Sunday, December 23, 2012

COAST UNION YA TANGA YAPATA NAFASI YA PILI KOMBE LA UHAI

Azam mabingwa Kombe la Uhai 2012

 Wachezaji wa Azam wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Uhai kwa kuifunga Coastal Union kwa penalti 3-1 jana kwenye Uwanja wa Karume. Picha na Michael Matemanga 

AZAM imenyakua ubingwa wa Kombe la Uhai kwa kuichapa Coastal Union kwa penalti 3-1, baada timu hizo kutoka sare 2-2 katika dakika 120 kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Shujaa wa Azam alikuwa kipa wao Aishi Manula aliyeokoa penalti tatu kati ya nne zilizopigwa na Coastal Union na kuipa ubingwa timu yake.
Kwa ushindi huo Azam wamejinyakulia kitita cha Sh1.5 milioni, Coastal Union wakiondoka Sh1 milioni, huku mabingwa wa msimu uliopita Simba wakiondoka na Sh500,000 kama washindi wa tatu.
Katika mchezo huo Azam walianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza katika dakika 11 kupitia, Samwel Mkomolo, kabla ya Kelvin Friday kupachika bao la pili kwa mkwaju wa penalti katika dakika 34.
Coastal Union ‘Wagosi Wakaya’ walibadilika kipindi cha pili na kufanikiwa kupata mabao ya kusawazisha yaliyofungwa kwa kichwa kwa kupitia Mohamed Miraji katika dakika 61 na Ally Iddi (77) na kufanya mchezo huo kwenye dakika 30 za nyongeza.
Fainali hiyo ilishudiwa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga, Idd Kipingu na Said Mohamed mwenyekiti wa Azam pamoja na mamia ya mashabiki waliojitokeza kwenye uwanja huo.
Mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Mzee alinyakua Sh300,000 tuzo ya ufungaji bora baada ya kufunga mabao sita, huku mchezaji bora wa mashindano, Joseph Kimwaga wa Azam alipata Sh350,000.
Ruvu Shooting ilitwaa tuzo ya timu yenye nidhamu itakabidhiwa Sh400,000, wakati kipa bora Mansour Ally wa Coastal Union alipata Sh300,000.
Kocha bora Bakari Shime wa Coastal Union alizawadiwa Sh300,000 kama ilivyokuwa kwa mwamuzi bora wa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment