A
1. Adui lakini po pote uendako yuko nawe.
2. Afahamu kuchora lakini hajui achoracho.
3. Afuma hana mshale.
4. Ajenga ingawa hana mikono.
5. Ajifungua na kujifunika.
6. Akitokea watu wote humwona.
7. Akitokea watu wote hunungunika na kuwa na huzuni.
8. Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi apendeza.
9. Alipita mtu ana bunda la mshale.
10. Alipita mtu mwenye kibandiko cha nguo.
11. Aliwa, yuala; ala, aliwa.
12. Amchukuapo hamrudishi.
13. Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi.
14. Amefunua jicho jekundu.
15. Ameingia shimoni akiwa uchi, akatoka amevaa nguo nzuri.
16. Amejitwika mzigo mkubwa kuliko yeye mwenyewe.
17. Amekaa kimya na watoto wamemzunguka pande zote.
18. Amekula ncha mbili.
19. Amevaa joho kubwa kuliko yeye mwenyewe.
20. Anakuangalia tu wala halali au kutembea.
21. Anakula kila siku lakini hashibi na hatashiba.
22. Anakula lakini hajashiba na hatashiba milele.
23. Anakula lakini hashibi.
24. Anapendwa sana ingawaje ni mkali sana.
25. Anatoka kutembea, anakuja nyumbani anamwambia mama, ‘Nieleke’.
26. Ashona mikeka wala hailali.
27. Askari wangu wote wamevaa kofia upande.
28. Askari wangu wote wamevaa mavazi meusi.
29. Asubuhi atembea kwa miguu mine, adhuhuri kwa miwili.
30. Atapanya mbegu nyingi sana lakini hazioti.
31. Atolewapo nje hufa.
B
32. Baba alinipa mfupa, nikautunza ukawa fahali.
33. Baba ameweka mkuki nje nikashindwa kuukwea, mdogo wangu akaukwea.
34. Babako akojoapo hunung’unika.
35. Babu amefunga ushanga shingoni.
36. Babu anakula ng’ombe, analea fupa linakuwa ng’ombe.
37. Babu hupiga kelele akojoapo.
38. Babu mkubwa ameangushwa na babu mdogo.
39. Babu, nyanya, mjomba, mama, baba na watoto, mna safari ya wapi?
40. Bak bandika, bak bandua.
41. Bawabu mmoja tu asiyeogopa chochote duniani.
42. Bibi kikongwe apepesa ufuta.
43. Bibi yake hutandikwa kila siku, lakini hatoroki.
C
44. Chakula kikuu cha mtoto.
45. Cha ndani hakitoki nje, cha nje hakiingii ndani.
46. Chang’aa chapendeza, lakini hakifikiwi.
47. Chatembea na hakijapata kupumzika hata nukta moja.
48. Cheupe chavunjika manjano yatokea.
49. Chumba change kina ukuta niondoa na kuusimika nitakapo.
50. Chungu change cha udongo hakipasuki kikianguka.
D
52. Dada yangu akitoka kwao harudi kamwe.
53. Dada yangu kaoga nusu.
54. Drrrrrh1 Ng’ambo.
55. Dume wangu amelilia machungani.
F
56. Fahali wa ng’ombe na mbuzi wadogo machungani.
57. Fika umwone umpendaye.
58. Fuko kajifukia, mkia kaacha nje.
59. Funga mizigo twende Kongo.
H
60. Hachelewi wala hakosei safari zake.
61. Haina miguu wala mikono, lakini, yabeba magogo.
62. Hakihitaji maji, wala udongo, wala chakula; lakini chamea.
63. Hakionekani wala hakishikiki.
64. Hakisimami, na kikisimama msiba.
65. Hakuchi wala hakuchwi.
66. Halemewi wala hachoki kubeba.
67. Hamwogopi mtu yeyote.
68. Hana mizizi, nimemkata mara nyingi lakini haachi kukua.
69. Haoni kinyaa.
70. Hapo nje panapita mtu mwenye miguu mirefu.
71. Hasemi, na akisema hatasahaulika.
72. Hasimamishwi akiwa na ghadhabu.
73. Hata inyeshe namna gani haifiki humu.
74. Hata jua likiwaka namna gani hakauki wala kupata joto.
75. Hata Mzungu ameshindwa.
76. Hauchagui chifu wala jumbe.
77. Hausimiki hausimami.
78. Hawa wanaingia hawa wanatoka.
79. Hesabu haihesabiki.
80. Huitumia kila siku lakini haiishi.
81. Huku kutamu, huku kutamu, katikati uchungu.
82. Huku unasikia ‘pa’ Huku unasikia ‘pa!
83. Hula lakini hashibi.
84. Hulala tulalapo, huamka tuamkapo.
85. Humu mwetu tuko wanne tu, ukimwona wa tano mwue.
86. Huna macho lakini wakamata wanyama.
87. Hupanda mtini na mwenye kichaa wake.
88. Hutembea watatu.
89. Hutoka upesi sana lakini hasalimu.
90. Huwafanya watu wote walie.
91. Huwezi kukalia alipokalia msichana wangu mweusi.
92. Huzikwa mmoja, hufufuka mmoja, huzeeka wengi.
I
93. Inaonekana mara mbili katika dakika moja na mara moja tu katika mwaka.
94. Ini la ng’ombe huliwa hata na walioko mbali.
J
95. Jembe la Wangoni haliishi.
96. Je, unaweza, kukua ukampita mzee wako?
97. Jiwe litoalo maji.
K
98. Kaburi la mfalme lina milango miwili.
99. Kaka yangu anapanda darini na fimbo nyuma.
100. Kama kingekuwa mkuki, ungekuta kimekwisha kuua wote.
101. Kama unapenda, mbona usile?
102. Kanipa ngozi nikapikia, kanipa nyama nikala, kanipa mchuzi nikanywa, kanipa mfupa nikautumia.
103. Kapanda mti pamoja na uchawi wake.
104. Kidimbwi kimezungukwa na majani.
105. Kikioza hutumiwa, kikiwa kichungu hakitumiwa.
106. Kila linapofika kwetu hutanguliza makelele.
107. Kila mtu atapitia malango huo.
108. Kila mtu hata mfalme huheshimu akipita.
109. Kila siku hupita njia hiyo hiyo bali arudipo hatumwoni.
110. Kileee! Hiki hapa.
111. Kilimsimamisha chifu njiani.
112. Kina mikono na uso lakini hakina uhai.
113. Kinaniita lakini sikioni.
114. Kisima cha Bimpai kina nyoka muwai, ndiye fisadi wa maji.
115. Kisima kidogo kimejaa changarawe.
116. Kitendawili change ukikitambua nitakupa hirizi.
117. Kiti cha dhahabu hakikaliwi na watu.
118. Kiti cha Sulatni hukaliwa na mwenyewe.
119. Kiti nyikani.
120. Kitu change asubuhi chatembea kwa miguu mine, saa sita kwa miguu miwili, jioni kwa miguu
mitatu.
121. Kiwanja kizuri lakini hakifai kuweka mguu.
122. Kombe ya Sultani I wazi.
123. Kondoo wangu amezaa kwa paja.
124. Kondoo wangu mnene kachafua njia nzima.
125. Kondoo za mtoto zamaliza mavuno.
126. Kufanya kwa ridhaa mojamoja.
127. Kuku wangu aliangua mayai jana, lakini si kuku wala ndege.
128. Kuku wangu amezalia miibani.
129. Kuku wetu hutagia mayai mikiani.
130. Kuna mlima mmoja usio pandika
131. Kuna mtu mwenye tumbo kubwa aliyesimama nje.
132. Kuna ziwa kubwa ambalo limekauka na limebakiza mizizi.
133. Kunguru akilia hulilia mirambo.
134. Kwenye msitu mkubwa Napata mti mmoja tu, lakini kwenye msitu mdogo naweza kupata miwili.
135. Kwetu mishale na kwenu mishale.
136. Kwetu twalala tumesimama.
L
137. La mgambo limelia wakatoka weusi tu.
138. Likienda hulia, likirudi halilii.
139. Likitoka halirudi.
140. Liwali amekonda lakini hana mgaga.
M
141. Mama ametengeneza chakula lakini hakula.
142. Mbona kinakumeza lakini hakikuli?
143. Mbona mwakunjiana ngumi bila kupigana?
144. Mbona mwasimama na mikuki, mwapigana na nani?
145. Mchana ‘ti’ usiku ‘ti’.
146. Mdogo lakini humaliza gogo.
147. Mfalme amesimika mkuki wake hapa name nikausimika wangu kando yake, baadaye
hatukuitambulisha tena.
