Monday, December 31, 2012

Much Better In Time,Happy New Year 2013 Watanzania Wote Kutoka Watu Milioni 34.4 Hadi Kufikia Watu Milioni 44.9!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete Ametangaza Matokeo Ya Sensa Ya Watu Na Makazi Ambapo Watanzania Waongezeka Kutoka Watu Milioni 34.4 Hadi Kufikia Watu Milioni 44.9,Rais Kikwete Awataka Watanzania Kupunguza Kasi Ya Kuzaliana.

Ramani ya Tanzania.
 
Tanzania bara kuna watu 43.6 milioni na Zanzibar watu 1.3milioni.
 http://1.bp.blogspot.com/-AcVRFFHSi4k/UOHHdp_wRbI/AAAAAAAANGw/WH1Hq0G5m6U/s1600/idadi+.jpg

 Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja  kwenye bango linaloonyesha idadi ya watu Tanzania na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Akizungumza katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa uzinduzi huo, Rais Kikwete ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali wa kitaifa, alisema kuwa matokeo hayo ni ishara kwamba ifikapo mwaka 2016 kuna uwezekano wa idadi hiyo kufikia milioni 51 jambo ambalo linaweza kuwa ni mzigo kwa taifa, jamii na hata katika masuala ya uchumi.
 Sensa hii ni ya tano kufanyika tangu Muungano ambapo ya kwanza ilifanyika mwaka 1967 na idadi ya watu ilikuwa milioni 12,313,469, bara wakiwa milioni 11,958,654 na visiwani 354,400.
Alisema kuwa sensa ya kwanza ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za mwisho zilifanyika baada ya Uhuru katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002.
Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika Agosti 2002, idadi ya watu nchini ilikuwa 34,443,603.