Sunday, March 31, 2013

mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam

jengo lililoporomoka na shughuli za uokozi mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam Machi 29, 2013

PICHA TOFAUTITOFAUTI ZIKIONESHA SHUGHULI ZA UOKOZI ZINAVYOENDELEA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjih22Xpq4njTzY8r3PphRh1uZLSdgFIef-WoxGAMpYdIWWVJpPAkIqdPOMIE6Iosu6bIhMmr6VTHXaFxU0YS2bs3BNF9NLYmkkGWpTsKzdx95fxVx4NGxofEamb9i8G8suruGPCMa5UT4/s1600/Untitled.png



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDNt_J7aN8oKOA8LqIXNxm_JK54Hpek10yREe0fWr8B3znTOKOn3js8zr0yU1FT-a0u3D5ZCRABZtgcKMM3bmTf2NzPXSGerNYjqv_Py4k8nR5uXs6VCy6gBEWiQuSR9_MhC0FNJaLLZw/s1600/GOPR5667.jpg

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjV3mdlwf41pkcC97srIC_03kq8upqudKc5mZD29C2V5F1XaKhK1KeLZYYTOYX6Eus92mYrgpy5chiFcayDibPgwZoj9qcXEl7X13f975a2qo46qVRuJ4wwh-JFaT-cilhmqZPNSnVLvdg/s1600/GOPR2834.jpg

 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiEVkc1EdrBnnEqFbPH3MUbkUtPEs-9ijULF3EwYVrQvf28oY8a1pocmmmj3VL-bosbM4jEy0M2C9unnh535L2diJakEJ3MwqJXyRmGJJ09Df5kN7hiCBHSOSg3mPN28jnP77iir_W3EOQ/s1600/C27B5717.jpg

Wednesday, March 27, 2013

ibada takatifu ya kubariki mafuta ya Krisma na kurudiwa kwa kiapo cha mapadri, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, jana.

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1731754/highRes/482598/-/maxw/600/-/dhe7iaz/-/pengo.jpg
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, akiendesha ibada takatifu ya kubariki mafuta ya Krisma na kurudiwa kwa kiapo cha mapadri, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, jana. Picha na Emmanuel Herman.


Kiongozi wa Kanisa  Katoliki nchini, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, amewataka mapadri wa Kanisa hilo kuwa kioo kwa matendo mema kwa kila wanachokifanya kwa wengine.
Kardinali Pengo aliyasema hayo jana wakati wa misa ya sherehe ya Sakramenti ya Upadri na kubariki mafuta ya Pasaka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini humo.
Alisema ni lazima kuwa watimilifu wa kibinadamu kwa kupitia njia ya sadaka, mateso na kifo hivyo kuwataka kuwafundisha yaliyo mema na yenye kumpendeza Yesu Kristu.
“Ili kufikia ukamilifu hatuwezi kukwepa misalaba, waumini mnatakiwa kutuombea ili kuweza kumwakilisha Yesu Kristu kwa matendo yaliyo mema na ya kumpendeza,” alisema Kardinali Pengo. “Hivi sasa  shida na mahangaiko ya dunia ni mengi  lazima  kumwonyesha Yesu ili aweze kutusadia na kushinda.
“Tukianza kuangalia chanzo cha matatizo na mahangaiko yalivyo hivi sasa hatuwezi kufika na tutaangamia,” alisema Kardinali Pengo.
Alisema njia nyingine zozote ambazo zinashabikia kama anasa na ukatili haziwezi kufanikiwa, hivyo aliwataka Mapadri hao kuwahubiria amani waumini.

Tuesday, March 26, 2013

MAFUNZO YA MGAMBO JKT YAMEFUNGWA RASMI LEO

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRngLz7DOBnW22i2cxjGzU3nqIck3t1bYybkRgD55xIXTRMQKp35LXrLLkl4asSJJIhgepUFLGgCExABtjia3OshhMEW3A7qPWhQtI8wUG2Eqa1r4bBsFcclCWyuHfxZjk6xAxAehm21g/s1600/8E9U3088.JPG
Mheshimiwa Esther Bulaya akikabidhiwa cheti cha kuhitimu mafunzo ya mgambo RUVU JKT na Amiri jeshi mkuu wa Tanzania,Raisi wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Mrisho Kikwete

