Friday, December 21, 2012

mfumo mpya wa ORM uliotumika mwaka huu kusahihisha mtihani darasa la saba 2012 na kuokoa fedha nyingi na muda wa usahihishaji kutokana na mitihani yote ya mwaka huu kusahihishwa kwa kutumia kompyuta badala ya kusahihishwa kwa mikono na walimu kama ilivyokua kwa miaka iliyopita.



.
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dr Shukuru Kawambwa amesema kiwango cha kufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba 2012 kujiunga na kidato cha kwanza  kimeongezeka kwa asilimia 8.8 ikilinganishwa na mwaka 2011.
Hiyo sentensi ameitoa wakati akitangaza matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2012 ambapo amesema pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha kufaulu, vitendo vya wanafunzi kugushi mitihani vimepungua kutoka wanafunzi 9,736 mwaka 2011 mpaka wanafunzi 293 ambao tayari wamefutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu kwenye mitihani.
Amesema alama za juu ya ufaulu kwa wanafunzi wote ni 234 kati ya 250, wasichana wamefaulu kwa wingi zaidi kuliko wavulana ambapo namkariri akisema “jumla ya wanafunzi laki tano na elfu sitini mia saba na sita kati ya wanafunzi laki nane na elfu sitini na tano mia tano thelathini na nne waliofanya mtihani, wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari za serikali”
“Idadi hiyo ni sawa na asilimia 64.78 ya wanafunzi waliofanya mtihani, kati ya wanafunzi hao waliochaguliwa wasichana ni laki mbili na 81 elfu 460 sawa na asilimia 50.2 na wavulana ni laki mbili elfu 79, 24e sawa na asilimia 49.8″ – Kawambwa
Kuhusu mfumo mpya wa ORM uliotumika mwaka huu na kufanya maswali yote kwenye mtihani kuwa na majibu ya kuchagua, waziri Kawambwa amesema mfumo huo umesaidia kuokoa fedha nyingi na muda wa usahihishaji kutokana na mitihani yote ya mwaka huu kusahihishwa kwa kutumia kompyuta badala ya kusahihishwa kwa mikono na walimu kama ilivyokua kwa miaka iliyopita.
Kuhusu ishu ya usahihishaji namkariri akisema “safari hii ni mara ya kwanza kusahihisha kwa kutumia kompyuta, sio binadamu anaeshika kalamu na kuweka tiki…. hapana, karatasi ndio inatumbukizwa kwenye mashine na usahihi ni mkubwa zaidi kwenye kusahihisha yani haitegemei mwalimu huyu ameamka vipi labda A akadhani ni B”