Miss East Africa Jocelyne Maro 2012
Jocelyne
Maro Miss East Africa Tanzania akipunga mkono kwa mashabiki wake mara
baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa
kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
akiwashinda warembo wenzake kutoka mataifa mbalimbali ya Ukanda wa
Afrika Mashariki na nchi Jirani na Ukanda huo.
Jocelyne
Maro ni Mtanzania wa kwanza kushinda taji hilo tangu lililpoanzishwa,amejinyakulia zawadi zenye thamani ya dola za kimarekani 30,000 likiwemo
Gari aina ya Toyota Verossa, mara baada ya majaji kumtangaza mrembo
huyo ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe huku watu mbalimbali
wakimpongeza kwa ushindi wake.m
Miss East Africa Jocelyne Maro akipongezwa na wenzake mara baada ya kushinda katika shindano hilo.
o
Miss
East Africa Jocelyne Maro akipiga picha ya pamoja na Miss Uganda Ayisha
Nagudi mshindi wa pili katika shindano hilo kushoto na Miss Burundi
Ariela Kwizera ambaye alipata nafasi ya tatu katika shindano hilo.
No comments:
Post a Comment