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgdt0nvR_tBWIXPePxX5qfj1-l6ABcDVNgYPd0L8qvTxxJQN1LtOONhJu-qi94zKesrM-b2lRezcFbDK1IfjjQaYaIh9rc1lVqlDhjQ9fq4TGIfsAmqu4bDiCjAhwQ5eaJioDH8k5xZn-k/s1600/9.JPG
Mheshimiwa Zitto Kabwe akikabidhiwa cheti cha kuhitimu mafunzo ya mgambo MGAMBO JKT Wilaya ya Handeni na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEha0ZSoXAUq10TBbx-rMFAE1JdhvB3uIjHv7EDcv0nJTSSfzvylBFih9kvD9nsSGAlDzPxRd7bq19Ru8O2SiyWq0YP_9csqOIBlwweXJcHPkWN0YU8LZRWMCWKFjeXmNA6CXm7OOlL4Q80/s1600/8E9U3018.JPG
Baadhi ya Waheshimiwa wakila kiapo,kushooto ni Halima Mdee


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiu9us9yJS57IAlllZNSKWZnzJgd3G1GJPEgLvl1Fv2qdKabnRnyQh-Mvc-FBgDgYZXcL4zqQUoDlA0uDpUmw8lDajB-JwwgvqyJff6SPfz_TMqJ9IW4sNCkr8N20HPKThhOmqXkGp85xE/s1600/1+(2).JPG
Upande wa mbele kushoto katikati ni Iddi Azani akihitimu mafunzo ya mgambo na wenzake kwa kutembea kwa ukakamavu


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiF4cZ6TxpgJC4BNaBwaTUfvi_oGoH3L3Ek_ML735mBrFyzlQXzjMtWURXq6IXAMRLiS8A_TrB4SagEmLu6F2WKanfbfCHnaE1PbQA-lnDQ2KXmknrGTJ8qh77jzbo-QWzHh4E4-Gh5b5I/s1600/5.JPG
Mbunge Athanas Mbassa wa Biharamulo akila kiapo Kambi ya Mgambo JKT Tanga


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjxmRjQeCKnETW0w-XkIuW46C4v7RaPT9PnH4_achfRrj6GP1fTvJwqydCdZwY7KCrhm42FqIj2t7QnE_0JgGEQFkthZI6ThhoB-GD_gD8nTfWLfiiA7FWIektcrU9zqBq1wKe7oe0gDxI/s1600/6.JPG
Mheshimiwa Abdallah Hjji Alli,Mbunge wa Kiwani Pemba akihitimu mafunzo ya Mgambo JKT Tanga

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh-wTNwREgx-fHGjKgLMNRC3BgY5KcohGedz7-k45s6hk0z4UN0SlLCShPUDQF8iGaO90QBtK2XiIqCmT_nIuO3xGI_J3MHA9LUMAs804dR3suJ7VSh-XcyRRRsXIwHihOurwbqUpIWufA/s1600/7.JPG
Mbunge Raya Khamisi wa Viti Maalumu naye alihitimu mafunzo ya Mgambo JKT Tanga

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1DqPzMobpATbfQFBdxJ4cxSKCS8r4ec6v2JuXvxuMFXka2aPppnFqnamtQW3iyxeQzQj8WciC-crNDsFeq7ECpaSx08ryYm5TN3Zn3nzBsy28X4XTQNKhqyiZ4QnzibY_9mCHbnLlQVI/s1600/8E9U3151.JPG
 Mbunge wa Mtera Mheshimiwa Livingstone Lusinde *kibajaji* alihitimu mafunzo(watatu kutoka kulia)

Monday, March 11, 2013

tanzania hatarini kufungiwa fifa


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiB8e3u-phmmb0iOw8ItXTaj-ZQeRQc-AEgxcMyp4R4JRqRZfjwIYXwdpXb1mWu_SyxHInz3y0cdmxyEqITamhnIwQUK7Qn8QxNfFFtSgWot4lP_aSizNpepOuKJsucWp5w8PPlWLWxJcM/s1600/1-fifa-logo.jpg
SHIRIKISHO LA SOKA

OFISA Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura 
--
Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) limesema litaifungia Tanzania iwapo itabainika kuwa Serikali imekuwa ikiingilia shughuli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

FIFA imesema kumekuwa na shutuma kupitia taarifa mbalimbali za vyombo vya habari nchini kuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeonesha nia ya kuingilia uendeshaji wa TFF.


Kwa mujibu wa barua ya jana (Machi 10 mwaka huu) ya FIFA kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, vyombo vya habari vimemkariri Waziri (Dk. Fenella Mukangara) kuwa Serikali imeiagiza TFF kutumia Katiba ya mwaka 2006 katika uchaguzi wakati tayari imeshafanyiwa marekebisho.

“Pia imeelezwa kuwa TFF imetakiwa kufanya Mkutano Mkuu pamoja na ule
wa uchaguzi kwa tarehe ambazo zimepangwa na Serikali. Vilevile imeelezwa kuwa Serikali inakusudia kuunda Kamati ya Muda iwapo TFF haitatekeleza maagizo yake,” imesema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valke.

FIFA imesema iwapo yaliyoripotiwa na vyombo vya habari yatathibitika kuwa kweli, maana yake huo ni uingiliaji wa wazi wa Serikali kwa shughuli za TFF.

“Tunapenda kuwakumbusha kuwa wanachama wote wa FIFA wanatakiwa kuendesha shughulizao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu mwingine kama ilivyoelezwa katika ibara za 13 na 17 za Katiba ya FIFA.

“Hivyo kama maagizo hayo yanayodaiwa kutolewa na Serikali yatatekelezwa, suala hili litapelekwa katika mamlaka za juu za FIFA kwa hatua zaidi ikiwemo  kuisimamisha Tanzania kama ambavyo inakuwapale panapokuwa na uingiliaji wa Serikali,” imesema barua hiyo.

Barua hiyo ambayo nakala yake pia imetumwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) imeelezea baadhi ya athari ambazo Tanzania itakumbana nazo endapo itasimamishwa ni timu za taifa pamoja na klabu kutoshiriki mechi za kimataifa kwa mujibu wa Ibara ya 14 ya Katiba ya FIFA.

Vilevile si TFF au wanachama wake na maofisa wengine watakaoweza kunufaika na programu za maendeleo, kozi au mafunzo yanayotolewa na FIFA na CAF.

“Madai ya uamuzi uliofanywa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni ya kusikitisha kutokana na ukweli kuwa FIFA ilishatangaza itatuma ujumbe wake kuchunguza jinsi hali ilivyo kwa sasa na kutoa mapendekezo yake. Kutokana na hali hii, ujumbe wa FIFA uliokuwa uje kuchunguza(suala la uchaguzi) itabidi usubiri kwa vile ni muhimu kushughulikia tatizo hili kwanza.

“Katika mazingira haya tunaomba ueleze msimamo huu wa FIFA kwa mamlaka zinazohusika (Serikali) na athari ambazo mpira wa miguu wa Tanzania utakumbana nazo. Tunakushuru na tunatarajia utatufahamisha kila hatua inayoendelea katika suala hili,” imesema barua hiyo.

OFISA Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Boniface Wambura

Saturday, March 9, 2013

vigogo wavuliwa madaraka TBS

Profesa Mhilu alisema hatua hiyo imekuja baada ya bodi hiyo kufanya usaili kwa vigogo mbalimbali wa shirika hilo
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1714304/highRes/473595/-/maxw/600/-/no9v67z/-/tbss.jpg'

 Profesa Mhilu alisema hatua hiyo imekuja baada ya bodi hiyo kufanya usaili kwa vigogo mbalimbali wa shirika hilo,Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Cuthbert Mhilu alisema jana kuwa waliovuliwa madaraka ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora, Dominic Mwakangale na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upimaji na Huduma za Vifungashio, Kezia Mbwambo.
 Baada ya hatua hiyo, bodi hiyo ilimteua Tumaini Mtitu kuwa Mkurugenzi mpya wa Udhibiti Ubora na Agnes Mneney kuwa Mkurugenzi wa Upimaji na Huduma za Vifungashio,Wengine walioteuliwa ni Emmanuel Ntelya atakayekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Shirika na Edna Ndumbaro kuwa Meneja Uandaaji Viwango vya Uhandisi.
Kadhalika, Matrida Kasanga ameteuliwa kuwa Meneja wa Hati na Tehama na Anitha Kaveva anakuwa Meneja Mipango na Utawala.
Alipoulizwa kama hatua hiyo inakwenda sanjari na sifa baada ya kufanyika kwa usaili Profesa Mhilu alisema: “Ninachowaambia ni hicho... hakuna tatizo tulilobaini kuhusu viongozi hawa, haya ni mabadiliko ya kawaida.”
Alipoulizwa kuhusu hatua hiyo, Mbwambo alijibu kwa kifupi: “Sifahamu, wasiliana na mwenyekiti wa bodi au  mkurugenzi mkuu ndiyo wenye nafasi ya kuzungumzia zaidi kuhusu hatua hiyo.”
Akizungumzia uteuzi huo, Profesa Mhilu alisema: “Hata hawa tuliowateua kushika nyadhifa hizo watambue kwamba tutawafuatilia kwa karibu tukiangalia utendaji wao, asiyefanya kazi kwa ufanisi atang’olewa.”
Alisema Bodi hiyo imetoa maagizo kwa Menejimenti ya TBS kuhakikisha kwamba inakomesha bidhaa feki, inafanya ukaguzi wa magari, pia kuhakikisha inaondoa urasimu wa upatikanaji wa leseni kwa wajasiriamali wadogo lakini kwa kuzingatia viwango vya bidhaa wanazotengeneza.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Joseph Masikitiko alisema kuwa amejipanga kushirikiana na menejimenti yake ikiwa ni pamoja na kukomesha makundi miongoni mwa wafanyakazi ili kuleta tija.
Tangu ilipozinduliwa, bodi hiyo imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kusafisha safu za utawala za shirika hilo baada ya kuanza kwa kumvua madaraka Kaimu Mkurugenzi Mkuu Leandiri Kinabo na kumteua Masikitiko kabla ya kuitisha usaili upya wa wakurugenzi.

Friday, March 8, 2013

SAI BABA,basi linalofanya safari zake kutoka Ruvuma(kwa wakunyumba) kwenda Dar es salaam,limemgonga mwendesha pikipiki na kusababisha mauti yake



Hili ndilo basi lililomgonga  mwendesha pikipiki,lenye namba za usajili T 690 BUW.


Upande wa mbele wa basi lilipogongana


Abiria wakieleza ajali ilivyotokea eneo la Mburushi


 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusdedit Nsimeki alie vua kofia akiwa katika eneo la tukio maeneo ya kwa Mburushi


 
Pikipiki ya marehemu  Steven Adam (62) yenye namba za usajili  T 618 ATX

 

  Umati wa wasafiri wakiwemo wapita njia wakiangalia ajali hiyo mbaya iliyotokea leo majira ya saa moja asubuhi.

 Marehem Steven alikuwa ni mfanyabiashara,mkazi wa Liumbu Mletele akielekea mjini kupeleka maziwa yake kwa wateja ndipo alipopatwa na mauti hayo.Kwa maelezo ya wasafiri wamesema mwenye makosa ni dereva wa pikipiki ambaye hakuwa makini barabari kwa kuendesha vibaya na kwa mwendo kasi pasipo kuzingatia sheria za barabarani.

Wednesday, March 6, 2013

Ofisa elimu awavua madaraka walimu 50


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjuCV9LyT-zhZFca_QDGQlRo9uMbdItAY9KdhW35_-VI-6yhGZ4njzDmAneWU72KyR_lzgFFEyWW3qZ8klrk9EzvZPLbdzqpmQZJzquBoB-526v3fi9lvIW4DNR3L5Rjq22qsvFmQy7AiU/s1600/HakiElimu2.JPG

Kilindi. Ofisa Elimu ya Msingi Wilaya ya Kilindi, Mkoa wa Tanga, Geofrey Abayo amewavua madaraka walimu wakuu 50 wa shule za msingi, lengo likiwa ni kusuka upya timu ya kuinua kiwango cha taaluma.
Abayo aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya matokeo ya darasa la saba mwaka jana wilayani hapa kuwa mabaya, baada ya asilimia 18 ya wanafunzi waliofanya mtihani ndiyo waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza.
Alitoa taarifa hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano na walimu wa shule za msingi na sekondari, uliofanyika katika kata tano za Kwediboma, Mabaranga, Negero, Kikunde na Songe.
Ofisa huyo akiwa ameambatana na Mkuu wa wilaya hiyo, Suleiman Liwowa  na Katibu Tawala Msaidizi Elimu Mkoa wa Tanga, Ramadhani Chomola walisema  walitarajia kupata matokeo hayo.
Alisema walitarajia watoto wengi kushindwa kutokana na kuongeza udhibiti katika usimamizi wa mitihani kitaifa kwa darasa la saba, kwa kuziba mianya inayotumiwa na baadhi ya walimu wasio waaminifu kuwapa majibu watahiniwa.
Abayo aliapa kuendelea kuwa mkali kwa walimu wanaowafanyia mitihani watoto ili wafaulu.
Mwalimu Ali Mganga wa Shule ya Msingi Kikunde, alipendekeza mitihani ya kitaifa ikishafanywa ipelekwe shuleni ili wanafunzi na walimu waweze kutambua walipojikwaa.
Hata hivyo, Mwalimu Mganga alitupia lawama kwa watungaji mitihani ya taifa  kwamba, haieleweki hivyo inachangia kwa kiwango kikubwa kufeli kwa watoto.
Naye Mwalimu Bakari Mwaliko wa Shule ya Msingi Mabaranga, Tarafa ya Mswaki, alishauri Serikali kuwachunguza watu waliosahihisha mitihani ya wanafunzi wa msingi na sekondari, akihisi huenda kuna hujuma za kisiasa.