Tuesday, October 23, 2012

In 1988; Soni Seminary of CATHOLIC DIOCESE OF TANGA took the first position National wise in Form IV National Exam Results.


SOME COOL BEHIND THE SCENE,THE BEST TANGA RECORD


http://www.dioceseoftanga.org/pages_inswahili/offices/education/soniseminary/soniseminary2.jpg


 http://www.dioceseoftanga.org/pages_inswahili/offices/education/soniseminary/soniseminary3.jpg

 http://www.dioceseoftanga.org/pages_inswahili/offices/education/soniseminary/soniseminary1.jpg

 http://www.dioceseoftanga.org/pages_inswahili/offices/education/soniseminary/soniseminary5.jpg

 http://www.dioceseoftanga.org/pages_inswahili/offices/education/soniseminary/soniseminary4.jpg

 http://www.dioceseoftanga.org/pages_inswahili/offices/education/soniseminary/soniseminary6.jpg

In 1978 Fr. Ndunguru was sent to Dar es Salam University for further studies in teaching. Fr. Maganga took the leadership of Soni Seminary as Rector. After finishing his studies Fr. Ndunguru came back to Soni Seminary as Rector and Teacher up to 1988 when Fr. George Mhuza took his position as Teacher and Rector. Fr. George was coming from Dar es Salam University where he hired his degree in education. He became Rector for 10 years. In 1998 his position was taken by Fr. Fraternus Mbuya. Since 1998 up to 2005 Soni had different leaders who served for a very short time. These are, Fr. Fraternus Mbuya, Gerald Kabarega, Severine Msemwa, Benedict Shemfumbwa and Fr. Thomas Kiangio who started his career since 2005.
The Patron Saint was changed in the year 1979 from Saint Michael to Saint Joseph the Husband of Mary. St. Joseph was prefered due to his role in taking care of the child Jesus so as to take the same role of caring of the young Seminarians in their eary stage of formation. It was also in the same year the first form four did National Exams and came out with good results, which proved that the staff was doing a good job. Since 1979 form four result has been giving hope to the Bishop as well as the faithful of Tanga Diocese. In 1988; Soni Seminary took the first positin National wise in Form IV National Exam Results. More than that, there has been also a lot of development in buildings and in 1996 Soni had students who did form VI exams. These A-level classes were stopped in the year 1998. Now effort is made to bring back A-level classes.

Benki ya NMB Lushoto.

https://encrypted-tbn3.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcS8cgF8E-Tpkj6TjBelFhHrdSHo2bcWM9LjWfIKs-J5qiGWnlvQ

TBL Yadhamiria Kujenga Visima Handeni

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo amemkabidhi Diwani wa Kata ya Kwamgwe, wilayani Handeni, Tanga, Shariffa Abebe mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 40.5 kwa ajili ya ujenzi wa visima.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjh5KCbqkB1juk7a79uBcBadC3Zi8g8D2DP_mPRnj1JLDfJu32J1mA4-cAFxeV2SY2a_v2dif92e7YLjguhddO0S_cJgHFXR_Fcftg3Jmx8zYmo3azZtdu7qTV2rAfGYoWSOMLONCeGum5_/s400/safirri6.jpg

