Friday, September 21, 2012

WILAYA ZA TANGA NA BAADHI YA MAENEO YAKE

 TANGA
Wilaya ya Tanga ni wilaya moja ya Mkoa wa Tanga nchini Tanzania. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Tanga ilihesabiwa kuwa 243,580







MUHEZA
Kabla na baada ya Uhuru eneo la Muheza lilikuwa lipo Wilaya ya Tanga ambalo lilijulikana kwa jina la Tanga Nje mpaka mwaka 1974.   Kutokana na sababu mbalimbali mwaka 1974 eneo  la  Muheza  liligawanywa  na  kuunda  Wilaya  inayojitegemea  ambayo  ni  Wilaya  ya Muheza. Wakati Wilaya ya Muheza inagawanywa ilikuwa na Jimbo moja (1) la Uchaguzi na Tarafa sita (6) ambazo ni Bwembwera, Amani, Ngomeni, Maramba na Mkinga, Kata 35 na vijiji 174. Mwaka 1980, Wilaya iliongeza Jimbo la uchaguzi ambalo ni Mkinga na kufanya Wilaya kuwa na majimbo mawili ya  uchaguzi ambayo ni Muheza na Mkinga

Muheza


 PANGANI
Wilaya ya Pangani ni moja kati ya Wilaya kongwe tano za Mkoa wa Tanga ambayo ilikuwepo kabla na baada Uhuru. Mji wa Pangani upo Km 47 kusini mwa mji wa Tanga na ina eneo lenye  kilometa  za  mraba  (km2) 1,830.8  ambapo sehemu kubwa  ya Wilaya iko kwenye ukanda wa Pwani  na mji wake mkuu ni Pangani ambapo mto Pangani unaingia Bahari ya Hindi.
Imepakana na wilaya ya Muheza upande wa Kazkazini, Wilaya ya Handeni upande wa magharibi, wilaya ya Bagamoyo (Mkoa wa Pwani) upande wa kusini na Bahari Hindi upande wa mashariki. Makao makuu ya wilaya yako Pangani mjini.
Wilaya ina wakazi 44,107 (2002) [1]. Kuna kata (au shehia, kwa Kiingereza ni Ward) zifuatazo (idadi ya wakazi katika mabano):
 Pangani


 MKINGA
Wilaya  ya Mkinga ni  Wilaya  ya hivi  karibuni  kati  ya Wilaya nane za Mkoa wa Tanga ambayo  ilianzishwa  rasmi  mwaka 2005 baada ya kugawanywa toka  Wilaya  ya  Muheza ambayo ilianzishwa mwaka 1974.
Wilaya hii imepakana na Wilaya ya Muheza na Tanga kwa upande wa Kusini, Wilaya ya Lushoto na Korogwe upande wa Magharibi, Jamhuri ya Kenya upande wa Kaskazini na Bahari ya Hindi kwa upande wa Mashariki.

 

 KOROGWE
Wilaya ya Korogwe ilianza mwaka 1966  ambapo ilitenganishwa na Wilaya ya Lushoto. Kutokana na Wilaya ya Lushoto kuwa na eneo kubwa kiutawala, ilikuwa vigumu kutoa huduma kwa wananchi. Kabla eneo hili halijatengana na Wilaya ya Lushoto lilijulikana kama Korogwe “Sub-District” na mtawala wa eneo alikuwa ni “District Officer Incharge”.
Asili ya jina Korogwe ni jina la mmoja wa wakazi wa awali wa eneo hilo ambaye alijulikana kama Mkorogwe ambaye alikuwa ni Mzigua kwa kabila aliyeishi katika kitongoji cha Kilole- Kambi  ya  Maziwa.  Mwaka 1966  Korogwe ilitangazwa kuwa Wilaya kupitia Tangazo la Serikali Na. 429 la Mwaka 1966 (GN No.429 of 1966). Mkuu wa Wilaya wa kwanza aliitwa Rajabu Semvua, wakati huo ilikuwa na Tarafa nne (4) ambazo ni Korogwe, Mombo, Bungu na Magoma kwa kuzingatia mfumo wa Kichifu uliokuwepo kabla ya Uhuru.

