Abayo aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya matokeo
 ya darasa la saba mwaka jana wilayani hapa kuwa mabaya, baada ya 
asilimia 18 ya wanafunzi waliofanya mtihani ndiyo waliofaulu kujiunga 
kidato cha kwanza.
Alitoa taarifa hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita 
kwenye mkutano na walimu wa shule za msingi na sekondari, uliofanyika 
katika kata tano za Kwediboma, Mabaranga, Negero, Kikunde na Songe.
Ofisa huyo akiwa ameambatana na Mkuu wa wilaya 
hiyo, Suleiman Liwowa  na Katibu Tawala Msaidizi Elimu Mkoa wa Tanga, 
Ramadhani Chomola walisema  walitarajia kupata matokeo hayo.
Alisema walitarajia watoto wengi kushindwa 
kutokana na kuongeza udhibiti katika usimamizi wa mitihani kitaifa kwa 
darasa la saba, kwa kuziba mianya inayotumiwa na baadhi ya walimu wasio 
waaminifu kuwapa majibu watahiniwa.
Abayo aliapa kuendelea kuwa mkali kwa walimu wanaowafanyia mitihani watoto ili wafaulu.
Mwalimu Ali Mganga wa Shule ya Msingi Kikunde, alipendekeza mitihani ya kitaifa ikishafanywa ipelekwe shuleni ili wanafunzi na walimu waweze kutambua walipojikwaa.
Mwalimu Ali Mganga wa Shule ya Msingi Kikunde, alipendekeza mitihani ya kitaifa ikishafanywa ipelekwe shuleni ili wanafunzi na walimu waweze kutambua walipojikwaa.
Hata hivyo, Mwalimu Mganga alitupia lawama kwa 
watungaji mitihani ya taifa  kwamba, haieleweki hivyo inachangia kwa 
kiwango kikubwa kufeli kwa watoto.
Naye Mwalimu Bakari Mwaliko wa Shule ya Msingi 
Mabaranga, Tarafa ya Mswaki, alishauri Serikali kuwachunguza watu 
waliosahihisha mitihani ya wanafunzi wa msingi na sekondari, akihisi 
huenda kuna hujuma za kisiasa.
 
