A
1.                  Adui  lakini po pote uendako yuko nawe.
2.                  Afahamu  kuchora lakini hajui achoracho.
3.                  Afuma hana  mshale.
4.                  Ajenga  ingawa hana mikono.
5.                  Ajifungua  na kujifunika.
6.                  Akitokea  watu wote humwona.
7.                  Akitokea  watu wote hunungunika na kuwa na huzuni.
8.                  Akivaa  nguo hapendezi, akiwa uchi apendeza.
9.                  Alipita  mtu ana bunda la mshale.
10.              Alipita  mtu mwenye kibandiko cha nguo.
11.              Aliwa, yuala;  ala, aliwa.
12.              Amchukuapo  hamrudishi.
13.              Amefunika  kote kwa blanketi lake jeusi.
14.              Amefunua jicho  jekundu.
15.              Ameingia  shimoni akiwa uchi, akatoka amevaa nguo nzuri.
16.              Amejitwika  mzigo mkubwa kuliko yeye mwenyewe.
17.              Amekaa kimya  na watoto wamemzunguka pande zote.
18.              Amekula ncha  mbili.
19.              Amevaa  joho kubwa kuliko yeye mwenyewe.
20.              Anakuangalia  tu wala halali au kutembea.
21.              Anakula  kila siku lakini hashibi na hatashiba.
22.              Anakula lakini  hajashiba na hatashiba milele.
23.              Anakula lakini  hashibi.
24.              Anapendwa  sana ingawaje ni mkali sana.
25.              Anatoka  kutembea, anakuja nyumbani anamwambia mama, ‘Nieleke’.
26.              Ashona mikeka  wala hailali.
27.              Askari  wangu wote wamevaa kofia upande.
28.              Askari wangu  wote wamevaa mavazi meusi.
29.              Asubuhi  atembea kwa miguu mine, adhuhuri kwa miwili.
30.              Atapanya mbegu  nyingi sana lakini hazioti.
31.              Atolewapo  nje hufa.
B
32.           Baba alinipa mfupa, nikautunza  ukawa fahali.
33.           Baba  ameweka mkuki nje nikashindwa kuukwea, mdogo wangu akaukwea.
34.           Babako akojoapo  hunung’unika.
35.           Babu  amefunga ushanga shingoni.
36.           Babu  anakula ng’ombe, analea fupa linakuwa ng’ombe.
37.           Babu hupiga  kelele akojoapo.
38.           Babu  mkubwa ameangushwa na babu mdogo.
39.           Babu, nyanya,  mjomba, mama, baba na watoto, mna safari ya wapi?
40.           Bak bandika, bak  bandua.
41.           Bawabu mmoja  tu asiyeogopa chochote duniani.
42.           Bibi kikongwe  apepesa ufuta.
43.           Bibi  yake hutandikwa kila siku, lakini hatoroki.
C
44.           Chakula kikuu cha mtoto.
45.           Cha ndani  hakitoki nje, cha nje hakiingii ndani.
46.           Chang’aa  chapendeza, lakini hakifikiwi.
47.           Chatembea na  hakijapata kupumzika hata nukta moja.
48.           Cheupe chavunjika  manjano yatokea.
49.           Chumba  change kina ukuta niondoa na kuusimika nitakapo.
50.           Chungu change cha  udongo hakipasuki kikianguka.
D
52.           Dada yangu akitoka kwao harudi  kamwe.
53.           Dada yangu  kaoga nusu.
54.           Drrrrrh1  Ng’ambo.
55.           Dume wangu  amelilia machungani.
F
56.           Fahali wa ng’ombe na mbuzi  wadogo machungani.
57.           Fika  umwone umpendaye.
58.           Fuko  kajifukia, mkia kaacha nje.
59.           Funga  mizigo twende Kongo.
H
60.           Hachelewi wala hakosei safari  zake.
61.           Haina miguu  wala mikono, lakini, yabeba magogo.
62.           Hakihitaji maji,  wala udongo, wala chakula; lakini chamea.
63.           Hakionekani wala  hakishikiki.
64.           Hakisimami,  na kikisimama msiba.
65.           Hakuchi  wala hakuchwi.
66.           Halemewi  wala hachoki kubeba.
67.           Hamwogopi  mtu yeyote.
68.           Hana  mizizi, nimemkata mara nyingi lakini haachi kukua.
69.           Haoni kinyaa.
70.           Hapo nje panapita  mtu mwenye miguu mirefu.
71.           Hasemi,  na akisema hatasahaulika.
72.           Hasimamishwi  akiwa na ghadhabu.
73.           Hata  inyeshe namna gani haifiki humu.
