Parokia hii ipo katika mji wa Korogwe. 
        Ilianzishwa mnamo mwaka 1937 na Mapadre wa shirika la Roho Mtakatifu. 
        Mwaka 1948 Padre Benedict Forsyth aliteuliwa kuwa paroko wa Kilole. Mwaka 
        1976 parokia ya Kilole ilikabidhiwa kwa Mapadre wazalendo wa Jimbo la 
        Tanga. Na Padre Odillo Mtoi aliteuliwa kuwa paroko wa kwanza wa Kilole. 
      
Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wakatoliki mjini 
        Korogwe. Parokia ya Kilole ilimegwa na kuanzishwa kwa parokia nyingine 
        mjini Korogwe. Parokia hii mpya inaitwa parokia ya Mt. 
        Augustino Manundu. Mapadre walioishi parokiani Kilole waliendelea 
        kotoa huduma katika parokia ya Manundu mpaka Manundu ilipopatiwa Paroko 
        wake.
Masista 
        wa mama yetu wa Usambara wanatoa huduma ya kufundisha katekesi katika 
        shule za msingi zilizopo mjini Korogwe.
Parokia ya Kilole ni moja ya makanisa ya hija Jimboni 
        Tanga. hii ni parokia pekee ambayo mapadre wazalendo wanazikwa katika 
        parokia hii.
Parokia ya kilole imezalisha mapadre wafuatao: Severine 
        Msemwa, Severine 
        Yagaza, Nemes Kiama 
        na Gerald Kabarega.
Kwa sasa Paroko wa parokia hii ya Kilole ni Pd. Josefu 
        Sekija.
 Parokia 
              inavigango vifuatavyo:
| 
 | 
 
 
No comments:
Post a Comment