Wednesday, February 27, 2013

SHULE TOFAUTI ZA SEKONDARI NA MAZINGIRA YAKE

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfjQpM09Na70fzoUWHeslwmP5WTgujkgGaogY7-GyphHtucDAJXR7_bfzV7NjF7JWav5yXDFikF4jfxbC105bD4SENC5raRFqw6nP_Geb5ukLEYGR5uj86F019lgWVA1SanQpY_6vveG4/s1600/r2.png
MTWARA:MASASI SEC

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjilULZGgCgcrh1AoUfSGi6vO9o1xN_h7SgRTGe4UMpajQbd5ozVo8ZUhFDcKlupiDBgkDjkXJQKL6TtnjnV_gR29URTZeykUqo5Kq1CJLeKNMVDzxvPLqb1EzJZOK0SSn7vPCIYrAcXak/s1600/r5.pngLINDI:NGONGO SEC

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi474uKMA56V0_sDTFbqCnl25Jy57jTq_ukmizQfBfunmAaSwxGyJgEZ4gAjecKXPJdh_VfthpHoGAT-re8tMvMIYRXQ408N3vvvWAisPRjXF76Dm-D3FsT9WBvtoN-M4P3OcKUOgUaJKU/s1600/r4.png
MOROGORO:MANDELA SEC


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRHs4nerjKiNpme8-IryhLhioFKG7tMVtThdWt6T3hhua6csStr9erWUDKfoBw8FaxdWo5mbfAzBVoRc4wBI1pVODLNyog9r0Ss5eZagxY4s3ftDG7LnjSBEpK2AWrhLRniuklZfUO6wY/s1600/r6.pngDAR ES SALAAM:TWIGA SEC

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiB4_nE9rW2huuIjuwn8bqvameeJ88Vvosw3Cyw6KoQw8g9tr-5SRbhccPxz-FiFiEssq_rc4yhgEK06Qtv2_ZY7yUj7q8fc2_rqpWiRC4SARzcRxmPeFqHKesART9iJl2licB9_cic9vU/s1600/r3.png
PWANI:KISARAWE LUTHERAN SEMINARY

Urais 2015: Utafiti wa Synovate wapondwa,wadau wadai una ajenda ya siri

 
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye amesema haziamini tafiti zinazotolewa na Syonovate akidai hazina ukweli wowote.


Katika maoni yao, baadhi ya wasomi kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini walieleza wasiwasi wao kuhusu usahihi wa matokeo hayo na kuhoji mbinu zilizotumika wakisema inawezekana hazikuwa sahihi.
Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo ameuponda akisema haukufuata misingi ya sayansi ya siasa.
Dk Makulilo alisema alifanya utafiti kwa kampuni zinazofanya tafiti kama hizo kati ya mwaka 2010 hadi 2011 na kugundua udhaifu mkubwa katika kampuni hizo.
“Kwanza wanakosea, kwa mfano wanaposema kuwa utafiti huu ni mwendelezo wa ule uliofanyika Desemba 5 hadi 18, 2011. Ukichunguza utakuta data hizo hazipo. Zilizopo ni za Mei 2 hadi 19, 2011.”
“Kwa kawaida uelewa wa wananchi wa vijijini ni mdogo ukilinganisha na mijini kwa sababu mijini kuna vyombo vya habari. Kwa mfano, ukiangalia swali la nani anafaa kuwa Rais, mwaka 2011 walisema Dk Wilbrod Slaa alikuwa na asilimia 42, lakini sasa ana asilimia 17.
Vijijini wengi bado wanaikubali CCM kutokana na uelewa mdogo, iweje Dk Slaa ambaye chama chake hakina wafuasi wengi vijijini ashinde?” alihoji.
“Utafiti wa Synovate una dosari kubwa kisayansi, hauonyeshi tarehe wala wapi umefanyika. Waliohojiwa wameonyeshwa umri wao, lakini hawaelezwi maoni yao kulingana na umri, jinsia, wanatoka vijijini na mijini. Nilipofanya utafiti wangu niliwafuata wakakimbia…” alisema Dk Makulilo.
Mhadhiri mwingine wa UDSM, Profesa Gaudence Mpangala alisema nyakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu, tafiti nyingi hufanyika zikiwa na malengo ya kubeba watu au chama fulani.
Hata hivyo, alisema kilichofanywa na Synovate ni utafiti hivyo kwa kuwa yeye hajafanya utafiti ni vigumu kuupinga moja kwa moja... “Ila kwa mtizamo wa kawaida unatia shaka.”

Thursday, February 14, 2013

Papa: Nimejiuzulu kwa hiyari

“Kama mnavyofahamu, nimeamua kuachia madaraka niliyopewa na Mungu Aprili 19, 2005,” alisema na kushangiliwa. Aliongeza: “Nimefanya hivi kwa uhuru kamili kwa manufaa ya kanisa.”
Alisema:

 Jumatatu wakati akitangaza kujiuzulu, baadhi ya makardinali waliokuwapo walibubujikwa machozi.
Kumekuwa na mawazo tofauti kuwa huenda uamuzi huo haukutokana na afya yake kuyumba wala umri wake mkubwa, bali huenda kuna shinikizo linalotokana na masuala mengine ama ya kihistoria au kisiasa.
Wachukunguzi wa masuala ya Kanisa Katoliki wanasema hata umri wa miaka 78 aliokuwa nao alipochaguliwa kuwa Papa mwaka 2005 tayari ulikuwa mkubwa na wakati huo hakikuonekana kikwazo.
Pia wanasema mbali na kuwa wapo mapapa wengine waliowahi kujiuzulu kabla, lakini suala hilo si la kawaida ndani ya kanisa, na halikuwahi kutokea kwa miaka 600 iliyopita, tangu alipojiuzulu Papa Gregory XII mwaka 1415.
Hata hivyo, Vatican imeendelea kushikilia kuwa sababu ya kujiuzulu kwa kiongozi huyo ni kulegalega kwa afya yake na umri mkubwa, huku ikithibitisha kuwa Benedict (Joseph Rutzinger) amefanyiwa upasuaji wa moyo miezi mitatu iliyopita.
Msemaji wa Vatican pia alikiri jana kuwa moyo wa Papa unasaidiwa na kifaa maalumu kinatumia betri inayochajiwa mara kwa mara.
-Ni uamuzi wa kustukiza sana ila kuna maana kubwa na tungependa pia kuifahamu.

JK awapa polisi ‘meno’ kudhibiti maandamano

“Wajibu wenu umetajwa kisheria, mamlaka yenu mlikabidhiwa na Bunge na wanapopiga kelele kuwa mmetumia nguvu kubwa, waambie sheria mmezitunga ninyi kwa hiyo nendeni mkazibadilishe,”

Aliwaagiza polisi kutimiza wajibu wao kuhakikisha wanadhibiti vurugu zote bila ya kusikiliza maneno ya wanasiasa na watu wengine, ambao wanalaumu bila  kujua kazi nzuri inayofanywa na askari.
“Wajibu wenu umetajwa kisheria, mamlaka yenu mlikabidhiwa na Bunge na wanapopiga kelele kuwa mmetumia nguvu kubwa, waambie sheria mmezitunga ninyi kwa hiyo nendeni mkazibadilishe,” alisema Rais Kikwete.
Pia, Rais Kikwete alishangazwa na  kauli za watu kuwa, polisi wanatumia nguvu kubwa kupita kiasi, lakini hajajua tafsiri hiyo inacholenga.
Aliwaagiza polisi kufanya kazi kwa uweledi na kujituma zaidi kulingana na mafunzo waliyoyapata kutoka vyuoni, ikiwamo  kutafuta jinsi bora ya kuzuia machafuko hata kabla ya kutokea.
Akitaja baadhi ya vyanzo vya vurugu hizo, alisema ni kutokana na baadhi ya wanasiasa kushindwa kutii maagizo ya polisi hata pale wanapozuiwa kufanya mikutano.
Awali, Mkuu wa Polisi nchini, Said Mwema alisema wanaendelea  kuratibu na kusimamia mikakati  kuhakikisha wanakuwa wa kisasa zaidi.

Tuesday, February 5, 2013

elimu yetu inavyojenga matabaka katika jamii.


 wanafunzi wa shule ya msingi wakiwa darasani,hii ndio tofauti kubwa kati ya shule yenye kutoa maarifa na ujuzi na shule yenye kutoa vyeti na sifa za kumuwezesha mtu kupata kazi.


MATOKEO mazuri au mabaya  ya elimu kwa mtu,  huonekana katika namna anavyotenda mambo na dhamira yake ya kutenda,  na wala hayatokani na alichojifunza, namna alivojifunza na sababu ya kujifunza.
Hiyo ndio tofauti kubwa kati ya shule yenye kutoa maarifa na ujuzi na shule yenye kutoa vyeti na sifa za kumuwezesha mtu kupata kazi.
Watu wengine wanapozungumzia elimu wanafikiri kuhusu utaratibu mzima wa kujifunza wenye lengo la kumpatia mtu ujuzi na maarifa na kumudu vyema kile alichojifunza.
Ujuzi na maaarifa ndio hasa lengo na upatikanaji wake  unaotarajiwa utumike katika kupambana na changamoto na hata kuibua na kuleta maarifa mengine zaidi.
Kuna watu wengine wanapozungumzia elimu,  wanafikiria umiliki wa cheti kinachoonyesha una ujuzi fulani.
Elimu ya aina hii sio kwa ajili ya kutumika katika maisha wala kutafuta maarifa mengine,  bali ni kwa ajili ya mtu kukariri anachojifunza na  kuyatoa yale maarifa yaliyokaririwa katika mitihani ili apate cheti kizuri kitakachowezesha kupata kazi yenye kipato kizuri.
Kimsingi,  cheti kazi yake ni kumpatia mtu kazi. Cheti ndio ‘pasipoti’ ya kwenda katika nchi ya kipato.
Watanzania wengi kama sio wote,  tumeangukia katika kundi hili. Wengi wetu tunataka pasipoti ya kwenda katika ‘nchi’ ya kipato cha kuajiriwa, tunataka vyeti!
Katika mfumo wetu wa elimu mpaka sasa ufaulu wa mtihani ndio unaosema fulani apangiwe shule gani, apangiwe kozi gani  chuoni, apate kiasi gani kwenye mikopo ya elimu ya juu na apangiwe kazi gani na alipwe kiasi gani.
Sasa kuna vita kati yetu, kila mmoja anataka mwanawe, yeye mwenyewe au ndugu yake  afaulu ili afike katika nchi ya ahadi.
Mbinu mbalimbali zinatumika  kufanikisha lengo hili, vita haina macho! Mbinu kuu ikiwa matumizi ya pesa. Kusoma shule nzuri na ghali, kulipia twisheni, walimu bora, kununua vitabu na mwishowe hata kununua mitihani.
Mchakamchaka  huu wa kutaka kufaulu kisha kupata vyeti,  unawaacha nyuma watu wa kipato cha chini kwani hawawezi kumudu kununua mitihani, au kusoma twisheni  za gharama.
Wenye nacho wananeemeka na mtindo huu. Mwelekeo unaonyesha masikini  wataachwa kwa kiasi kikubwa na wenye uwezo.
Mwanzo wa kujenga matabaka mawili kupitia elimu bila kificho  unaonekana.

Alhamisi hii feb 7,2013 kwenye AMPLIFAYA Clouds Fm.

Alhamisi hii feb7 2013 kuanzia saa moja usiku kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM dakika 120 zitatumika kuirusha Exclusive interview ya BABU WA LOLIONDO, ni safari iliyochukua dakika 570 kutoka Arusha mjini, ni zaidi ya saa masaa tisa(9).
Safari ya kwenda kwa Babu wa Loliondo Samunge ilianza kwenye defender ya polisi kwa sababu magari ya watu binafsi yalikua yanagoma kwenda kutokana na vita kali ya Wasonjo na Wamasai, hivyo njia pekee ya kufika kwa Babu ni kusindikizwa na Polisi, stori kamili ni Alhamisi hii feb 7 2013 kwenye AMPLIFAYA Clouds Fm.
Kwenye interview ya zaidi ya dakika 60 na Babu wa Loliondo Ambilikile, picha na stori nyingine zitapatikana kwenye millardayo.com kuanzia jumatano usiku na alhamisi.

kikao kazi cha maafisa habari wa serikali Dodoma

Picha na 1 f90c5Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifungua mkutano wa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine amewataka kufanya kazi  kwa kuzingatia weledi na kutoa taarifa sahihi kwa umma mara kwa mara kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali.


Picha no 8 03ec7
 Mmiliki na muendeshaji wa mtandao wahabari na matukio wa Mjengwa Blog kutoka Iringa Bw. Maggid Mjengwa akitoa mada kwa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali kuhusu Faida na Changamoto za matumizi ya mitandao ya kijamii kwa Mawasiliano Serikalini mjini Dodoma.


Picha na 7 f660a
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi chao kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma.


Picha na 2 5c000
Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi hicho  mjini Dodoma.


Picha na 3 958db
Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabuza Serikali  Sarah Reuben akichangia moja ya mada katika kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma.


hab1 55f16
Baadhi ya maafisa habari wa serikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiAwasilishwa katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Bw. Peter Millanzi mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw. Midradji Maez, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Bw. Abel Ngapemba, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Shiririka la Maendeleo la Taifa NDC


hab2 6bb7f
. Maafisa Habari kutoka wilaya na Mikoa mbalimbali waliohudhuria kikao kazi cha maafisa habari mjini Dodoma wakiwa katika majadiliano ya pamoja kuhusu mafanikio na changamoto zinzoyakabili maeneo yao ya kazi.


hab3 bf999
Maafisa Habari kutoka wizara mbalimbali waliohudhuria kikao kazi cha maafisa habari mjini Dodoma wakiwa katika majadiliano ya vikundi kuhusu mafanikio na changamoto zinazoyakabili maeneo yao ya kazi wakiongozwa na mwenyekiti wa kikundi hicho Luteni Kanali Juma Sipe, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano.


hab 50c83
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akiwasilisha mada kuhusu mkakati wa Mawasiliano wakati wa Kikao kazi cha maafisa habari wa serikali kinachoendelea mjini Dodoma.

5/2/2013, Dodoma
Kikao kazi cha Maafisa habari wa Serikali kutoka Wizara, taasisi, wakala wa serikali, mashirika ya umma, mikoa na wilaya mbalimbali nchini leo kimeingia siku ya pili mjini Dodoma kwa  maafisa hao kupata fursa ya kujadili changamoto zinazokabili vitengo vya  habari na mawasiliano serikalini na namna ya kuzitatua.
Katika kikao hicho mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo ile ya Mwongozo wa Ofisi za Mawasiliano serikalini iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Msaidizi kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) anayeshughulikia uratibu wa vitengo vya mawasiliano serikalini akitoa msisitizo mkubwa  kwa maafisa habari kuyafahamu vizuri majukumu yao ya kazi kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma ili kuboresha utendaji wa kazi.
 Pia maafisa hao wamepata fursa ya kujifunza namna ya kuboresha  mawasiliano serikalini kupitia mada ya mkakati wa mawasiliano (Communication Strategy) wa kuiwezesha jamii kupata taarifa sahihi kwa muda muafaka ,mada iliyowasilishwa na Meneja mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy.
Katika mada hiyo Bw. Mungy ametoa wito kwa maafisa hao kuzitumia nafasi zao kutoa taarifa kwa umma mara kwa mara ili kuwapa fursa wananchi kufahamu yale yanayofanywa na serikali.
Ametoa wito maafisa hao kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari katika kutekeleza mkakati huo kwa kuhakikisha kuwa wanatoa habari kwa umma kupitia radio, magazeti, televisheni na mitandao ya kijamii ili kuepusha madhara yanayoweza ku.sababishwa na jamii kukosa taarifa sahihi za serikali za utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo

Friday, February 1, 2013

polisi Mtwara wakimbia makazi

Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)  katika ubishi Mtwara hivi karibuni

SHINIKIZO la wananchi mkoani Mtwara kutaka gesi isitoke mkoani humo, limesababisha polisi takriban 50 kuzikimbia familia zao baada ya kutishiwa maisha na wananchi.

Habari za kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maria Nzuki zimeeleza kuwa polisi hao ambao wengi wao ni wale wanaoishi mitaa mbalimbali mjini humo, wamehamia kambini kutokana na kutishiwa maisha na wananchi kwamba watawadhuru wao na familia zao.

Habari hizo zilieleza kuwa, vurugu zilizotokea Januari 25 na 26, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu wanne huku jengo la Mahakama ya Mwanzo na nyumba zikiwamo za wabunge kuchomwa moto na nyingine kuharibiwa vibaya, ni moja ya sababu zilizowatisha polisi hao.
“Wamerudi kambini kwa sababu ya kutishiwa ila ni baadhi ya askari, siyo wote,” alisema kamanda huyo.

Juzi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema hasira za wananchi hao ni kudhani kuwa gesi hiyo itapelekwa wilayani Bagamoyo nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete.
Alisema pia mpasuko ndani ya CCM mkoani humo na harakati za kisiasa ni sababu nyingine zilizochochea mgogoro huo.

Hata hivyo, Kamanda Njuki alisema hana idadi kamili ya askari waliokimbia makazi yao huku akifafanua kuwa mambo yatatulia mkoani humo ikiwa Serikali itatekeleza ahadi zake.
“Serikali inatakiwa kutekeleza ahadi zake ilizozitoa kwa wananchi ili kuweka hali shwari, lakini pamoja na hayo sisi tutaendelea na ulinzi kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda sawa na hali inakuwa shwari,” alisema Njuki.

Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakiwatisha polisi hao na kutokana na hali hiyo imeonekana ni vyema waende kambini.

Askari wengi waliokimbia nyumba zao ni wale ambao makazi yao yanafahamika na wananchi ambao wakati wa vurugu hizo, walikuwa miongoni mwa askari waliokuwa waki zituliza. Inaelezwa kwamba wapo polisi zaidi ya 40 ambao hawaonekani mtaani na hata katika nyumba wanazoishi.

“Hivi sasa hawapo, si unaona mji ulivyokuwa mweupe, watu wana hasira na wanataka gesi isitoke, kwa hiyo hata wakimwona polisi wanaweza kumfanya lolote,” alisema mtoa habari ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini na kuongeza:

“Wananchi sasa wamekuwa kitu kimoja, wameweka siasa na tofauti zao nyingine kando kutaka gesi iwanufaishe, ila binafsi naomba jambo hili limalizike kwa amani.”

SIRI YA MGOGORO WA GESI MTWARA YAFICHUKA

MTWARA KUMEKUCHA: SIRI YA MGOGORO WA GESI MTWARA YAFICHUKA: MOJA ya mambo yaliyoamsha hisia za wakazi wa Mkoa wa Mtwara hadi kushinikiza kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani humo, ni taarifa kuwa...

TASWIRA YA MTWARA
 uwanja wa ndege


 mtwara posta


hekaheka za kushinikiza kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani humo


fanya fujo uone



kumekucha
 

 juhudi
 


ruaha national park

ruaha umefika?

TASWIRA YA USAFIRI WA GARIMOSHI RELI YA KATI


hekaheka
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgu_OsSQH60IMQQNubkSvirps2i3DShxoVnDi8D6WqhqyKSub-ZN5AObw65wji5-I3yS_rcQH2QVrfcK2KF-kwGOjs4oB6OR2eajOA-azKvRwiboQ-7UqScAMRGDl2zjje7Q00TeEABdPA/s1600/IMG_9422.jpg
mishemishe
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgElkUelk7e-3ar-FpnKsZ_w6D4JSRsUYpZza34bbIvcKYJ_b2K3jqVCe1TyHh0A32qI_SB4Er1zGmXkl9_Yqwmo_3eFNjTh7vA5FNFiXnGKRFB84WlT6rE8ZQuHnTd0iRz2nDQO72M5QE/s1600/IMG_8970.jpg

harakati
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhx7x-x4hjTF2ZY2qMN1skCjrUj4i_VSWcY05a3neiyGlENWsFG7Lmajn5InKkxPXNQPOxNJc1WksLP84GSJzXGYEiWJua7hsf4JLoX-xU4sGB3M92DvLQLi7X3foSJx7KKmKAfkGH9Zrs/s1600/IMG_8850.jpg


mchango wako bado unahitajika kwa ajili ya kunusuru maisha ya mtoto Zawadi

Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima: MBUNGE LUKUVI AANZA KUMCHANGIA MTOTO WA AJABU IR...: Mbunge  wa jimbo la Ismani Wiliam Lukuvi ameanza kumchangia mtoto  aliyezaliwa akiwa na macho matatu ,uvimbe usoni na kichwa mfano  wa uy...