Kihistoria
 Mkoa wa Tanga ulitumiwa sana na wakoloni wa Kireno, Kiarabu, Kijerumani
 na Kiingereza ikiwa lango la biashara na uchumi kwa kuunganisha sehemu 
za ndani za Afrika Mashariki  na Kati na sehemu mbalimbali za Dunia
 hii ni ofisi ya mkuu wa mkoa wa tanga maeneo ya masiwani
kupitia
 bahari ya Hindi. Mwaka 1840 eneo  la  Manga  lilikuwa  njia  waliopitia
 wafanyabiashara  kutoka  Bara  Arabu  waliokuja kutafuta meno ya tembo 
 na  watumwa. Waarabu walikuwa wakiacha vyombo vya usafiri (majahazi) 
eneo la Sadani (Bagamoyo) na kuanza safari kupitia Manga, Kimbe hadi 
Kondoa Irangi. Misafara mingine ya  wafanyabiashara ilianzia Unguja 
kupitia Pangani, Kiwanda (Sindeni), Ngugwini, Mbego, Kwediboma, Mgera 
hadi Kondoa Irangi ambapo walileta nguo, shanga na vitu ili 
 kubadilishana  na  pembe  za ndovu, watumwa, chakula na mifungo. 
Kutokana na mwingiliano wa tamaduni mbalimbali, wenyeji wa Tanga 
wamerithi tamaduni, lugha na ustaarabu  wa mataifa  mbalimbali ya 
Washirazi, Waarabu,  Wachina, Wahindi, Wareno, Wajerumani, Waingereza na
 Waswahili.
Mkoa
 wa Tanga ni mzizi na chimbuko la Tanganyika kabla ya kuungana na visiwa
 vya Unguja na Pemba mwaka 1964 na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa 
Tanzania. Tanganyika ilipata Uhuru mwaka 1961 huku Mkoa wa Tanga ukiwa 
ni msafirishaji mkubwa wa zao la Mkonge  duniani  na  mhimili  wa  kukua
 kwa uchumi  wa  nchi.  Jina  Tanga  lilitolewa  na wafanyabiashara  wa 
 Kishirazi  likiwa  na maana  nne  ambazo  ni  Tambarare,  Mabonde  ya 
Kijani, Barabara za Milimani na Kilimo cha  Milimani. Neno nyika ni la 
kibantu ambalo lilikuwa likitumiwa sana na wenyeji wakimaanisha mbuga au
 pori zaidi ya jina Tanga.
Harakati
 za kudai Uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza zilifanikiwa na 
Tanganyika kupata   Uhuru tarehe 9 Disemba, 1961 chini ya uongozi wa 
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya chama cha TANU. Wakati 
huo (1961) Mkoa wa Tanga ulikuwa ni Jimbo lenye Wilaya tano (5) ambazo 
ni Wilaya ya Tanga, Handeni, Pangani, Usambara na Same.

 
 
No comments:
Post a Comment