Friday, September 28, 2012

Halmashauri ya jiji la Tanga



 UTANGULIZI
Halmashauri ya Jiji la Tanga ni moja kati ya Halmashauri tisa za Mkoa wa Tanga. Nyingine
ni Pangani, Mkinga, Muheza, Korogwe mji, Korogwe wilaya, Lushoto, Handeni na Kilindi.
Ina eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 600 kati ya hizo kilomita za mraba 62 ni eneo
la maji (covered with wáter bodies). Halmashauri ya jiji la tanga ipo kati ya 38053’ na
39010’mashariki, na 50 na 5016’kusini, kaskazini mashariki mwa Tanzania. Eneo kubwa ni
tambarare na maeneo machache ni miinuko midogomidogo.
Idadi ya watu
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, jiji la Tanga lilikuwa na jumla ya
idadi ya watu 242,640 ambao ni karibu asilimia 14.8 ya watu wote wa mkoa wa tanga. Kati
ya hao 119,621 walikuwa wanaume (49.3%) na watu 123,019 walikuwa wanawake (50.7%)
karibu asilimia 37.5 ya watu wote walikuwa watoto chini ya miaka 15 na watu wenye uwezo
wa kufanya kazi (potential labour forcé) walikuwa ni asilimia 58.8 ya watu wote ambao walikuwa watu wenye umri kati ya miaka 15-64. Wastani wa watu kwenye kaya ilikuwa ni
karibu watu 4.6 na mtawanyiko wa watu(population density) ulikuwa ni wastani wa watu
451 kwenye eneo la kilomita ya mraba . kutokana na ongezeko la watu la asilimia 1.88 kwa
mwaka(population growth rate) jiji la Tanga kwasasa linakadiriwa kuwa na watu 292890
Hali ya hewa
Hali ya hewa ni ya ukanda wa pwani ambao una joto la wastani ya sentigredi 240C
mpaka 330C. Tanga inapata mvua ya misimu mitatu kama ifuatavyo:-
 Mvua ndefu za masika ambazo zinaanza katikati ya mwezi wa Machi mpaka Mei
kwa kiasi cha milimita 1000 mpaka 1,400
 Mvua nyepesi za mchoo ambazo zinanyesha kati ya mwezi wa julai mpaka
augosti kwa kiasi cha milimita 100
 Mvua fupi za vuli zinazonyesha kati ya mwezi oktoba na Desemba kwa kiwango
cha milimita 500 mpaka 800
Uoto wa Asili
Uoto wa asili wa halmashauri ni vichaka na misitu ya asili. Misitu ya mikoko katika ukanda wa
pwani yenye ukubwa wa hekta 1,200 mpaka 3,000. Misitu ya asili ni hekta 1,500 na sehemu
iliyobaki ni mimea iliyopandwa na watu.
MUUNDO WA UTAWALA
Halmashauri ya jiji la Tanga ina Tarafa 4, kata 24 na vijiji 23, mitaa 146 na vitongoji 129. Jiji la
Tanga limegawanyika katika maeneo ya mjini na vijijini ambapo Jumla ya kata 14 zipo mjini,
kata 8 vijijini na kata 2 ni mchanganyiko wa mjini na vijijini. Jiji lina jimbo moja la uchaguzi
ambalo ni jimbo la Tanga.
Halmashauri ya jiji laTanga inaundwa na baraza la madiwani lenye wajumbe 33 kati ya hao 24 ni
wa kuchaguliwa na tisa ni wa viti maalum wanawake. Pia kuna jimbo moja la uchaguzi (jimbo la
Tanga) lenye mbunge mmoja wa kuchaguliwa (mh. Omar Rashid Nundu) na wabunge wawili
viti maalum wanawake mmoja toka chama cha mapinduzi CCM na mwingine toka chama cha
wananchi CUF.
Orodha ya tarafa na kata za jiji la Tanga

1 NGAMIANI KASKAZINI
1. Usagara,
2. Mzingani
3. makorora,
4. central
5. ngamiani
kaskazini

2 NGAMIANI KATI
1. Msambweni
2. Mwanzange
3. Majengo
4. ngamiani kati
5. ngamiani kusini
6. mabawa

3 CHUMBAGENI
1. Nguvumali
2. Chumbagen
3. kiomoni,
4. Mzizima
5. Mabokweni
6. chongoleani

4 PONGWE
1. Maweni
2. Pongwe
3. Marungu
4. Tongoni
5. Tangasisi
6. Duga
7. kirare

JUMLA 4 24

Aidha Mtendaji Mkuu wa Halmashauri ni Mkurugenzi Mtendaji akisaidiana na Wakuu
wa Idara na Wakuu wa Vitengo.

Muundo wa Idara za Halmashauri ya Jiji unajumuisha Idara zifuatazo:
1. Utumishi na Utawala
2. Fedha
3. Uchumi na Biashara
4. Elimu ya Msingi
5. Elimu ya Sekondari
6. Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
7. Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
8. Kilimo,Mifugo na Ushirika
9. Afya na Usafishaji
10. Ujenzi na Zimamoto

Aidha, Muundo huo pia umejumuisha vitengo vifuatavyo:
1. Sheria na Usalama
2. Ukaguzi wa Ndani
3. Ugavi
4. Uchaguzi

 DIRA YA JIJI
Maisha ya wakazi wa Jiji la Tanga yameboreka kwa kuzingatia matumizi endelevu ya
rasilimali zote zilizopo na miundombinu muhimu imeimarika chini ya misingi ya utawala
bora.

DHAMIRA YA JIJI
Halmashauri ya Jiji la Tanga kupitia misingi ya utawala bora imedhamiria kutoa huduma
bora kwa kuzingatia uchumi na ustawi endelevu wa wananchi wake na kushirikisha
wadau katika kupanga na kutumia rasilimali zilizopo kupitia uongozi uliochaguliwa
kidemokrasia.



No comments:

Post a Comment