HALMASHAURI ya Jiji la Tanga, imeziteketeza dawa, vipodozi na bidhaa za vyakula ambavyo muda wa kutumiwa kwake, umekwisha.Kwa pamoja, bidhaa hizo zina thamani ya Sh. 13.908,730.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya tukio hilo, Kaimu Mfamasia wa Jiji la Tangam Abdillah Mnenge, alisema dawa hizo zilikamatwa kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali wa jijini hapa .
Mnenge alisema uteketezaji wa dawa hizo, ulifanyika juzi katika dampo kubwa lililoko Duga Maforoni na kwamba ulisimamiwa na wataalamu kutoka katika halmashauri ya Jiji na askari polisi.
Aliiomba Serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuimarisha mipaka na ukaguzi ili kudhibiti uingizwaji wa vipodozi haramu hapa nchini.
Pia aliviomba vyombo vya habari hapa nchini, kutoa elimu juu ya madhara ya utumiaji wa bidhaa ambazo si rafiki wa binadamu na zilivyokwisha muda wake.
Kaimu Mfamasia huyo alisema wataendelea kuimarisha i ukaguzi kila baada ya miezi mitatu katika maeneo yote ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, ili kudhibiti uingizwaji wa bidhaa zilizokwisha muda wake.
No comments:
Post a Comment