74.           Hata jua likiwaka  namna gani hakauki wala kupata joto.
75.           Hata Mzungu  ameshindwa.
76.           Hauchagui  chifu wala jumbe.
77.           Hausimiki  hausimami.
78.           Hawa  wanaingia hawa wanatoka.
79.           Hesabu  haihesabiki.
80.           Huitumia  kila siku lakini haiishi.
81.           Huku  kutamu, huku kutamu, katikati uchungu.
82.           Huku unasikia  ‘pa’ Huku unasikia ‘pa!
83.           Hula  lakini hashibi.
84.           Hulala  tulalapo, huamka tuamkapo.
85.           Humu  mwetu tuko wanne tu, ukimwona wa tano mwue.
86.           Huna macho lakini  wakamata wanyama.
87.           Hupanda  mtini na mwenye kichaa wake.
88.           Hutembea watatu.
89.           Hutoka upesi sana  lakini hasalimu.
90.           Huwafanya  watu wote walie.
91.           Huwezi  kukalia alipokalia msichana wangu mweusi.
92.           Huzikwa mmoja, hufufuka mmoja,  huzeeka wengi.
I
93.           Inaonekana mara mbili katika  dakika moja na mara moja tu katika mwaka.
94.           Ini la ng’ombe huliwa hata na  walioko mbali.
J
95.           Jembe la Wangoni haliishi.
96.           Je, unaweza,  kukua ukampita mzee wako?
97.           Jiwe  litoalo maji.
K
98.           Kaburi la mfalme lina milango  miwili.
99.           Kaka yangu  anapanda darini na fimbo nyuma.
100.       Kama kingekuwa mkuki,  ungekuta kimekwisha kuua wote.
101.       Kama unapenda, mbona  usile?
102.       Kanipa ngozi  nikapikia, kanipa nyama nikala, kanipa mchuzi nikanywa, kanipa mfupa  nikautumia.
103.       Kapanda  mti pamoja na uchawi wake.
104.       Kidimbwi  kimezungukwa na majani.
105.       Kikioza  hutumiwa, kikiwa kichungu hakitumiwa.
106.       Kila linapofika kwetu  hutanguliza makelele.
107.       Kila  mtu atapitia malango huo.
108.       Kila  mtu hata mfalme huheshimu akipita.
109.       Kila siku hupita njia  hiyo hiyo bali arudipo hatumwoni.
110.       Kileee! Hiki hapa.
111.       Kilimsimamisha chifu  njiani.
112.       Kina mikono na  uso lakini hakina uhai.
113.       Kinaniita  lakini sikioni.
114.       Kisima  cha Bimpai kina nyoka muwai, ndiye fisadi wa maji.
115.       Kisima kidogo kimejaa  changarawe.
116.       Kitendawili  change ukikitambua nitakupa hirizi.
117.       Kiti cha dhahabu  hakikaliwi na watu.
118.       Kiti  cha Sulatni hukaliwa na mwenyewe.
119.       Kiti nyikani.
120.       Kitu change asubuhi  chatembea kwa miguu mine, saa sita kwa miguu miwili, jioni kwa miguu 
           mitatu.
121.       Kiwanja kizuri lakini  hakifai kuweka mguu.
122.       Kombe  ya Sultani I wazi.
123.       Kondoo  wangu amezaa kwa paja.
124.       Kondoo  wangu mnene kachafua njia nzima.
125.       Kondoo za mtoto  zamaliza mavuno.
126.       Kufanya  kwa ridhaa mojamoja.
127.       Kuku  wangu aliangua mayai jana, lakini si kuku wala ndege.
128.       Kuku wangu amezalia  miibani.
129.       Kuku  wetu hutagia mayai mikiani.
130.       Kuna mlima mmoja usio  pandika
131.       Kuna  mtu mwenye tumbo kubwa aliyesimama nje.
132.       Kuna ziwa kubwa  ambalo limekauka na limebakiza mizizi.
133.       Kunguru akilia  hulilia mirambo.
134.       Kwenye  msitu mkubwa Napata mti mmoja tu, lakini kwenye msitu mdogo naweza  kupata miwili.
135.       Kwetu  mishale na kwenu mishale.
136.       Kwetu  twalala tumesimama.
L
137.       La mgambo limelia wakatoka weusi  tu.
138.       Likienda hulia,  likirudi halilii.
139.       Likitoka  halirudi.
140.       Liwali  amekonda lakini hana mgaga.
M
141.       Mama ametengeneza chakula lakini  hakula.
142.       Mbona kinakumeza  lakini hakikuli?
143.       Mbona  mwakunjiana ngumi bila kupigana?
144.       Mbona mwasimama na  mikuki, mwapigana na nani?
145.       Mchana  ‘ti’ usiku ‘ti’.
146.       Mdogo  lakini humaliza gogo.
147.       Mfalme  amesimika mkuki wake hapa name nikausimika wangu kando yake, baadaye 
           hatukuitambulisha tena.
