Kihistoria Mkoa wa Tanga ulitumiwa sana na wakoloni wa Kireno, Kiarabu, Kijerumani na Kiingereza ikiwa lango la biashara na uchumi kwa kuunganisha sehemu za ndani za Afrika Mashariki na Kati na sehemu mbalimbali za Dunia kupitia bahari ya Hindi.
Wednesday, February 27, 2013
SHULE TOFAUTI ZA SEKONDARI NA MAZINGIRA YAKE
MTWARA:MASASI SEC
LINDI:NGONGO SEC
MOROGORO:MANDELA SEC
DAR ES SALAAM:TWIGA SEC
PWANI:KISARAWE LUTHERAN SEMINARY
Urais 2015: Utafiti wa Synovate wapondwa,wadau wadai una ajenda ya siri
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye amesema haziamini tafiti zinazotolewa na Syonovate akidai hazina ukweli wowote.
Katika maoni yao, baadhi ya wasomi kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini walieleza wasiwasi wao kuhusu usahihi wa matokeo hayo na kuhoji mbinu zilizotumika wakisema inawezekana hazikuwa sahihi.
Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo ameuponda akisema haukufuata misingi ya sayansi ya siasa.
Dk Makulilo alisema alifanya utafiti kwa
kampuni zinazofanya tafiti kama hizo kati ya mwaka 2010 hadi 2011 na
kugundua udhaifu mkubwa katika kampuni hizo.
“Kwanza wanakosea, kwa mfano wanaposema kuwa
utafiti huu ni mwendelezo wa ule uliofanyika Desemba 5 hadi 18, 2011.
Ukichunguza utakuta data hizo hazipo. Zilizopo ni za Mei 2 hadi 19,
2011.”
“Kwa kawaida uelewa wa wananchi wa vijijini ni
mdogo ukilinganisha na mijini kwa sababu mijini kuna vyombo vya habari.
Kwa mfano, ukiangalia swali la nani anafaa kuwa Rais, mwaka 2011
walisema Dk Wilbrod Slaa alikuwa na asilimia 42, lakini sasa ana
asilimia 17.
Vijijini wengi bado wanaikubali CCM kutokana
na uelewa mdogo, iweje Dk Slaa ambaye chama chake hakina wafuasi wengi
vijijini ashinde?” alihoji.
“Utafiti wa Synovate una dosari kubwa
kisayansi, hauonyeshi tarehe wala wapi umefanyika. Waliohojiwa
wameonyeshwa umri wao, lakini hawaelezwi maoni yao kulingana na umri,
jinsia, wanatoka vijijini na mijini. Nilipofanya utafiti wangu
niliwafuata wakakimbia…” alisema Dk Makulilo.
Mhadhiri mwingine wa UDSM, Profesa Gaudence
Mpangala alisema nyakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu, tafiti nyingi
hufanyika zikiwa na malengo ya kubeba watu au chama fulani.
Hata hivyo, alisema kilichofanywa na Synovate
ni utafiti hivyo kwa kuwa yeye hajafanya utafiti ni vigumu kuupinga moja
kwa moja... “Ila kwa mtizamo wa kawaida unatia shaka.”
Subscribe to:
Posts (Atom)