148. Mfalme hushuka kwa kelele.
149. Mfalme katikati lakini watumishi pembeni.
150. Mfalme wetu hupendwa sana, lakini wakati wa kumwona lazima umtoe nguo zote kwanza.
151. Mhuni wa ulimwengu.
152. Mkanda mrefu wafka mpaka pwani.
153. Mke wangu mfupi, lakini huvaa nguo nyingi.
154. Mlango wa nyumba yangu uko juu.
155. Mlima mkubwa wapandwa kuanzia juu.
156. Mlimani sipandi.
157. Mlima umezuia kutazama kwa mjomba.
158. Mlima wa kupanda kwa mikono.
159. Mlima wa kwetu hupandwa na mfalme.
160. Mlima wa mwenyewe hupandwa na mwenyewe.
161. Mpini mmoja tu lakini majembe hayahesabiki.
162. Msitu ambao haulii hondohondo.
163. Mti mkubwa, lakini una matawi mawili tu.
164. Mti mnyanya mti kerekeche mti ah mti ah!.
165. Mti wangu una matawi kumi na mawili na kila tawi lina majani kadiri ya thelathini.
166. Mtoto asemea pangoni.
167. Mtu mdogo mwenye miguu mirefu ambaye aweza kutembea dunia nzima kwa dakika tano.
168. Mvua hema na jua hema.
169. Mvua kidogo ng’ombe kaoga kichwa.
170. Mwadhani naenda lakini siendi.
171. Mwalimu analala na mwanafunzi wanamsomea.
172. Mwanamke mfupi hupiga kelele njiani.
173. Mwanamke mfupi hutengeneza pombe nzuri.
174. Mwanang’ang’a hulia mwituni.
175. Mwepesi, lakini aweza kuvunja nyumba za mji wote.
176. Mwezi wangu umepasuka.
177. Mzee Kombe akitoa machozi wote hufurahi.
178. Mzee Kombe akilia watu hufurahi.
179. Mzizi wa miti hutokea mbali.
180. Mzungu yuko ndani na ndevu ziko nje.
N
181. Naitumia ngazi hiyo kwa kupandia na kushukia.
182. Nakikimbilia lakini sikikuti.
183. Nakupa lakini mbona huachi kudai.
184. Nakwenda msituni na mdogo wangu, lakini yeye namwacha huko.
185. Nameza lakini sishibi.
186. Namkimbiza lakini simkuti.
187. Namlalia lakini halii.
188. Namwomba atangulie lakini hukataa kabisa.
189. Nanywa supu na nyama naitupa.
190. Napigwa na mvua na nyumba ipo.
191. Natembea juu ya miiba lakini hainichomi.
192. Natembea juu ya miiba lakini sichomwi.
193. Natembea na wenzangu lakini tukifika kwenye nyumba mimi hukaa mlangoni.
194. Natengeneza mafuta lakini nimepauka sana.
195. Natengeneza mbono lakini alama hazionekani.
196. Ndege wengi baharini.
197. Ndugu wawili wafanana sana, lakini hawatembeleani.
198. Ngoja nikumbuke.
199. Ng’ombe wa baba watelemka mtoni.
200. Ng’ombe wa babu huchezea miambani.
201. Ng’ombe za babu zikienda machungani hulia, zikirudi hazilii.
202. Ng’ombe za babu zinalala na mkia nje.
203. Ng’ombe wamechanganyika nikakosa wa kwangu.
204. Ng’ombe wangu ni weupe kwatoni.
205. Ng’ombe wangu wote hunywa maji isipokuwa mmoja.
206. Ngozi ndani nyama juu.
207. Nguo ivaliwayo kila siku isiyoingiwa na chawa.
208. Nikicheka kinacheka, nikinuna kinanuna.
209. Nikienda arudi, nikirudi aenda.
210. Niiita ‘baba’ huitika ‘baba’.
211. Nikija kwenye ndege wananifukuza, na nikienda kwenye wanyama hawanitaki.