148.       Mfalme hushuka kwa  kelele.
149.       Mfalme katikati  lakini watumishi pembeni.
150.       Mfalme  wetu hupendwa sana, lakini wakati wa kumwona lazima umtoe nguo zote  kwanza.
151.       Mhuni wa  ulimwengu.
152.       Mkanda  mrefu wafka mpaka pwani.
153.       Mke  wangu mfupi, lakini huvaa nguo nyingi.
154.       Mlango wa nyumba  yangu uko juu.
155.       Mlima  mkubwa wapandwa kuanzia juu.
156.       Mlimani sipandi.
157.       Mlima umezuia  kutazama kwa mjomba.
158.       Mlima  wa kupanda kwa mikono.
159.       Mlima  wa kwetu hupandwa na mfalme.
160.       Mlima wa mwenyewe  hupandwa na mwenyewe.
161.       Mpini  mmoja tu lakini majembe hayahesabiki.
162.       Msitu ambao haulii  hondohondo.
163.       Mti  mkubwa, lakini una matawi mawili tu.
164.       Mti mnyanya mti  kerekeche mti ah mti ah!.
165.       Mti  wangu una matawi kumi na mawili na kila tawi lina majani kadiri ya  thelathini.
166.       Mtoto  asemea pangoni.
167.       Mtu  mdogo mwenye miguu mirefu ambaye aweza kutembea dunia nzima kwa dakika  tano.
168.       Mvua hema na jua  hema.
169.       Mvua kidogo  ng’ombe kaoga kichwa.
170.       Mwadhani  naenda lakini siendi.
171.       Mwalimu  analala na mwanafunzi wanamsomea.
172.       Mwanamke mfupi hupiga  kelele njiani.
173.       Mwanamke  mfupi hutengeneza pombe nzuri.
174.       Mwanang’ang’a hulia  mwituni.
175.       Mwepesi,  lakini aweza kuvunja nyumba za mji wote.
176.       Mwezi wangu  umepasuka.
177.       Mzee  Kombe akitoa machozi wote hufurahi.
178.       Mzee Kombe akilia  watu hufurahi.
179.       Mzizi  wa miti hutokea mbali.
180.       Mzungu  yuko ndani na ndevu ziko nje.
N
181.       Naitumia ngazi hiyo kwa kupandia  na kushukia.
182.       Nakikimbilia  lakini sikikuti.
183.       Nakupa  lakini mbona huachi kudai.
184.       Nakwenda  msituni na mdogo wangu, lakini yeye namwacha huko.
185.       Nameza lakini  sishibi.
186.       Namkimbiza  lakini simkuti.
187.       Namlalia  lakini halii.
188.       Namwomba  atangulie lakini hukataa kabisa.
189.       Nanywa supu na nyama  naitupa.
190.       Napigwa  na mvua na nyumba ipo.
191.       Natembea  juu ya miiba lakini hainichomi.
192.       Natembea juu ya miiba  lakini sichomwi.
193.       Natembea  na wenzangu lakini tukifika kwenye nyumba mimi hukaa mlangoni.
194.       Natengeneza mafuta  lakini nimepauka sana.
195.       Natengeneza  mbono lakini alama hazionekani.
196.       Ndege wengi baharini.
197.       Ndugu wawili wafanana  sana, lakini hawatembeleani.
198.       Ngoja nikumbuke.
199.       Ng’ombe wa baba  watelemka mtoni.
200.       Ng’ombe  wa babu huchezea miambani.
201.       Ng’ombe  za babu zikienda machungani hulia, zikirudi hazilii.
202.       Ng’ombe za babu  zinalala na mkia nje.
203.       Ng’ombe  wamechanganyika nikakosa wa kwangu.
204.       Ng’ombe wangu ni  weupe kwatoni.
205.       Ng’ombe  wangu wote hunywa maji isipokuwa mmoja.
206.       Ngozi ndani nyama  juu.
207.       Nguo ivaliwayo  kila siku isiyoingiwa na chawa.
208.       Nikicheka kinacheka,  nikinuna kinanuna.
209.       Nikienda  arudi, nikirudi aenda.
210.       Niiita  ‘baba’ huitika ‘baba’.
