Saturday, September 22, 2012

Wagosi wa Kaya - Tanga kunani?

 Picture of Wagosi wa Kaya
(verse 1)
Tanga kwa kweli ni kijimji kidogo,
na pia kuna mambo ya uswahili si kidogo.
lakini habari zake kwa kweli ni kubwa,
na mji ule ukiuvamia kwa papara palee,
mengi yatakukumba!
Ukifika Tanga utatambuaje kama
kweli huu nd'o mkoa wa Tanga?
Utaona wanawake wengi pale
wamejifunika mabaibui na vijikanga.
Waume makanzu baraghashia, mkononi tasibihi
wanakuhesabia.

Baiskeli ndiyo teleeee, mpaka
zawakera wenye magari barabarani
Halafu hali ya sasa sii kama ile ya
zamani, ukaenda ovyo tu utauza
kila kitu chako cha thamani.
Matajiri wa enzi zile ukiwaona
leo hii tena hawana thamani
Enzi zile bwana mkoa wa Tanga kila
kitu mambo yalikuwa swafi.
Mijikazi ilikuwa tele, na
kulikuwa hakuna mambo ya
ukorofi, lakini sasa hivi thubutu,
twendelea kuchakaa mpaka tutoke
ukurutu, hakuna ndimaa, kilo mtu
ambiwa ajifanya mvuvi ati, na
ukamshauri mtu akushushia
varangati, astaghafirullai laadhim!
Watu waongea peke yao kama
vile wendawazimu, labda tutambike
mizimu huenda kidogo pale mambo
yakany'oka.
Palikuwa na viwanda na mashamba ya mkonge telee. Haviwapi sasa? Utafikiri mamiye mwali aliyefunga kizazi bwana, maana havizalishi ati, vyote viko, nyang'anyang'a.
Hali hii kutupa vitu njia panda, yaonyesha kabisa tayari maisha yeshatushinda.
Watu kilo siku waenda kwa waganga, ukipita pale mara kumevunjwa nazi, mara huku nako kule kumetupwa hirizi, mwatakani basi nyiye wana msiotulia?

KIITIKIO
Tanga, kunani paleee,
mbona kila kitu pale kimekufa,
Tanga, kunani paleee,
mbona maisha pale yanasikitisha.


(verse 2)
lshi Tanga lakini kuwa makini,
watu wajua mpaka siri zako za
ndani, sijui habari hizi huwa waambiwa
na nani?

Hospitali ya Bombo ya leo ni vichekesho,
ukienda pale hata kama utumbo uko nje,
utaambiwa tu matibabu kesho.
Tanga, Tanga jamani yarabi toba.
Ndege pia kwa mwezi twaona mara moja,
basi balaa hili watu tumekuwa twaishi maisha ya
tumbiri,
sijui tusomeane alubadili,
ili tumkamate alotu filisi utajiri.
Bandari nayo sasa yachungulia shimo,
zamani waweza ona miji meli palee
wala haina kipimo, lakini! sasa hivi si meli tena,
wala hazina uwezo wa kubeba hata kontena.
Ukiondoa Wahindi na Waarabu,
Waswahili wenye pesa ni wa kuhesabu,
halafu wikiendi angalia nyendo zao,
kuchukua wake za watu na kutaka mambo nje ya
uwezo wao.

Saruji ndo kiwanda arnbacho
kimebakia, panga pangua makaburu wameingia ubia. watafanyabiashara miaka mitano haifiki nao wale pia watajiondokea

Railway kimyaa, zamani wenyewe
pale tulishaizoea mijihoni, sasa hivi
behewa moja la abiria hatulioni,
mwawekani basi mabehewa
yaloozana pale. Si muondoe jama
yaleta mafico wezi yale.

KIITIKIO
(verse 3)
Hatijawahi kulalamika sisi hata
siku moja,najuu ya maisha ya Tanga MC natoa hoja, msije mkaona mzaha jamani hivi si vioja,
kucheka mtacheka lakini mkoa unadoda
Viongozi wetu kazi yao hawajui hata moja,
vikao vyao n'vingi wanakutana Mkonge Hotei,
na agenda za huko hawatiambii ukweli.

Promise zao ni za uongo haziambiiki,
sijui wametuona mma'bahau ama m'visiki,
Tinapomichagua majukumu yenu mnayatambua?
Au mnaona raha dada zetu kuuza vitumbua?

Titabeba zege mpaka lini na kujitutumua?
Inaelekea mmetisahau halafu pesa mnazitumbua.
Na huu mpango mpango wa Tanga wa vipande vya baiskei,
titakuja kutoana roho mchana mchana aisee, tinashikwa na mgambo ili tilipie manispaa,
wakati wagosi wa kaya wenyewe ti nakufa na njaa. asalam alekum wallahi
Ndio maana akili zetu mnasema hazifai,
na asubuhi ni mnazi badala ya chai.
Pamoja na viwanda na upuuzi huo kufa,
elimu tinaichezea halafu kingereza n'cha ugoko. Tisibishane hapoo!
Sasa tirudi katika suala ya maendeleo,
tinapataje mtaji kwa ajili ya haya maendeeo?
Kama si kupakiza magunia kwenye Shengena,
tinalipwa hela kidogo haafu tinasengenywa.
Chai asubuhi ni kavu hakuna cha kutafuna,
watoto wamezoea ubwabwa siku huna hela wananuna,

Wake zetu wamekakamaa utadhani wanafanya diet, haku nacha diet hapo ukapa umepanda chati
Na ukitaka kujua n'balaa kwa haya tinayosema,
uwanja wa sabasaba umekufa, hata jumba ya sinema.
Msije mkani kumbusha mimi hapa naweza kulia.
Oh Tate none wa Tanga tushikamane.
Mike Byanaku ni fundi mzuri wa baiskeli,
anasaidia sana lazima niseme ukweli.
Anapogonga nyundo Wahindi wanasema n'kelele,
nntafutieni nyundo yasailensa aondoe hizo kelele.

Na nyie na magari yenu msipige honi wala misele, hapo titaelewana.
Tanga tina barabara maarufu na ziko ishirini na moja, na hizi zimejipanga panga na ni hatari kwa vioja,
tega sikio usikie ni kitu gani kinakuja.

Tinao akina kaka wanaoshikishwa ukuta,
wengine wanajifanya waswalihina wanakula kitimoto, hatiwasemi tinaogopa mkong'oto.
Tanga Wahindi wamejazana kwenye maghorofa ya msajii,
tunabaki kuhangahanga Kwanjeka sisi waswahii, ukipita chini ya ghorofa wanakutemea mate ya paliki
Ukiuliza hivi n'kwa nini matusi yake hayaambiiki.
Weee Master J!
Kuna siku n'tampandia mtu ghorofani nimtoe roho, halafu n'pelekwe kwenye gereza la Maweni n'kanyee ndoo.
Timeshachanganyikiwa mnatiletea ubishoo.
Juhudi zako zinaonekana sana Kapteni Mkuchika. Afadhali sasa kidogo Tanga tinahema na kucheka.
Maneno tinayoongea hapa hatumpigi mtu kamba, Wagosi tinamalizia na salamu kwa Makamba.
Baba yetu Makamba,
hawa akina matonya hawako tu pekee Daisaama, hata kule Tanga wamejazana ni kiama.

KIITIKIO

No comments:

Post a Comment