
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye amesema haziamini 
tafiti zinazotolewa na Syonovate akidai hazina ukweli wowote.
Katika
 maoni yao, baadhi ya wasomi kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu 
nchini walieleza wasiwasi wao kuhusu usahihi wa matokeo hayo na kuhoji 
mbinu zilizotumika wakisema inawezekana hazikuwa sahihi.
Mhadhiri wa 
Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo 
ameuponda akisema haukufuata misingi ya sayansi ya siasa.
Dk Makulilo alisema alifanya utafiti kwa 
kampuni zinazofanya tafiti kama hizo kati ya mwaka 2010 hadi 2011 na 
kugundua udhaifu mkubwa katika kampuni hizo.
“Kwanza wanakosea, kwa mfano wanaposema kuwa 
utafiti huu ni mwendelezo wa ule uliofanyika Desemba 5 hadi 18, 2011. 
Ukichunguza utakuta data hizo hazipo. Zilizopo ni za Mei 2 hadi 19, 
2011.”
“Kwa kawaida uelewa wa wananchi wa vijijini ni
 mdogo ukilinganisha na mijini kwa sababu mijini kuna vyombo vya habari.
 Kwa mfano, ukiangalia swali la nani anafaa kuwa Rais, mwaka 2011 
walisema Dk Wilbrod Slaa alikuwa na asilimia 42, lakini sasa ana 
asilimia 17.
Vijijini wengi bado wanaikubali CCM kutokana 
na uelewa mdogo, iweje Dk Slaa ambaye chama chake hakina wafuasi wengi 
vijijini ashinde?” alihoji.
“Utafiti wa Synovate una dosari kubwa 
kisayansi, hauonyeshi tarehe wala wapi umefanyika. Waliohojiwa 
wameonyeshwa umri wao, lakini hawaelezwi maoni yao kulingana na umri, 
jinsia, wanatoka vijijini na mijini. Nilipofanya utafiti wangu 
niliwafuata wakakimbia…” alisema Dk Makulilo.
Mhadhiri mwingine wa UDSM, Profesa Gaudence 
Mpangala alisema nyakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu, tafiti nyingi 
hufanyika zikiwa na malengo ya kubeba watu au chama fulani.
Hata hivyo, alisema kilichofanywa na Synovate 
ni utafiti hivyo kwa kuwa yeye hajafanya utafiti ni vigumu kuupinga moja
 kwa moja... “Ila kwa mtizamo wa kawaida unatia shaka.”