zimebainika kwamba zipo madukani
Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) 
wamelazimika kufanya msako mkali kwenye baadhi ya maduka ya dawa jijini 
Dar es Salaam baada ya kubainika kwamba tayari kondomu hizo zipo sokoni.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es 
Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Leandri Kinabo alizitaja kondomu 
hizo kuwa ni aina ya Melt Me zenye thamani ya Sh222.1   milioni 
zilizokamatwa tangu Oktoba 23 mwaka huu na kuzuiliwa bandarini hapo kwa 
taratibu zaidi za kisheria.
“Jambo lililotushtua ni kwamba zimebainika kwamba 
zipo madukani, tukajaribu kufuatilia tena bandarini tukifikiri kuwa 
huenda zimetolewa kinyemela licha ya kuzuiliwa ili ziteketezwe au 
zirejeshwe nchini India kwa gharama zao wahusika.
Tulipokwenda bandarini tukabaini kwamba bado zipo 
katika hali ile ile, kumbe  zimeingizwa nchini kwa njia ya panya, kwa 
kweli ni mbovu na ndiyo maana tumelazimika kuwajulisha wanahabari ili 
muwape taarifa wananchi wawe makini,” alisema Kinabo.
Alifafanua zaidi kwamba kondomu hizo ni mbovu 
kwani zimebainika kuwa na vitundu, pia zinapasuka haraka, hazina kabisa 
viwango vya ubora wa bidhaa unaotakiwa na Shirika la Viwango la 
Kimataifa (ISO).
Kinabo alisema kuwa TBS bado wanaendelea kufanya 
mawasiliano na kampuni iliyotengeneza kondomu hizo, lakini kwenye kasha 
 lake inaonyesha kuwa inaingizwa nchini na kampuni ya Fair Deal Exim ya 
Dar es Salaam.   
 
 
No comments:
Post a Comment