211.       Nikija  kwenye ndege wananifukuza, na nikienda kwenye wanyama hawanitaki.
212.       Nikimpiga huyu huyu  alia.
213.       Nikimpiga  mambusu.
214.       Nikimwita  hunijibu nani.
215.       Nikipewa  chakula nala bali natema.
216.       Nikitembea  walio wafu huniamkia na walio hai hukaa kimya.
217.       Nikitembea yuko,  nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayupo.
218.       Ni kitu gani ambacho  kutoa ni kuongeza?
219.       Nikitupa  mshale wangu mchana huenda mbali sana, lakini niutupapo usiku hauendi  mbali.
220.       Nikiwaambia  ondokeni hukataa, lakini mjomba akitokea wote hukimbia.
221.       Nilijenga nyumba  yangu nikaiacha bila kuiezeka majani; lakini niliporudi nilikuta  imekwisha 
           ezekwa  majani.
222.       Nilijenga  nyumba yangu yenye mlango mmoja.
223.       Nilimkata alafu  nikamridhia.
224.       Nilimtuma  askari vitani akaniletea kondoo mweusi.
225.       Nilipandia majanini  nikashukia majanini.
226.       Nilipigwa  na tonge la ugali la moto nilipopita msituni.
227.       Nilipitisha mkono  wangu chini la ardhi, nikamshika beberu mkubwa sana.
228.       Nilipoangalia kwenye  magereza ya Wazungu, nikaona wameketi juu ya mabati.
229.       Nilipofika msituni  nilikuta chungu cha pure kinachemka.
230.       Nilipoingia Rumi,  alitoka mtu na wake kumi; kila mke na tundu kumi, kila tundu na kuku 
           kumi; kila kuku na mayai  kumi. Mayai, kuku, tundu, wake, kumi kumi kumi. Wangapi 
           walikwenda Rumi?
231.       Nilipo, juu kuna  miiba na chini vivyo hivyo; lakini sichomwi.
232.       Nilipokuwa mchanga  nilikuwa na kijikia lakini sasa sinacho.
233.       Nilitembea na  mwezangu naye hupita vichakani.
234.       Nimechoma fimbo yangu  pakabaki pa kushikia tu.
235.       Nimefyeka  mitende yote kiungani isipokuwa minazi miwili tu.
236.       Nimejenga nyumba babu  akaihamia kabla mimi sijahamia.
237.       Nimekata mti, akaja  samba mwekundu akaukalia.
238.       Nimekata  mti bara ukaangusha matawi pwani.
239.       Nimekwenda na rafiki  yangu kwa jirani, yeye akafika kabla yangu.
240.       Nimemtahiri binti  wangu akatoa damu mchana kutwa.
241.       Nimempeleka kondoo  wangu akatoa damu mchana kutwa.
242.       Nimemtuma mtu  kumwamkua mtu, yeye amekuja, Yule aliyetumwa hajaja.
243.       Nimemwacha mzee  kikongwe mtoni anangojea mgeni kulaki.
244.       Nimempandikiza mti  wangu ukapeleka matawi ng’ambo ya mto.
245.       Nimesimama mbali  nyikani lakini naonekani.
246.       Nimetembea  kitambo, kukumbuka sikufunga nyumba.
247.       Nimetoka kutembea  kutembea, nikashika ng’ombe mkia.
248.       Nimetupa mshale  angani wala sitambui utateremsha ndege wa namna gani.
249.       Nimeweka ndizi yangu,  asubuhi siioni.
250.       Nimezaliwa  na mguu mmoja.
251.       Nimezungukwa  na adui wengi, lakini siumizwi.
252.       Nina kijiti change,  nizidivyo kukikata ndivyo kizidivyo kuwa kirefu.
253.       Nina kitu change  kitumiwacho na wengine kuliko mimi.
254.       Nina kitu kizuri sana  nyumbani, lakini siwezi kukichukua.
255.       Nina kitu nipendacho  ambacho hata baba, mama, dada, kaka hata na mgeni nimpendaye sana 
           siwezi kumwazima.
