Alisema:
Jumatatu wakati akitangaza kujiuzulu, baadhi ya makardinali waliokuwapo walibubujikwa machozi.
Kumekuwa na mawazo tofauti kuwa huenda uamuzi huo haukutokana na afya yake kuyumba wala umri wake mkubwa, bali huenda kuna shinikizo linalotokana na masuala mengine ama ya kihistoria au kisiasa.
Wachukunguzi wa masuala ya Kanisa Katoliki
wanasema hata umri wa miaka 78 aliokuwa nao alipochaguliwa kuwa Papa
mwaka 2005 tayari ulikuwa mkubwa na wakati huo hakikuonekana kikwazo.
Pia wanasema mbali na kuwa wapo mapapa wengine
waliowahi kujiuzulu kabla, lakini suala hilo si la kawaida ndani ya
kanisa, na halikuwahi kutokea kwa miaka 600 iliyopita, tangu
alipojiuzulu Papa Gregory XII mwaka 1415.
Hata hivyo, Vatican imeendelea kushikilia kuwa
sababu ya kujiuzulu kwa kiongozi huyo ni kulegalega kwa afya yake na
umri mkubwa, huku ikithibitisha kuwa Benedict (Joseph Rutzinger)
amefanyiwa upasuaji wa moyo miezi mitatu iliyopita.
Msemaji wa Vatican pia alikiri jana kuwa moyo wa Papa unasaidiwa na kifaa maalumu kinatumia betri inayochajiwa mara kwa mara.
-Ni uamuzi wa kustukiza sana ila kuna maana kubwa na tungependa pia kuifahamu.