
“Vyombo vya usalama vinatambua wajibu wao na kama havitimizi wajibu wao huo utakuwa ulegevu wao na siyo kwamba ni sera na maelekezo yangu au ya Serikali,” alisema Kikwete.

Aliongeza; “Mtakumbuka kuwa mara kadhaa nimewakumbusha wakuu wa mikoa, wilaya na vyombo vya usalama kuacha ajizi katika kutimiza wajibu wao kwenye suala hili.”

Kikwete alisema kuuawa kwa viongozi wa dini na kuchomwa makanisa kusichukuliwe kama Serikali yake imeshindwa kulinda usalama wa raia wake.

“Kama ingekuwa hivyo, tungeshuhudia mauaji ya raia, viongozi wa dini na matukio ya kuchomwa nyumba za ibada yakiwa mengi hapa nchini,” alisema Rais Kikwete.

Ajali ya Jengo la ghorofa lililoanguka

Kikwete alisema sheria zitafuata mkondo kwa waliosababisha kuanguka kwa jengo hilo baada ya uchunguzi unaofanywa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.

Alisema watakaobainika kuhusika watatakiwa kufikishwa mahakamani ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni zao za kuendesha shughuli za ujenzi.

Alitaka mikoa yote nchini kujifunza katika ajali hiyo kwa kufuata kanuni za ujenzi ili kuondokana na maafa yanayoweza kujitokeza.

Monday, April 1, 2013

Ajali; Simulizi ya aliyenusurika kifo kutoka ghorofa ya 15


Rais Kikwete na Mkewe, Mama Salma Kikwete wakimpa pole Yusuph Abdallah katika Hospitali ya Muhimbili walipotembelea majeruhi wa ajali ya kuporomoka jengo la ghorofa 16

“Majira ya asubuhi kati ya saa mbili na saa tatu hivi nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu jina maarufu anajulikana kama Tafu, ambapo alinitaka niende nikaonane na mkandarasi wa jengo hilo ili anipe kazi ya kuweka madirisha,” anasema Mlela.
Anasema wakati akijiandaa kutoka mke wake alimwambia siku hiyo apumzike asiende kufanya kazi naye akakubali, lakini haikupita muda mrefu mke wake alimfuata na kumuuliza amesikia taarifa kwamba kuna jengo limedondoka?
“Niliamua kwenda katika eneo la tukio na ndipo alipogundua kwamba eneo hilo ndiyo alipotakiwa kwenda kufanya kazi. Wakati juhudi za uokoaji zikiendelea nilijaribu tena kumpigia simu rafiki yangu.Nikiwa bado kwenye eneo la tukio ghafla nikaona mguu ukitolewa kwenye mchanga na nilitambua ulikuwa mguu wa rafiki yangu baada ya kuona kiatu chake.”

Sunday, March 31, 2013

mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam

jengo lililoporomoka na shughuli za uokozi mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam Machi 29, 2013

PICHA TOFAUTITOFAUTI ZIKIONESHA SHUGHULI ZA UOKOZI ZINAVYOENDELEA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjih22Xpq4njTzY8r3PphRh1uZLSdgFIef-WoxGAMpYdIWWVJpPAkIqdPOMIE6Iosu6bIhMmr6VTHXaFxU0YS2bs3BNF9NLYmkkGWpTsKzdx95fxVx4NGxofEamb9i8G8suruGPCMa5UT4/s1600/Untitled.png



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDNt_J7aN8oKOA8LqIXNxm_JK54Hpek10yREe0fWr8B3znTOKOn3js8zr0yU1FT-a0u3D5ZCRABZtgcKMM3bmTf2NzPXSGerNYjqv_Py4k8nR5uXs6VCy6gBEWiQuSR9_MhC0FNJaLLZw/s1600/GOPR5667.jpg

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjV3mdlwf41pkcC97srIC_03kq8upqudKc5mZD29C2V5F1XaKhK1KeLZYYTOYX6Eus92mYrgpy5chiFcayDibPgwZoj9qcXEl7X13f975a2qo46qVRuJ4wwh-JFaT-cilhmqZPNSnVLvdg/s1600/GOPR2834.jpg

 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiEVkc1EdrBnnEqFbPH3MUbkUtPEs-9ijULF3EwYVrQvf28oY8a1pocmmmj3VL-bosbM4jEy0M2C9unnh535L2diJakEJ3MwqJXyRmGJJ09Df5kN7hiCBHSOSg3mPN28jnP77iir_W3EOQ/s1600/C27B5717.jpg

Wednesday, March 27, 2013

ibada takatifu ya kubariki mafuta ya Krisma na kurudiwa kwa kiapo cha mapadri, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, jana.

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1731754/highRes/482598/-/maxw/600/-/dhe7iaz/-/pengo.jpg
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, akiendesha ibada takatifu ya kubariki mafuta ya Krisma na kurudiwa kwa kiapo cha mapadri, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, jana. Picha na Emmanuel Herman.


Kiongozi wa Kanisa  Katoliki nchini, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, amewataka mapadri wa Kanisa hilo kuwa kioo kwa matendo mema kwa kila wanachokifanya kwa wengine.
Kardinali Pengo aliyasema hayo jana wakati wa misa ya sherehe ya Sakramenti ya Upadri na kubariki mafuta ya Pasaka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini humo.
Alisema ni lazima kuwa watimilifu wa kibinadamu kwa kupitia njia ya sadaka, mateso na kifo hivyo kuwataka kuwafundisha yaliyo mema na yenye kumpendeza Yesu Kristu.
“Ili kufikia ukamilifu hatuwezi kukwepa misalaba, waumini mnatakiwa kutuombea ili kuweza kumwakilisha Yesu Kristu kwa matendo yaliyo mema na ya kumpendeza,” alisema Kardinali Pengo. “Hivi sasa  shida na mahangaiko ya dunia ni mengi  lazima  kumwonyesha Yesu ili aweze kutusadia na kushinda.
“Tukianza kuangalia chanzo cha matatizo na mahangaiko yalivyo hivi sasa hatuwezi kufika na tutaangamia,” alisema Kardinali Pengo.
Alisema njia nyingine zozote ambazo zinashabikia kama anasa na ukatili haziwezi kufanikiwa, hivyo aliwataka Mapadri hao kuwahubiria amani waumini.