
Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda akisaini kitabu cha 
wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, kabla ya kuanza ziara yake ya 
siku tatu (3) kutembelea Viwanda mkoani Tanga.
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda akionesha kukubaliana 
na Maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha kuzalisha mifuko na maturubai
 cha Pee Pee kilichopo mkoani Tanga.
  
 
 
Mashine za kisasa za kusaga na kupanga unga katika viwango mbalimbali 
zilizopo katika Kiwanda cha Unga cha Pembe kilichopo mkoani Tanga.
 

Mgodi wa malighafi za kuzalisha saruji (limestone) ambao umekuwa ukitoa 
malighafi hizo tangu kuanzishwa kwa Kiwanda hicho miaka zaidi ya 30 
iliyopita. Tafiti zinaonesha kuwa, malighafi hiyo itaendelea kupatikana 
kwa zaidi ya miaka 130 ijayo.