Saturday, December 1, 2012

Siku ya Ukimwi duniani 1/12/2012

 
Siku ya Ukimwi Duniani inakumbukwa kila tarehe ya kwanza ya mwezi Desemba. Hii ni siku maalum ya kupanua ufahamu kuhusu maafa yanayoletwa na ugonjwa wa Ukimwi. Desemba ya kwanza ya kila mwaka ilichaguliwa kuwa ni siku ya Ukimwi kutokana na tarehe hiyo kuwa ndio siku ambayo kirusi cha Ukimwi kilitambulika rasmi mwaka 1981. Toka mwaka 1981 watu zaidi ya milioni 25 wameshafariki kutokana na Ukimwi.
Siku hii ilichaguliwa rasmi mwaka 1988 wakati wa Mkutano wa Dunia wa Mawaziri wa Afya Kuhusu Mpango wa Kuzuia Ukimwi. Kuanzia hapo siku hii imekuwa ikikumbukwa rasmi na serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wanaharakati.
Toka mwaka 1988 hadi 2004, Siku ya Ukimwi Duniani ilikuwa ikiratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Ukimwi (UNAIDS). Mwaka 2005 UNAIDS ililipa shirika lisilo la kiserikali la Kampeni ya Ukimwi Duniani (the World AIDS Campaign)wajibu wa kuratibu siku hii.
Kila mwaka siku hii hukumbukwa kwa ujumbe maalum. Ujumbe wa mwaka huu 2012
"Tanzania Bila Maambukizi mapya, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi Inawezekana"