Kihistoria
Mkoa wa Tanga ulitumiwa sana na wakoloni wa Kireno, Kiarabu, Kijerumani
na Kiingereza ikiwa lango la biashara na uchumi kwa kuunganisha sehemu
za ndani za Afrika Mashariki na Kati na sehemu mbalimbali za Dunia
hii ni ofisi ya mkuu wa mkoa wa tanga maeneo ya masiwani
kupitia
bahari ya Hindi. Mwaka 1840 eneo la Manga lilikuwa njia waliopitia
wafanyabiashara kutoka Bara Arabu waliokuja kutafuta meno ya tembo
na watumwa. Waarabu walikuwa wakiacha vyombo vya usafiri (majahazi)
eneo la Sadani (Bagamoyo) na kuanza safari kupitia Manga, Kimbe hadi
Kondoa Irangi. Misafara mingine ya wafanyabiashara ilianzia Unguja
kupitia Pangani, Kiwanda (Sindeni), Ngugwini, Mbego, Kwediboma, Mgera
hadi Kondoa Irangi ambapo walileta nguo, shanga na vitu ili
kubadilishana na pembe za ndovu, watumwa, chakula na mifungo.
Kutokana na mwingiliano wa tamaduni mbalimbali, wenyeji wa Tanga
wamerithi tamaduni, lugha na ustaarabu wa mataifa mbalimbali ya
Washirazi, Waarabu, Wachina, Wahindi, Wareno, Wajerumani, Waingereza na
Waswahili.
Mkoa
wa Tanga ni mzizi na chimbuko la Tanganyika kabla ya kuungana na visiwa
vya Unguja na Pemba mwaka 1964 na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania. Tanganyika ilipata Uhuru mwaka 1961 huku Mkoa wa Tanga ukiwa
ni msafirishaji mkubwa wa zao la Mkonge duniani na mhimili wa kukua
kwa uchumi wa nchi. Jina Tanga lilitolewa na wafanyabiashara wa
Kishirazi likiwa na maana nne ambazo ni Tambarare, Mabonde ya
Kijani, Barabara za Milimani na Kilimo cha Milimani. Neno nyika ni la
kibantu ambalo lilikuwa likitumiwa sana na wenyeji wakimaanisha mbuga au
pori zaidi ya jina Tanga.
Harakati
za kudai Uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza zilifanikiwa na
Tanganyika kupata Uhuru tarehe 9 Disemba, 1961 chini ya uongozi wa
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya chama cha TANU. Wakati
huo (1961) Mkoa wa Tanga ulikuwa ni Jimbo lenye Wilaya tano (5) ambazo
ni Wilaya ya Tanga, Handeni, Pangani, Usambara na Same.