Maktaba iliyopo kijiji cha Lushongo wilaya ya Pangani

Mohammed Dar Muasisi wa jina la Tanzania aliyesahaulika

Saumu Mwalimu
UNAPOTAJA historia ya nchi Tanzania, ni dhahiri kwamba hutaacha kutaja majina ya wapigania uhuru na viongozi mbalimbali walioiongoza tangu enzi za ukoloni, hadi kupata uhuru.
Hata hivyo, katika kila historia ya taifa lolote iliyojengwa, kuna watu waliofanikisha historia hiyo, lakini kwa sababu moja au nyingine, michango ya baadhi yao imesahaulika na pengine kutotajwa kabisa kwenye historia hizo.
Wengi wa Watanzania tunafahamu kuwa jina la nchi yetu Tanzania, limetokana na majina ya nchi mbili zilizoungana na kuwa moja ambazo ni Tanganyika na Zanzibar. Hivi ndivyo tulivyofundishwa shuleni.
Wengine wanaamini kuwa Rais wa kwanza na muasisi wa taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ndiye aliyebuni jina la Tanzania.
Lakini ukweli ni kwamba, jina la Tanzania lilibuniwa na mmoja wa wananchi walioshiriki mchakato wa kutafuta jina la nchi hii, baadaya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Mohammed Iqbal Dar ndiye aliyebuni jina la Tanzania, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 akiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari  Mzumbe.
Ilikuwaje?
 “Nilikuwa maktaba najisomea, nilishika gazeti la Daily News, wakati huo likiitwa The Standard, ndipo nikaona tangazo hilo,” anaeleza Dar alivyopata hamasa na kuongeza:
“Siku hiyo hiyo, nikafanya majaribio ya kutafuta jina bila hata ya kuishirikisha familia yangu. Nilichuka karatasi na kalamu, lakini kabla sijaanza kufanya chochote, nilimwomba Mungu aniwezeshe kwa maana naamini Mungu, ndiye kila kitu wakati wa kufanya jambo lolote.”
“Kwa hiyo kwenye ile karatasi nikaandika Tanganyika na Zanzibar kisha, nikaandika majina yangu mawili;  Iqbal na Ahmadiya,” anasema Dar na kufafanua kuwa Iqbal ni jina lake na jina la ubini na  Ahmadiyya ndiyo dhehebu lake.
Kupata jina Tanzania
Akisimulia alivyopata jina Tanzania, anasema kuwa ilimchukua dakika tano tu kufikiria na kulipata jina hilo.
“Nilichukua Tan kutoka kwenye Tanganyika na kuongeza Zan kutoka kwenye Zanzibar na kupata Tanzan, niliona halitimii vizuri,”anasimulia Dar.
Anabainisha kuwa baadaye alifikiria na kugundua kuwa majina mengi ya nchi za Afrika yanaishia na IA mfano akitoa mfano wa Ethiopia, Gambia, Tunisia, Nigeria, Algeria, Somalia, Zambia, Namibia na kwamba baada ya kubaini hilo aliamua kuongezea herufi hizo mbili na kupata jina Tanzania.
“NIlituma maombi yangu katika shindano hilo, bila kumwambia mtu yeyote nyumbani,” anasema Dar.
Baada ya muda mfupi baba yake, mzee Tufail Ahmad Dar, alipokea barua kutoka Wizara ya Habari na Utalii (wakati huo), ambapo ndani yake kulikuwa na ujumbe wa pongezi ya kwamba kijana wake ameshinda katika shindano hilo.
“Wakati naandika, sikuwa na matumaini kama nitashinda kwa kuwa shindano hilo lilikua wazi kwa watu mbalimbali, hivyo sikuwa na tarajio lolote kama ningeshinda,
“Jioni wakati narudi nyumbani, baba mzazi alinifungulia mlango wakati si kawaida yake kwani mama ndiye alikuwa akinifungulia siku zote, hapo nikajua kuna kitu hakipo sawa. Lakini, nilikaribishwa na tabasamu la baba, pamoja na pongezi nyingi, nilifurahi sana,” anaeleza.
Tuzo
Dar anasema kuwa kwa ushindi huo, alitunukiwa ngao pamoja na fedha taslimu Sh200 kama zawadi ya ubunifu wake.
Pamoja na kuibuka mshindi wa ubunifu huo na hadi leo jina la Tanzania alilolibuni yeye linaendelea kutumika, lakini Dar anadai kuwa mchango wake huo kwa taifa ni kama hautambuliwi na Serikali imemsahau katika kuandika historia ya taifa la Tanzania.
“Sijui kwa nini sitambuliwi tangu wakati huo? Hakuna chochote kinachoelezea uhusika wangu katika kupata jina la Tanzania na ukiwauliza watu, wengi watakwambia ilikuwa ni Nyerere aliyeleta jina Tanzania, hii inaumiza,” anasema akilalamika.
Tanzania ya sasa
Baada ya miaka 13 tangu kufariki kwa Nyerere,  Dar anasema kuwa Tanzania haimtendei haki mwasisi huyo wa Taifa, ambalo ni kisiwa cha amani.
“Ni kama imepita miaka mingi sana tangu kifo chake. Watanzania wamesahau kila kitu alichokiota Mwalimu Nyerere. Nakumbuka moja ya vita kubwa aliyopigana ni dhidi ya rushwa, yeye aliichuki rushwa lakini kwa sasa, rushwa imekua kama ndiyo tafsiri ya maisha ya Tanzania. Hakuna kitu kinachoweza kufanyika kwa urahisi hata kama ni haki ya mtu, bila kutoa rushwa,” anasema.
Anaongeza kuwa: “Mwalimu Nyerere alikua ni rafiki ya baba yangu na walikua wakionana na kuongea, nakumbuka siku moja kulikuwa na sherehe nyumbani na kwa kuwa tulikuwa watoto, nilimhudumia chai Mwalimu.
“Nakumbuka Mwalimu aliwahi kumuuliza baba yangu; Lini Malaria itaisha nchini hii? Baba alimjibu kuwa, kamwe malaria haitaisha ikiwa hakutakuwa na kujitolea kwa kila mmoja wetu, bila kumtegea mwengine,” anasema.
Katika kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Dar anaishauri Tanzania iendeleze misingi ya maisha ambayo Hayati Mwalimu Nyerere aliisimmamia, ikiwamo umoja na mashikamano, ili kuondoa tofauti kubwa kati ya maskini na matajiri.
“Tunaona namna ambavyo matajiri wanendelea kuwa tajiri zaidi, wakati maskini wanazidi kudidimia. Kama kungekuwa na ushirikiano kati ya watu hawa wawili, tofauti kati yao ingekuwa ndogo au isingekuepo kabisa,” anaeleza.
Anashauri pia kuwepo na sanamu za utambulisho ya Baba wa Taifa kila mahali, ili kulienzi jina lake liishi milele. “Kwa ninavyomjua Mwalimu natamani jina lake liishi milele na litangazwe lijulikane dunia nzima,”anasema.
Mohammed Iqbal Dar aliazaliwa mwaka 1944 jijini Tanga, ni mtoto wa tatu kati ya watoto saba wa Tufail Ahmad Dar.
Dar ni baba wa mtoto mmoja, ambapo kwa zaidi ya miaka 40 sasa amekuwa akiishi nchini Uingereza alikoenda kwa ajili ya kusoma kabla ya kuwa raia wa nchi hiyo.
Mbunifu huyo wa jina la Tanzania ni Mhandisi wa Masuala ya Redio, kazi anayoifanya nchini Uingereza, akieleza kuwa katika kuienzi nchi yake, nyumba yake iliyopo mjini Birmingham, ameipa jina la Dar es Salaam, ikiwakilisha ubini wake, pamoja na Jiji la Dar es Salaam.