212. Nikimpiga huyu huyu alia.
213. Nikimpiga mambusu.
214. Nikimwita hunijibu nani.
215. Nikipewa chakula nala bali natema.
216. Nikitembea walio wafu huniamkia na walio hai hukaa kimya.
217. Nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayupo.
218. Ni kitu gani ambacho kutoa ni kuongeza?
219. Nikitupa mshale wangu mchana huenda mbali sana, lakini niutupapo usiku hauendi mbali.
220. Nikiwaambia ondokeni hukataa, lakini mjomba akitokea wote hukimbia.
221. Nilijenga nyumba yangu nikaiacha bila kuiezeka majani; lakini niliporudi nilikuta imekwisha
ezekwa majani.
222. Nilijenga nyumba yangu yenye mlango mmoja.
223. Nilimkata alafu nikamridhia.
224. Nilimtuma askari vitani akaniletea kondoo mweusi.
225. Nilipandia majanini nikashukia majanini.
226. Nilipigwa na tonge la ugali la moto nilipopita msituni.
227. Nilipitisha mkono wangu chini la ardhi, nikamshika beberu mkubwa sana.
228. Nilipoangalia kwenye magereza ya Wazungu, nikaona wameketi juu ya mabati.
229. Nilipofika msituni nilikuta chungu cha pure kinachemka.
230. Nilipoingia Rumi, alitoka mtu na wake kumi; kila mke na tundu kumi, kila tundu na kuku
kumi; kila kuku na mayai kumi. Mayai, kuku, tundu, wake, kumi kumi kumi. Wangapi
walikwenda Rumi?
231. Nilipo, juu kuna miiba na chini vivyo hivyo; lakini sichomwi.
232. Nilipokuwa mchanga nilikuwa na kijikia lakini sasa sinacho.
233. Nilitembea na mwezangu naye hupita vichakani.
234. Nimechoma fimbo yangu pakabaki pa kushikia tu.
235. Nimefyeka mitende yote kiungani isipokuwa minazi miwili tu.
236. Nimejenga nyumba babu akaihamia kabla mimi sijahamia.
237. Nimekata mti, akaja samba mwekundu akaukalia.
238. Nimekata mti bara ukaangusha matawi pwani.
239. Nimekwenda na rafiki yangu kwa jirani, yeye akafika kabla yangu.
240. Nimemtahiri binti wangu akatoa damu mchana kutwa.
241. Nimempeleka kondoo wangu akatoa damu mchana kutwa.
242. Nimemtuma mtu kumwamkua mtu, yeye amekuja, Yule aliyetumwa hajaja.
243. Nimemwacha mzee kikongwe mtoni anangojea mgeni kulaki.
244. Nimempandikiza mti wangu ukapeleka matawi ng’ambo ya mto.
245. Nimesimama mbali nyikani lakini naonekani.
246. Nimetembea kitambo, kukumbuka sikufunga nyumba.
247. Nimetoka kutembea kutembea, nikashika ng’ombe mkia.
248. Nimetupa mshale angani wala sitambui utateremsha ndege wa namna gani.
249. Nimeweka ndizi yangu, asubuhi siioni.
250. Nimezaliwa na mguu mmoja.
251. Nimezungukwa na adui wengi, lakini siumizwi.
252. Nina kijiti change, nizidivyo kukikata ndivyo kizidivyo kuwa kirefu.
253. Nina kitu change kitumiwacho na wengine kuliko mimi.
254. Nina kitu kizuri sana nyumbani, lakini siwezi kukichukua.
255. Nina kitu nipendacho ambacho hata baba, mama, dada, kaka hata na mgeni nimpendaye sana
siwezi kumwazima.