256.       Nina mwezi ndani ya  bakuli.
257.       Nina ng’ombe  wangu nisipomshika mkia hali majani.
258.       Nina nyumba yangu  imezungukwa na mifupa.
259.       Nina  pango langu lilojaa mawe.
260.       Nina  watoto wangu hamsini na wote nimewavisha visibau vyeupe.
261.       Nina watoto watatu,  mmoja akitoka kazi haifanyiki.
262.       Nina badilika umbo  langu baada ya kila muda mfupi.
263.       Ninachimba mizizi ya  mti usio na mizizi.
264.       Ninacho,  nakitumia, lakini kila nikitumiapo, sikiharibu ila nakipa rangi.
265.       Ninakula vitu vyote  vinono lakini sikui wala sinenepi.
266.       Ninakwenda naye na  kurudi naye.
267.       Ninao  mlima ambao una msitu kileleleni tu.
268.       Nitokeapo kila mmoja  asema namtazama yeye tu.
269.       Njia  yapitwa siku zote lakini haina alama.
270.       Njoo hapa nije hapo.
271.       Nne nne mapaka pwani.
272.       Nusu mfu nusu hai.
273.       Nyama ndogo  imewashibisha wengi wala isiishe.
274.       Nyama ya Reale haijai  kikombe.
275.       Nyanya  yako ana huruma kukubeba ulalapo.
276.       Nyumba yangu ina  makuti tele, lakini mvua ikinyesha huvuja.
277.       Nyumba yangu ina  milango mimgi.
278.       Nyumba  yangu ina nguzo moja.
279.       Nyumba  yangu kubwa, haina mlango.
280.       Nyumba  yangu kubwa, haina taa.
281.       Nyumba  yangu kubwa hutembelewa mgongoni.
O
282.       Oh!
283.       Ondoka nikae.
P
284.       Paa alipenga hata pua ikapasuka.
285.       Palikuwepo watu  watatu wakivuka mto. Mmoja alivuka pasipo kukanyaga maji wala kuyaona; 
           wa pili aliyaona maji lakini  alivuka bila kuyakanyaga; wa tatu aliyaona na kuyakanyaga alipovuka.
Ni nani hawa?
