Saturday, September 22, 2012

Parokia ya Kilole



Parokia hii ipo katika mji wa Korogwe. Ilianzishwa mnamo mwaka 1937 na Mapadre wa shirika la Roho Mtakatifu. Mwaka 1948 Padre Benedict Forsyth aliteuliwa kuwa paroko wa Kilole. Mwaka 1976 parokia ya Kilole ilikabidhiwa kwa Mapadre wazalendo wa Jimbo la Tanga. Na Padre Odillo Mtoi aliteuliwa kuwa paroko wa kwanza wa Kilole.
Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wakatoliki mjini Korogwe. Parokia ya Kilole ilimegwa na kuanzishwa kwa parokia nyingine mjini Korogwe. Parokia hii mpya inaitwa parokia ya Mt. Augustino Manundu. Mapadre walioishi parokiani Kilole waliendelea kotoa huduma katika parokia ya Manundu mpaka Manundu ilipopatiwa Paroko wake.
Masista wa mama yetu wa Usambara wanatoa huduma ya kufundisha katekesi katika shule za msingi zilizopo mjini Korogwe.
Parokia ya Kilole ni moja ya makanisa ya hija Jimboni Tanga. hii ni parokia pekee ambayo mapadre wazalendo wanazikwa katika parokia hii.
Parokia ya kilole imezalisha mapadre wafuatao: Severine Msemwa, Severine Yagaza, Nemes Kiama na Gerald Kabarega.
Kwa sasa Paroko wa parokia hii ya Kilole ni Pd. Josefu Sekija.
 Parokia inavigango vifuatavyo:

Ngombezi, Kwamsala, Mavuluni, Kwashemshi, Mahenje, Lwengera, Magunga Cheki, Mvuleni, Kwamdulu A, Kwamdulu B, Kwakombo, Lujela, Mandera, Maili Kumi, Kwamaligo, Mwananyamala na Old Korogwe

No comments:

Post a Comment