Friday, September 28, 2012

NGOMA YA BAIKOKO YENYE ASILI YA MKOA WA TANGA

Raha Za Ngoma Ya Baikoko Kutoka Tanga Inavyopagawisha Kwa Mauno na Manjonjo
 
 Ngoma ya Baikoko ni ngoma ya kiasili kutoka mkoa wa Tanga nchini Tanzania inayoambatana na uchezaji wa kina dada kukata nyonga kwa ustadi mkubwa au kama inavyojulikana na wengi kukata viuno au mauno.

 

 Ngoma hii ambayo imeanza kujipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kutokana na manjonjo yake wakati wa uchezaji wake.Ustadi na uhodari wa ukataji viuno kwa wachezaji wa ngoma hiyo ni kivutio kikubwa sana kwa mtizamaji yeyote. Viuno vya akina dada hao ambavyo ni laini mithili ya kukosa mifupa hutoa burudani tosha kwa wengi.Mkoa wa Tanga nchini Tanzania unasifika kwa akina dada wenye mauombo ya kuvutia huku wakiwa na uwezo mkubwa pia katika ukataji wa nyonga au viuno.

No comments:

Post a Comment