286.       Panda ngazi polepole.
287.       Para hata Maka.
288.       Pete ya mfalme ina  tundu katikati.
289.       Poopoo  mbili zavuka mto.
290.       Po  pote niendako anifuata.
R
291.       Rafiki yangu ana mguu mmoja.
292.       Reli yangu hutandika  ardhini.
293.       Ruka Riba.
S
294.       Shamba langu kubwa lakini mavuno  hayajazi kiganja.
295.       Shamba  langu miti mitano tu.
296.       Shangazi  yangu ni mrefu sana lakini hafikii tumbo la kondoo.
297.       Sijui aendako wala  atokako.
298.       Sijui  afanyavyo.
299.       Sina  dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa babangu. Ni nani  huyo?
300.       Subiri kidogo!
301.       Sultani alipiga mbiu watu waje  kufanya kazi yake lakini wakashindwa.
T
302.       Taa ya bure.
303.       Taa ya Mwarabu  inapepea.
304.       Tajiri  aniweka mfukoni na maskini anitupa.
305.       Tandika kitanga tule  kunazi.
306.       Tangu kuzaliwa  kwake sijamwona asimame wala kukimbia.
307.       Tatarata mpaka  ng’ambo yam to.
308.       Tatu  tatu mpaka pwani.
309.       Tega  nikutegue.
310.       Teke  teke huzaa gumugumu, na gumugumu huzaa teke teke.
311.       Tengeneza kiwanja  kikubwa kabila Fulani lije kupigania.
312.       Tonge la ugali  lanifikisha pwani.
313.       Tukate  kwa visu ambacho hakitakatika.
314.       Tulikaribishwa mahali  na mdogo wangu, yeye akaanza kushiba kabla yangu.
315.       Tuliua ng’ombe na  babu, kila ajaye hukata.
316.       Tuliua  ng’ombe wawili ngozi ni sawasawa.
317.       Tumvike mwanamke huyu  nguo.
318.       Tunajengajenga  matiti juu.
319.       Twamsikia  lakini hatumwoni.
U
320.       Ukimcheka atakucheka, ukimwomba  atakuomba.
321.       Ukimwita  kwa nguvu hasikii, lakini ukimwita polepole husikia.
322.       Ukimwona anakuona.
323.       Ukitaka kufahamu ana  mbio, mwonyeshe moto.
324.       Ukitembea  ulimwengu wote utakosa nyayo.
325.       Ukiukata haukatiki,  ukiushika haushikiki.
326.       Ukiwa  mbali waweza kumwona Fulani umatini.
327.       Ukoo wa liwali hauna  haya.
328.       Ule usile mamoja.
329.       Umempiga sungurra  akatoa unga.
330.       Unatembea  naye wote umjiao atakuona.
331.       Upande  wote umjiao atakuona.
332.       Ushuru  wa njia wa asili.
333.       Utahesabu  mchana na usiku na hutamaliza kuhesabu.
V
334.       Viti  kumi nyumbani, tisa vyakalika lakini kimoja hakikaliki.
W
335.       Wake wa mjomba kimo kimoja.
336.       Wako karibu lakini  hawasalimiani.
337.       Wanakuja  mmoja mmoja na kujiunga kuwa kitu kimoja.
338.       Wanameza watu jua  linapokuchwa.
339.       Wanamwua  nyoka.
340.       Wanangu wawili  hugombana mchana, usiku hupatana.
341.       Wanao wakati wao wa  kuringa, nao ni weupe kama barafu.
342.       Wanapanda mlima kwa  makoti mazuri meusi na meupe.
343.       Wanastarehe darini.
344.       Wanatembea lakini  hawatembelewi.
345.       Watoto  wa mtu mmoja hulala chini kila mwaka.
346.       Watoto wangu wana  vilemba, asio kilemba si mwanangu.
347.       Watoto wangu wote  nimewavika kofia nyekundu.
348.       Watoto  wangu wote wamebeba vifurushi.
349.       Watu ishirini  walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi 
           wakalimenya, wote  wakaridhirika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao?
350.       Watu waliokaa na  kuvaa kofia nyekundu.
351.       Watu  wamehama askari wekundu wakazidi nyikani.
352.       Watu wawili hupendana  sana; kati ya mchana hufuatana ingawa mmoja ni dhaifu. Usiku mdhaifu 
           haonekani tena.
353.       Watu wote ketini  tumfinye mchawi.
354.       Wewe  kipofu unaenda wapi huko juu?
Y
355.       Yaenda  mbali lakini haiondoki ilipo.
Z
356.       Zilitazamana na mpaka sasa  hazijakutana.
357.       Ziwa  dogo linarusha mchanga.
358.       Ziwa  kubwa, lakini naogelea ukingoni tu.
MAJIBU
          A
1.   Inzi
2.   Konokono
3.   Nungunungu (Kufuma ni kuchoma. Nungunungu  huchoma kwa miiba yake ingawa si sawa na mishalw ya mwindaji)