256. Nina mwezi ndani ya bakuli.
257. Nina ng’ombe wangu nisipomshika mkia hali majani.
258. Nina nyumba yangu imezungukwa na mifupa.
259. Nina pango langu lilojaa mawe.
260. Nina watoto wangu hamsini na wote nimewavisha visibau vyeupe.
261. Nina watoto watatu, mmoja akitoka kazi haifanyiki.
262. Nina badilika umbo langu baada ya kila muda mfupi.
263. Ninachimba mizizi ya mti usio na mizizi.
264. Ninacho, nakitumia, lakini kila nikitumiapo, sikiharibu ila nakipa rangi.
265. Ninakula vitu vyote vinono lakini sikui wala sinenepi.
266. Ninakwenda naye na kurudi naye.
267. Ninao mlima ambao una msitu kileleleni tu.
268. Nitokeapo kila mmoja asema namtazama yeye tu.
269. Njia yapitwa siku zote lakini haina alama.
270. Njoo hapa nije hapo.
271. Nne nne mapaka pwani.
272. Nusu mfu nusu hai.
273. Nyama ndogo imewashibisha wengi wala isiishe.
274. Nyama ya Reale haijai kikombe.
275. Nyanya yako ana huruma kukubeba ulalapo.
276. Nyumba yangu ina makuti tele, lakini mvua ikinyesha huvuja.
277. Nyumba yangu ina milango mimgi.
278. Nyumba yangu ina nguzo moja.
279. Nyumba yangu kubwa, haina mlango.
280. Nyumba yangu kubwa, haina taa.
281. Nyumba yangu kubwa hutembelewa mgongoni.
O
282. Oh!
283. Ondoka nikae.
P
284. Paa alipenga hata pua ikapasuka.
285. Palikuwepo watu watatu wakivuka mto. Mmoja alivuka pasipo kukanyaga maji wala kuyaona;
wa pili aliyaona maji lakini alivuka bila kuyakanyaga; wa tatu aliyaona na kuyakanyaga alipovuka.
Ni nani hawa?
