Monday, October 8, 2012

mabadiliko ya Tabia nchi

 http://www.mwananchi.co.tz/images/stories/00000000000000000000pangani.jpg
 ATHARI za mabadiliko ya Tabia nchi zinaendelea kujidhihirisha katika maeneo mbalimbali hapa nchini ukiwemo mji wa Pangani. Mji wa Pangani upo katika mwinuko wa mita 0 hadi  100 kutoka usawa wa bahari. Ni moja kati ya miji inayoathirika  na mabadiliko ya Tabia nchi ambapo mbali na kuongezeka kwa joto, ongezeko la kina cha maji limekuwa ni tishio kubwa kwa wakazi wa mji wa Pangani na mali zao.