4.   Ndege
5.   Mwavuli
6.   Jua
7.   Ugonjwa
8.   Mgomba (Migomba katika kiunga hupendeza  baada ya kukwanyua majani makavu)
9.   Mkindu
10.  Inzi
11.  Papa
12.  Kaburi
13.  Giza
14.  Jua
15.  Mbegu
16.  Konokono au Koa
17.  Mgomba (Shina la mgomba huzungukwa na  machipukizi)
18.  Wali
19.  Kaburi ( KAburi ni kama joho la mauti)
20.  Picha
21.  Mchanga
22.  Ardhi
23.  Mauti
24.  Moto
25.  Kitanda (Kueleka ni kuchukua mgomgoni)
26.  Maboga (Tunda la mboga hukaa chini ya  majani yake)
27.  Mahindi
28.  Chunguchungu
29.  Fedha
30.  Mvua (Matone yake ni kama mbegu  azitapanyazo mkulima)
31.  Samaki
          B
32.  Muwa (Kipande cha muwa kikipandwa hutokea  muwa mkubwa)
33.  Sisimizi
34.  Mawingu (Baba mawingu huleta mvua na  ngurumo)
35.  Mtama au  Nazi
36.  Muwa (Taz. 32 juu)
37.  Mvua (Taz 34 juu)
38.  Mti na Shoka
39.  Siafu
40.  Nyayo
41.  Mlango (BAwabu ni mngoja mlango)
42.  Kope za macho
43.  Kinu cha kutwangia
C
44.  Usingizi 
45.  Nyama na mfupa 
46.  Jua 
47.  Mwezi au Jua
48.  Yai
49.  Pazia
50.  Mjusi au panya
51.   Dunia na mbingu
D
52.   Jani likwanyukapo 
53.  Jiwe mtoni
54.  Daraja la buibui
55.   Radi
F
56.   Mwezi na nyota angani
57.  Kioo
58.  Kata mtungini 
59.   Mikia ya mbwa
H
60.  Jua
61.  Maji
62.  Nywele
63.  Hewa
64.  Moyo
65.  Kula
66.  Ardhi
67.  Njaa
68.  Ukucha
69.  Mvua
70.  Mvua
71.  Kalamu
72.  Upepo au Mvua
73.  Kwapani
74.  Pua ya Mbwa
75.  Mauti
76.  Utelezi
77.  Mkufu
78.  Nyuki mzingani
79.  Nyota
80.  Miguu
81.  Jua (Jua ni kali zaidi wakati wa mchana  kuliko asubuhi au jioni)
82.  Mkia wa  kondoo
83.  Sindano
84.  Jua
85.  Matendegu ya Kitanda
86.  Ndoana
87.  Kivuli
88.  Mafiga
89.  Kuku (Kuku akifunguliwa asubuhi hukimbia  nje upesi bila kusalimu)
90.  Moshi
91.  Chungu jikoni
92.   Mbegu na matunda
I
93.  Herufi ‘K’; 
94.   Kifo
J
95.  Miguu (yaani Nyayo)
96.  Nywele kichwani
97.   Macho
K
98.        Kata ya kuchukulia  mizigo kichwani
99.        Paka  na mkia wake
100.    Kizingiti  cha mlango
101.    Ulimi
102.    Nazi
103.    Tumbako inaponuswa puani
104.    Macho
105.    Maziwa
106.    Mvua (Taz. 34 juu)
107.    Kifo
108.    Mlango
109.    Jua
110.    Kivuli
111.    Chawa
112.    Saa
113.    Mwangwi
114.    Taa ya Utambi (Utambi ndio nyoka mkali  anayemaliza mafuta ya taa ambayo ni maji ya 
   kisima  Bimpai)
115.    Kinywa  na meno
116.    Mimba
117.    Moto
118.    Kuku aatamiapo mayai
119.    Uyoga
120.    Maisha ya binadamu (Mtoto mchanga  hutambaa na halafu hutembea na mzee kutumia 
   mkongojo)
121.    Kipara
122.    Kisima
123.    Mhindi
124.    Konokono
125.    Jiwe la kusagia 
126.    Kuska mkeka
127.    Nyoka au samaki
128.    Nanasi au chungwa
129.    Matunda
130.    Nafasi kati mdomo na pua (Ulimi hauwezi  kugusa pua)
131.    Ghala
132.    Chongo
133.    Mtoto akililia maziwa
134.    Watoto wa ng’ombe na muzi
135.    Mikia ya panya
136.     Nguzo za nyumba
L
137.    Chunguchungu
138.    Debe ama buyu
139.    Neno
140.     Sindano
M
141.    Chungu cha kupikia
142.    Nyumba
143.    Mafiga
144.    Katani
145.    Mlango
146.    Mchwa
147.    Kohozi
148.    Mvua (Taz. 34 juu)
149.    Moto na mafiga
150.    Hindi
151.    Inzi
152.    Njia
153.    Hindi
154.    Shimo la mchwa
155.    Sima (ugali)
156.    MAji
157.    Kisogo
158.    Sima
159.    Nafasi kati yam domo na pua ya ng’ombe
160.    Buibui na utando wake
161.    Mkungu wa ndizi
162.    Mimba
163.    Kichwa na masikio
164.    Ngoma na upatu
165.    Mwaka
166.    Ulimi mdomoni
167.    Mawazo
168.    Kobe
169.    Jiwe
170.    Jua
171.    Kinyesi na inzi
172.    Kunguru
173.    Nyuki
174.    Shoka (Mwanang’anga ni ndege aliaye  mwituni kama shoka.)
175.    Tufani
176.    Kweme (Tunda la mkweme)
177.    Mvua 
178.    Mvua
179.    Siafu
180.     Hindi
N
181.    Mwiba
182.    Njia
183.    Tumbo
184.    Kinyesi
185.    Mate
186.    Kivuli
187.    Kitanda
188.    Kisigino
189.    Muwa
190.    Matunda ya pua au kwapa
191.    Miiba