286. Panda ngazi polepole.
287. Para hata Maka.
288. Pete ya mfalme ina tundu katikati.
289. Poopoo mbili zavuka mto.
290. Po pote niendako anifuata.
R
291. Rafiki yangu ana mguu mmoja.
292. Reli yangu hutandika ardhini.
293. Ruka Riba.
S
294. Shamba langu kubwa lakini mavuno hayajazi kiganja.
295. Shamba langu miti mitano tu.
296. Shangazi yangu ni mrefu sana lakini hafikii tumbo la kondoo.
297. Sijui aendako wala atokako.
298. Sijui afanyavyo.
299. Sina dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa babangu. Ni nani huyo?
300. Subiri kidogo!
301. Sultani alipiga mbiu watu waje kufanya kazi yake lakini wakashindwa.
T
302. Taa ya bure.
303. Taa ya Mwarabu inapepea.
304. Tajiri aniweka mfukoni na maskini anitupa.
305. Tandika kitanga tule kunazi.
306. Tangu kuzaliwa kwake sijamwona asimame wala kukimbia.
307. Tatarata mpaka ng’ambo yam to.
308. Tatu tatu mpaka pwani.
309. Tega nikutegue.
310. Teke teke huzaa gumugumu, na gumugumu huzaa teke teke.
311. Tengeneza kiwanja kikubwa kabila Fulani lije kupigania.
312. Tonge la ugali lanifikisha pwani.
313. Tukate kwa visu ambacho hakitakatika.
314. Tulikaribishwa mahali na mdogo wangu, yeye akaanza kushiba kabla yangu.
315. Tuliua ng’ombe na babu, kila ajaye hukata.
316. Tuliua ng’ombe wawili ngozi ni sawasawa.
317. Tumvike mwanamke huyu nguo.
318. Tunajengajenga matiti juu.
319. Twamsikia lakini hatumwoni.
U
320. Ukimcheka atakucheka, ukimwomba atakuomba.
321. Ukimwita kwa nguvu hasikii, lakini ukimwita polepole husikia.
322. Ukimwona anakuona.
323. Ukitaka kufahamu ana mbio, mwonyeshe moto.
324. Ukitembea ulimwengu wote utakosa nyayo.
325. Ukiukata haukatiki, ukiushika haushikiki.
326. Ukiwa mbali waweza kumwona Fulani umatini.
327. Ukoo wa liwali hauna haya.
328. Ule usile mamoja.
329. Umempiga sungurra akatoa unga.
330. Unatembea naye wote umjiao atakuona.
331. Upande wote umjiao atakuona.
332. Ushuru wa njia wa asili.
333. Utahesabu mchana na usiku na hutamaliza kuhesabu.
V
334. Viti kumi nyumbani, tisa vyakalika lakini kimoja hakikaliki.
W
335. Wake wa mjomba kimo kimoja.
336. Wako karibu lakini hawasalimiani.
337. Wanakuja mmoja mmoja na kujiunga kuwa kitu kimoja.
338. Wanameza watu jua linapokuchwa.
339. Wanamwua nyoka.
340. Wanangu wawili hugombana mchana, usiku hupatana.
341. Wanao wakati wao wa kuringa, nao ni weupe kama barafu.
342. Wanapanda mlima kwa makoti mazuri meusi na meupe.
343. Wanastarehe darini.
344. Wanatembea lakini hawatembelewi.
345. Watoto wa mtu mmoja hulala chini kila mwaka.
346. Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu.
347. Watoto wangu wote nimewavika kofia nyekundu.
348. Watoto wangu wote wamebeba vifurushi.
349. Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi
wakalimenya, wote wakaridhirika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao?
350. Watu waliokaa na kuvaa kofia nyekundu.
