Hili ni darasa jipya lililojengwa sasa katika Shule ya Msingi Silabu iliyopo Wilaya ya Korogwe darasa hili linatumiwa na wanafunzi wa darasa la tatu
Mti huu kivuli chake ni ofisi ya walimu wa Shule ya Msingi Silabu iliyopo Wilaya ya Korogwe
Uchochoro huu ndio lililuwa darasa la tatu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Silabu iliyopo Wilaya ya Korogwe
Na Mwandishi wa Thehabari.com Korogwe WALIMU wa Shule ya Msingi Silabu Wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga bado wanatumia kivuli cha mti uliopo mbele ya shule hiyo kama ofisi ya walimu (staff room) kwa kukosa jengo la ofisi.
Hiki
ni kipindi cha miezi sita imepita sasa tangu mtandao wa Thehabari.com uripoti habari
hii mapema mwezi Agosti 2012.
Juzi mwandishi wa habari hizi alipita tena katika shule hiyo kuangalia
juhudi za Serikali na wananchi kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo, lakini
alishuhudia walimu wa shule hiyo wakiendelea kufanya shughuli zao chini
ya mtimu.
“…Hii
ndiyo ofisi yetu bado,jengo ambalo tutalitumia kama ofisi halijajegwa
shuleni hapa, hivyo tunatumia kivuli cha mti huu kama ofisi na wakati
mwingine jua likizidi huamia pembezoni mwa kingo za darasa lenye
kivuli,” alisema mmoja wa walimu ambaye alikutwa amekaa chini ya mti
huku akiendelea na kazi.
Hata
hivyo mwalimu huyo hakuwa tayari kutaja jina lake kwa madai si msemaji
wa shule hiyo, juhudi za kumpata Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Silabu,
Mizeki Charahani ziligonga ukuta baada ya kuambiwa alikuwa nje ya shule
kikazi.
Awali
mwezi Agosti mwandishi wa habari hizi aliripoti wanafunzi wa darasa la
tatu katika Shule hiyo kusomea kwenye uchochoro unaotenganisha kati ya
darasa moja na lingine kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.
Wanafunzi hao ambao darasa lao lilikuwa likihama kila muda kutengemea
hali ya hewa (jua na mvua) kufuata kivuli walilazimika kusomea nje
kwenye uchochoro ambao haujaezekwa kutokana na uhaba wa vyumba vya
madarasa shuleni hapo.
Hata
hivyo tayari limejengwa darasa moja ambalo kwa sasa linatumiwa na
wanafunzi wa darasa la tatu, huku darasa la kwanza na la pili
wakiendelea kusomea kwenye darasa moja kutokana na uhaba wa vyumba vya
madarasa unaoikabili shule hiyo, yenye darasa la kwanza hadi la saba.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment