Friday, March 8, 2013

SAI BABA,basi linalofanya safari zake kutoka Ruvuma(kwa wakunyumba) kwenda Dar es salaam,limemgonga mwendesha pikipiki na kusababisha mauti yake



Hili ndilo basi lililomgonga  mwendesha pikipiki,lenye namba za usajili T 690 BUW.


Upande wa mbele wa basi lilipogongana


Abiria wakieleza ajali ilivyotokea eneo la Mburushi


 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusdedit Nsimeki alie vua kofia akiwa katika eneo la tukio maeneo ya kwa Mburushi


 
Pikipiki ya marehemu  Steven Adam (62) yenye namba za usajili  T 618 ATX

 

  Umati wa wasafiri wakiwemo wapita njia wakiangalia ajali hiyo mbaya iliyotokea leo majira ya saa moja asubuhi.

 Marehem Steven alikuwa ni mfanyabiashara,mkazi wa Liumbu Mletele akielekea mjini kupeleka maziwa yake kwa wateja ndipo alipopatwa na mauti hayo.Kwa maelezo ya wasafiri wamesema mwenye makosa ni dereva wa pikipiki ambaye hakuwa makini barabari kwa kuendesha vibaya na kwa mwendo kasi pasipo kuzingatia sheria za barabarani.