351. Watu wamehama askari wekundu wakazidi nyikani.
352. Watu wawili hupendana sana; kati ya mchana hufuatana ingawa mmoja ni dhaifu. Usiku mdhaifu
haonekani tena.
353. Watu wote ketini tumfinye mchawi.
354. Wewe kipofu unaenda wapi huko juu?
Y
355. Yaenda mbali lakini haiondoki ilipo.
Z
356. Zilitazamana na mpaka sasa hazijakutana.
357. Ziwa dogo linarusha mchanga.
358. Ziwa kubwa, lakini naogelea ukingoni tu.
MAJIBU
A
1. Inzi
2. Konokono
3. Nungunungu (Kufuma ni kuchoma. Nungunungu huchoma kwa miiba yake ingawa si sawa na mishalw ya mwindaji)
4. Ndege
5. Mwavuli
6. Jua
7. Ugonjwa
8. Mgomba (Migomba katika kiunga hupendeza baada ya kukwanyua majani makavu)
9. Mkindu
10. Inzi
11. Papa
12. Kaburi
13. Giza
14. Jua
15. Mbegu
16. Konokono au Koa
17. Mgomba (Shina la mgomba huzungukwa na machipukizi)
18. Wali
19. Kaburi ( KAburi ni kama joho la mauti)
20. Picha
21. Mchanga
22. Ardhi
23. Mauti
24. Moto
25. Kitanda (Kueleka ni kuchukua mgomgoni)
26. Maboga (Tunda la mboga hukaa chini ya majani yake)
27. Mahindi
28. Chunguchungu
29. Fedha
30. Mvua (Matone yake ni kama mbegu azitapanyazo mkulima)
31. Samaki
B
32. Muwa (Kipande cha muwa kikipandwa hutokea muwa mkubwa)
33. Sisimizi
34. Mawingu (Baba mawingu huleta mvua na ngurumo)
35. Mtama au Nazi
36. Muwa (Taz. 32 juu)
37. Mvua (Taz 34 juu)
38. Mti na Shoka
39. Siafu
40. Nyayo
41. Mlango (BAwabu ni mngoja mlango)
42. Kope za macho
43. Kinu cha kutwangia
C
44. Usingizi
45. Nyama na mfupa
46. Jua
47. Mwezi au Jua
48. Yai
49. Pazia
50. Mjusi au panya
51. Dunia na mbingu
D
52. Jani likwanyukapo
53. Jiwe mtoni
54. Daraja la buibui
55. Radi
F
56. Mwezi na nyota angani
57. Kioo
58. Kata mtungini
59. Mikia ya mbwa
H
60. Jua
61. Maji
62. Nywele
63. Hewa
64. Moyo
65. Kula
66. Ardhi
67. Njaa
68. Ukucha
69. Mvua
70. Mvua
71. Kalamu
72. Upepo au Mvua
73. Kwapani
74. Pua ya Mbwa
75. Mauti
76. Utelezi
77. Mkufu
78. Nyuki mzingani
79. Nyota
80. Miguu
81. Jua (Jua ni kali zaidi wakati wa mchana kuliko asubuhi au jioni)
82. Mkia wa kondoo
83. Sindano
84. Jua
85. Matendegu ya Kitanda
86. Ndoana
87. Kivuli
88. Mafiga
89. Kuku (Kuku akifunguliwa asubuhi hukimbia nje upesi bila kusalimu)
90. Moshi
91. Chungu jikoni
92. Mbegu na matunda
I
93. Herufi ‘K’;
94. Kifo
J
95. Miguu (yaani Nyayo)
96. Nywele kichwani
97. Macho
K
98. Kata ya kuchukulia mizigo kichwani
99. Paka na mkia wake
100. Kizingiti cha mlango
101. Ulimi
102. Nazi
103. Tumbako inaponuswa puani
104. Macho
105. Maziwa
106. Mvua (Taz. 34 juu)
107. Kifo
108. Mlango
109. Jua
110. Kivuli
111. Chawa
112. Saa
113. Mwangwi
114. Taa ya Utambi (Utambi ndio nyoka mkali anayemaliza mafuta ya taa ambayo ni maji ya
kisima Bimpai)
115. Kinywa na meno
116. Mimba
117. Moto
118. Kuku aatamiapo mayai
119. Uyoga
120. Maisha ya binadamu (Mtoto mchanga hutambaa na halafu hutembea na mzee kutumia
mkongojo)