 images/stories/tanga/korogwe_web.jpg


LUSHOTO
Wilaya ya Lushoto ilianza kabla ya Uhuru wa Tanganyika. Chini ya utawala wa kikoloni ambapo ilijulikana kama  Usambara. Jina la Lushoto lilitungwa/kuandikwa na Mzungu aliyewauliza wenyeji jina la eneo zima akaambiwa ni Lushoto wakimaanisha kichaka cha kujificha. Mzungu akaliandika kwenye daftari lake na akaliweka kwenye ramani kuwa eneo hilo ni Lushoto kwa kujua ndilo jina la eneo.

 Lushoto


HANDENI
 Wilaya ya Handeni imegawanywa kuwa wilaya mbili za Handeni na Kilindi,Wazigua ni mojawapo wa makabila ya asili ya mkoa wa Tanga. Wazigua ambao lugha yao ni ya jamii ya lugha za kibantu yasemekana wamekuwepo mkoani Tanga, wilaya ya Handeni kwa karne nyingi zilizopita.
Maana ya Zigua ni kuchukua au ukamata eneo. Miaka mingi iliyopita Wazigua walipigana vita na kuyashinda makabila ya Wabondei na Wasambaa. Makabila hayo yaliyoshindwa vita yalikimbiliia maeneo ya mabondeni na mengine kusambaa milimani, Wabondei huko Mabondeni, na Wasambaa walisambalia milima ya Usambara. Na ndio chanzo cha majina ya makabila haya, kwani kabla ya hapo walikuwa wakiishi pamoja kama koo za jamii moja. Na walijulikana kwa jina la Boshazi maana yake Bondei, Zigua, Sambaa.Wilaya ya Handeni pia kuna makabila mbalimbali kama Wakilindi, Wanguu, na Wasambaa. Katika karne hii ya sayansi na tekinolojia, na kutokana na utandawazi, makabila mengi ya kiafrika yamekubwa na mabadiliko yasioepukika katika mila na desturi zao.
 Handeni


 KILINDI
Kabla na baada ya Uhuru wa Tanganyika Wilaya ya Kilindi ilikuwa ni sehemu ya Wilaya ya Handeni  ambayo ilitenganishwa Julai Mosi 2002 kutokana na uamuzi wa Serikali kuigawa Wilaya Handeni.  Mkuu wa Wilaya wa kwanza alikuwa ni Mhe. Lt. (Mst) Winfred Ligubi akiwa na Mkurugenzi aitwae Anunsiata Lyimo.
Mwaka  2005  kupitia  Sheria  No 7 ya  mwaka 1982 ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi ilianzishwa na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi iliunda Baraza Kamili la Madiwani. Kwa sasa Wilaya ina tarafa 4, kata 20 na vijiji 102 zinazounda eneo la kilomita za mraba 6129 zenye kukadiriwa kuwa na watu 177,850 kwa mwaka 2011.
Wakazi wa Wilaya hii wanajishighulisha na ufugaji wa ng’ombe, mbuzi na  kondoo pamoja na kilimo cha Maharage, Mahindi, Alizeti, Ndizi, Viazi Vitamu na Mboga. Aidha, katika Wilaya hii yanapatikana madini ya dhahabu, Gypsum, “Quartz” na “Germstones”.Makabila maarufu ya wilaya hii Wakilindi na Wanguu.

Kilindi ni kati ya wilaya 7 za Mkoa wa Tanga katika Tanzania. Imepakana na wilaya ya Handeni upande wa mashariki, Mkoa wa Kilimanjaro upande wa magharibi-kaskazini na Mkoa wa Morogoro upande wa kusini.
Mwaka 2002 ilikuwa na wakazi 144,359.[1]

Tarafa

Wilaya ya Kilindi ina tarafa 15:wilaya hii inapakana na mkoa wa Manyara kwa upande wa kaskazinimagharibi
 Eneo na Rasilimali za Wilaya - Kilindi DC
 Kilindi

No comments:

Post a Comment