MCHEKESHAJI 'pacha' na marehemu Sharo Milionea, Musa Kitale 'Teja'
FAMILIA ya Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ aliyefariki dunia Novemba 26, mwaka huu kwa ajali ya gari iliyotokea Songa-Kibaoni, Muheza, Tanga imemteua msanii wa vichekesho Musa Kitale kuwa mwangalizi wa mali za marehemu.
Alisema
 amepewa jukumu la kuhakikisha mikataba yote  ambayo marehemu aliifanya 
na makampuni mbalimbali inakwenda vizuri  sanjari na kuangalia mali kama
 vile gari na samani za ndani ya nyumba.
“Nimeambiwa
  nisimamie mikataba, niangalie mali za mshikaji (Sharo) kwa kipindi  
chote cha kusubiria arobaini ya marehemu ambayo itafanyika Januari 4,  
2013 kijijini alikozikwa,” alisema Kitale.
Kitale
 alisema baadhi ya  mikataba anaifahamu kwa vile yeye ndiye aliyekuwa 
shahidi, “lakini wa  DTV  aliosaini siku tano kabla ya kufariki dunia 
(hakuutaja) inabidi  aushughulikie Muddy Suma jamaa aliyemuazima gari 
marehemu,” alisema.
Kuhusu kwenda kuzima taa katika nyumba aliyokuwa akiishi marehemu, Sinza Palestina Dar, Kitale alisema:
“Kwa
  kipindi hiki ambacho tunasubiri arobaini ya marehemu ifike ni ngumu 
mtu  kwenda kufungua mlango ili azime taa, namuomba mama mwenye nyumba  
avumilie kwani zoezi la kufungua mlango wa kwa Sharo ni hadi familia  
yake iwepo hapa Dar na si mimi peke yangu.”
Akakumbuka
 jambo hili:  “Tulishtushwa na taarifa  tulizozisoma kwenye Gazeti la 
Risasi Jumamosi  iliyopita kuwa, kuna rafiki mmoja wa marehemu alikwenda
 pale nyumbani na  kutaka kutapeli vitu vya marehemu, kama isingekuwa 
msimamo wa  mwenye  nyumba jamaa angefanikisha utapeli wake ndiyo maana 
haraka sana familia  ikanipa mimi jukumu hili.”
 
 
No comments:
Post a Comment