192.    Ulimi (Miiba hapa ni meno)
193.    Mbwa
194.    Mzinga wa nyuki kwa nje
195.    Mzinga wa nyuki
196.    Nyota
197.    Macho
198.    Boga change
199.    Mawe mtoni
200.    Mijusi
201.    Vibuyu
202.    Viazi vitamu udongoni
203.    Pesa au nyayo
204.    Katani
205.    Fimbo ya kuchunga
206.    Firigisi (tumbo la kuku au ndege)
207.    Nyusi (Nywele zinazoota penye sehemu ya  uso inayotokeza kwa juu ya macho)
208.    Kioo
209.    Kivuli majini
210.    Mwangwi
211.    Popo
212.    Utomvu wa papai
213.    Puliza kidole wakati unapojikwaa
214.    Mwangwi
215.    Shoka
216.    Majani makavu na mabichi
217.    Kivuli
218.    Shimo
219.    Jicho
220.    Umande na jua
221.    Mahindi machanga
222.    Jani la mgomba la nchani
223.    Kupanda mbegu
224.    Fuko
225.    Mwiba
226.    Manyingu
227.    Kiazi kikuu
228.    Pelele
229.    Mzinga wa nyuki
230.    Hakuna
231.    Ulimi kinywani
232.    Chura
233.    KIvuli
234.    Njia
235.    Masikio
236.    Mjusi
237.    Utomvu
238.    Nzige
239.    Sauti ya njuga
240.    Kivuli
241.    Mgomba
242.    Kuangua tunda ama nazi
243.    Mtego
244.    Kivuli
245.    Moto
246.    Dirisha ama ufa
247.    Kata
248.    Mimba
249.    Nyota
250.    Uyoga
251.    Ulimi na meno
252.    Maisha (Kadiri siku zinavyopita, yaani  kukatwa, ndivyo umri unavyoongezeka)
253.    Jina
254.    Dada (Si kawaida mtu kuoa dada yake)
255.    Mke
256.    Maziwa
257.    Jembe
258.    Mdomo
259.    Kinywa
260.    Kunguru
261.    Mafiga
262.    Kivuli
263.    Jiwe
264.    Maji na mkojo (Mkojo unadhaniwa kuwa  maji yaliyobadilika rangi baada ya kupita mwilini)
265.    Chungu cha kupikia
266.    Kivuli
267.    Kichwa
268.    Jua ama mwezi
269.    Njia ya jua au mwezi angani
270.    Kiraka
271.    Matendegu
272.    Sungura alalapo
273.    Kinoo
274.    Mkufu
275.    Kitanda
276.    Mwembe
277.    Kichunguu
278.    Uyoga
279.    Yai
280.    Kaburi
281.     Konokono (Nyumba yake iko mgongoni wakati wote)
O
282.    Mwanamke aliyevunja chungu, mshangao  wake 
283.    Maji ya mfereji
P
284.    Mbarika
285.    Wa kwanza ni mtoto tumboni mwa mamake,  wa pili ni mtoto aliyebebwa mgongoni, wa tatu 
   ni  mama mwenyewe
286.    Sima ya  ugali
287.    Utelezi
288.    Kata ya kuchukulia mizigo
289.    Macho (Popoo ni tunda la mti uitwao  mpopoo)
290.    Kivuli
R
291.    Uyoga 
292.    Siafu
293.     Maiti
S
294.    Nywele kichwani (Nywele zikikatwa, hata  kichwa kikubwa namna gani, zafumbatika kwa 
   kiganja  cha mkono.
295.    Mkono  wa vidole
296.    Njia
297.    Upepo
298.    Nyoka apandavyo mtini
299.    Mtoto wangu
300.    Miiba (Mtu akichomwa na mwiba husubiri)
301.    Maji
T
302.    Jua au mwezi
303.    Kilemba
304.    Makamasi (Tajiri hutumia kitambaa cha  mfukoni kupenga makamasi, lakini maskini 
   hupenga  kwa mkono na kutupa)
305.    Nyota
306.    Mkufu
307.    Utando wa buibui
308.    Mafiga
309.    Mwiba
310.    Mhindi ama yai
311.    Mbono
312.    Jicho
313.    Maji
314.    Kucha
315.    Kinoo
316.    Mbingu nan chi
317.    Kuezeka nyumba
318.    Mpapai
319.     Sauti
            U
320.    Mwangwi
321.    Fisi
322.    Jua
323.    Kinyonga
324.    Mwamba
325.    Moshi
326.    Tundu la sindano
327.    Wanyama
328.    Kifo
329.    Tunda la mbuyu
330.    Fimbo ama bakora
331.    Kinyonga
332.    Kujikwaa
333.     Nywele
V
334.    Moto
W
335.    Vipande  vya kweme
336.    Nyumba  ama kuta zinazoelekeana
337.    MAtone  ya mvua
338.    Nyumba
339.    Watu wanaotwanga
340.    Mlango
341.    Nyota
342.    Vipepeo
343.    Panya
344.    Macho
345.    Maboga
346.    Fuu
347.    Jogoo
348.    Vitovu
349.    Waliopanda ni vidole vya miguu na  mikono, walioona ni macho wawili, waliochuma ni 
   vidole  vitano vya mkono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na  aliyelila ni 
   mdomo.
350.    Kuku, katani au mahindi
351.    Viroboto
352.    Kivuli
353.    Kula ugali
354.     Mkweme
Y
355.    Njia
Z
356.    Kingo za mto
357.    Chungu jikoni
358.     Moto
 