121. Kipara
122. Kisima
123. Mhindi
124. Konokono
125. Jiwe la kusagia
126. Kuska mkeka
127. Nyoka au samaki
128. Nanasi au chungwa
129. Matunda
130. Nafasi kati mdomo na pua (Ulimi hauwezi kugusa pua)
131. Ghala
132. Chongo
133. Mtoto akililia maziwa
134. Watoto wa ng’ombe na muzi
135. Mikia ya panya
136. Nguzo za nyumba
L
137. Chunguchungu
138. Debe ama buyu
139. Neno
140. Sindano
M
141. Chungu cha kupikia
142. Nyumba
143. Mafiga
144. Katani
145. Mlango
146. Mchwa
147. Kohozi
148. Mvua (Taz. 34 juu)
149. Moto na mafiga
150. Hindi
151. Inzi
152. Njia
153. Hindi
154. Shimo la mchwa
155. Sima (ugali)
156. MAji
157. Kisogo
158. Sima
159. Nafasi kati yam domo na pua ya ng’ombe
160. Buibui na utando wake
161. Mkungu wa ndizi
162. Mimba
163. Kichwa na masikio
164. Ngoma na upatu
165. Mwaka
166. Ulimi mdomoni
167. Mawazo
168. Kobe
169. Jiwe
170. Jua
171. Kinyesi na inzi
172. Kunguru
173. Nyuki
174. Shoka (Mwanang’anga ni ndege aliaye mwituni kama shoka.)
175. Tufani
176. Kweme (Tunda la mkweme)
177. Mvua
178. Mvua
179. Siafu
180. Hindi
N
181. Mwiba
182. Njia
183. Tumbo
184. Kinyesi
185. Mate
186. Kivuli
187. Kitanda
188. Kisigino
189. Muwa
190. Matunda ya pua au kwapa
191. Miiba
192. Ulimi (Miiba hapa ni meno)
193. Mbwa
194. Mzinga wa nyuki kwa nje
195. Mzinga wa nyuki
196. Nyota
197. Macho
198. Boga change
199. Mawe mtoni
200. Mijusi
201. Vibuyu
202. Viazi vitamu udongoni
203. Pesa au nyayo
204. Katani
205. Fimbo ya kuchunga
206. Firigisi (tumbo la kuku au ndege)
207. Nyusi (Nywele zinazoota penye sehemu ya uso inayotokeza kwa juu ya macho)
208. Kioo
209. Kivuli majini
210. Mwangwi
211. Popo
212. Utomvu wa papai
213. Puliza kidole wakati unapojikwaa
214. Mwangwi
215. Shoka
216. Majani makavu na mabichi
217. Kivuli
218. Shimo
219. Jicho
220. Umande na jua
221. Mahindi machanga
222. Jani la mgomba la nchani
223. Kupanda mbegu
224. Fuko
225. Mwiba
226. Manyingu
227. Kiazi kikuu
228. Pelele
229. Mzinga wa nyuki
230. Hakuna
231. Ulimi kinywani
232. Chura
233. KIvuli
234. Njia
235. Masikio
236. Mjusi
237. Utomvu
238. Nzige
239. Sauti ya njuga
240. Kivuli
241. Mgomba
242. Kuangua tunda ama nazi
243. Mtego
244. Kivuli
245. Moto
246. Dirisha ama ufa
247. Kata
248. Mimba
249. Nyota
250. Uyoga
251. Ulimi na meno
252. Maisha (Kadiri siku zinavyopita, yaani kukatwa, ndivyo umri unavyoongezeka)
253. Jina
254. Dada (Si kawaida mtu kuoa dada yake)
255. Mke
256. Maziwa
257. Jembe
258. Mdomo
259. Kinywa
260. Kunguru
261. Mafiga
262. Kivuli
263. Jiwe
264. Maji na mkojo (Mkojo unadhaniwa kuwa maji yaliyobadilika rangi baada ya kupita mwilini)
265. Chungu cha kupikia
266. Kivuli
267. Kichwa
268. Jua ama mwezi
269. Njia ya jua au mwezi angani
270. Kiraka
271. Matendegu
272. Sungura alalapo
273. Kinoo
274. Mkufu
275. Kitanda
276. Mwembe
277. Kichunguu
278. Uyoga
279. Yai
280. Kaburi
281. Konokono (Nyumba yake iko mgongoni wakati wote)
O
282. Mwanamke aliyevunja chungu, mshangao wake
283. Maji ya mfereji
P
284. Mbarika
285. Wa kwanza ni mtoto tumboni mwa mamake, wa pili ni mtoto aliyebebwa mgongoni, wa tatu
ni mama mwenyewe
286. Sima ya ugali
287. Utelezi
288. Kata ya kuchukulia mizigo
289. Macho (Popoo ni tunda la mti uitwao mpopoo)
290. Kivuli
R
291. Uyoga
292. Siafu
293. Maiti
S
294. Nywele kichwani (Nywele zikikatwa, hata kichwa kikubwa namna gani, zafumbatika kwa
kiganja cha mkono.
295. Mkono wa vidole
296. Njia
297. Upepo
298. Nyoka apandavyo mtini
299. Mtoto wangu
300. Miiba (Mtu akichomwa na mwiba husubiri)
301. Maji
T
302. Jua au mwezi
303. Kilemba
304. Makamasi (Tajiri hutumia kitambaa cha mfukoni kupenga makamasi, lakini maskini
hupenga kwa mkono na kutupa)
305. Nyota
306. Mkufu
307. Utando wa buibui
308. Mafiga
309. Mwiba
310. Mhindi ama yai
311. Mbono
312. Jicho
313. Maji
314. Kucha
315. Kinoo
316. Mbingu nan chi
317. Kuezeka nyumba
318. Mpapai
319. Sauti
U
320. Mwangwi
321. Fisi
322. Jua
323. Kinyonga
324. Mwamba
325. Moshi
326. Tundu la sindano
327. Wanyama
328. Kifo
329. Tunda la mbuyu
330. Fimbo ama bakora
331. Kinyonga
332. Kujikwaa
333. Nywele
V
334. Moto
W
335. Vipande vya kweme
336. Nyumba ama kuta zinazoelekeana
337. MAtone ya mvua
338. Nyumba
339. Watu wanaotwanga
340. Mlango
341. Nyota
342. Vipepeo
343. Panya
344. Macho
345. Maboga
346. Fuu
347. Jogoo
348. Vitovu
349. Waliopanda ni vidole vya miguu na mikono, walioona ni macho wawili, waliochuma ni
vidole vitano vya mkono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na aliyelila ni
mdomo.
350. Kuku, katani au mahindi
351. Viroboto
352. Kivuli
353. Kula ugali
354. Mkweme
Y
355. Njia
Z
356. Kingo za mto
357. Chungu jikoni
358. Moto