Tuesday, January 29, 2013

MUHIMU:::TUSIBEZE TAHADHARI YA MVUA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgh4CL4lD5LoA2aIBpKspBS9GJp_9MBRehN-elzmcwc8e1_Fx8SB2bWInUJ9sOG6Nc-KaKeRetmprw-Elc_SN9d1AzN1Ntn1gE6dQN3WcKpeT6D8EZx2N7PhgxZNU0hAQkKYkoVkQ-BBFE/s1600/FELLENG.jpg

Taarifa kuhusu uwezekano wa matukio ya Mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku) katika baadhi ya maeneo ya mikoa  ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara  na maeneo jirani ya mikoa hiyo kati ya tarehe 30 Januari, 2013 hadi 01 Februari, 2013.
Hali hii inatokana na kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu kutoka Congo kupitia maeneo tajwa.

Friday, January 4, 2013

.: KIKWETE AONGOZA MAZIKO YA SAJUKI!

 WAANDISHI NAO WAKISHIRIKI KWA NAMNA YA PEKEE MAZIKO YA SAJUKI!https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhUR2DGLo3FjiHPV6aQQYwxfkkiwCv9YxCB2w0SNNYl7zsXemUC8RPMMorKveFtC37GPVva7jJEamatpwdKQpyM14CrYq10UFPDFIIRIQMrb4y7nx99zW4C1kFDKPd9-RlQmfRlLJN4tBss/s1600/3.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQz_CqTwAKkrDCCoFWYiRipV22fTIgY2U_mku7iNsatN9S3B5wdVeNRYwlLxBAvn0VYFC7n7ncCJkxFf3f_i_6RqL0-QVZwHbOpe-E-Ur2xU0TqQR6su02IHPLLldPpBRF7LD9QeoyzOxD/s640/download.jpg


 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.saju3 1cb9a


Masanja Mkandamizaji akisubiria chepe kutupia dongo kaburini,kushiriki mazishi ya Sajuki
 Masanja akisubia zamu ya kufukia kaburi


 Mbunge wa Kinondoni Idd Azan akiteta jambo na William Malechella
 Mbunge wa kinondoni Iddy Azani akiteta jambo na Wiliiam  Malechela

Wednesday, January 2, 2013

Mbunge wa Handeni mkoani Tanga,Dk.Abdallah Kigoda,amesifu ukamilikaji wa barabara ya Mkata hadi Handeni iliyojengwa na Serikali kwa kiwango cha lami.

 
Mbunge wa Handeni, Abdallah Kigoda
Na Mashaka Mhando, Handeni
MBUNGE wa Handeni mkoani Tanga, Dk. Abdallah Kigoda, amesifu ukamilikaji wa barabara ya Mkata hadi Handeni iliyojengwa na serikali kwa kiwango cha lami hatua ambayo amesema itarahisisha mawasiliano kwa wananchi wa wilaya hiyo.
"Kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yangu, nimetembelea Jimbo langu kutoka nyumbani kwangu mjini Handeni, kwenda Mkata na kufanya mikutano ya hadhara, nikarudi kwa kupitia njia ya lami pekee, ni faraja kubwa sana, tuitunze, haya ni moja ya maendeleo ya wilaya yetu hii" alisema Dk Kigoda.
Dk Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, aliyasema hayo juzi alipokwa kwenye ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi wilayani humo kwa kufanya mikutano katika kata ya Mkata ikiwemo kukutana na wapiga kura wake.
"Haikuwa kazi rahisi kufanikisha kupitisha bajeti ya ujenzi wa barabara hizi za Handeni-Mkata, Handeni-Korogwe na Handeni-Mvomero. Namshukuru sana Rais Jakaya Kikwete pamoja na Bunge kwa kuweza kupitisha ujenzi wake," alisema Dk Kigoda.
Alisema anapotumia barabara hizo amekuwa akiwafikiria watu wake wa karibu, ambao walipigania kupata barabara hizo kwa kiwango cha lami. Lakini sasa hawapo tena duniani, hivyo alitamani nao waone matunda ya kuwa na subira.
Kuhusu suala la maji mbunge huyo alisema wanakabiliwa na mkakati mzito wa kujenga upya Mradi wa Maji wa Handeni Trank Man (HTM), wa kutoka mto Pangani (Ruvu) ili wananchi walio wengi waweze kuondokana na kero ya maji.
Waziri huyo alisema changamoto kubwa iliyobaki wilayani humo sasa ni upungufu wa maji, akisema kwa hesabu ya mwaka jana 2011, Handeni ilikuwa inahitaji kiasi cha Sh 120 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo wa HTM ambao tangu umejengwa mwaka 1978 na rais wa sasa wakati huo akiwa Waziri wa maji, haujafanyiwa ukarabati.
Alisema hata hivyo wanaendelea na jitihada za kutafuta wafadhili na Bajeti ya Serikali, ambapo wanaendelea kuchimba visima virefu na vifupi pamoja na mabwawa katika maeneo mbali mbali ili kupunguza makali ya uhaba wa maji kwa wananchi.
Dk Kigoda aliwashukuru na kuwapongeza wafanyabiashara wilayani humo hasa wa mjini Handeni, kwa kuiunga mkono Serikali kuchimba visima virefu ambavyo vimesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza shida ya maji mjini hapa, ambapo sasa ndoo ya maji huuzwa Sh 100 visimani, badala ya Sh 500 za awali.

Dk Kigoda ambaye ni Waziri wa Viwanda na Biashara pia ni Mbunge wa Handeni akihutubia wananchi katika vijiji mbalimbali vya Kata za Kwamsisi, Kwasunga na Kwaluguru, Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Dk Kigoda alisema kuwa, wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya kati ya 45 nchini, zinazokabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula, kutokana na eneo hilo kukumbwa na ukame mkali.

 
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amebainisha kuwa, wilaya zaidi ya 45 nchini ziko hoi kwa ukosefu wa  chakula, sababu ikielezwa kuwa ni kukithiri kwa ukame.
Waziri huyo amewaonya wafanyabiashara kuwa na utu kwa kuacha kuwaumiza wananchi kwa kupandisha bei ya chakula.
Akihutubia wananchi katika vijiji mbalimbali vya Kata za Kwamsisi, Kwasunga na Kwaluguru, Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Dk Kigoda alisema kuwa, wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya kati ya 45 nchini, zinazokabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula, kutokana na eneo hilo kukumbwa na ukame mkali, hivyo kusababisha baadhi ya wakazi wake kula mboga za majani.
Kufuatia upungufu huo wa chakula, kumesababisha mfumko mkubwa wa bei ya mahindi na unga wa sembe kuwa juu, ambapo, Handeni gunia moja la kilo 100 za mahindi limefikia kuuzwa kati ya Sh90,000 hadi Sh100,000, kiwango ambacho hakijawahi kutokea wilayani humo.
Dk Kigoda ambaye pia ni Mbunge wa Handeni, alikutana na changamoto kubwa ya wananchi kumlilia chakula cha msaada ama kinachoweza kuuzwa kwa bei nafuu vijijini, wakidai wengi wao wanakula mlo mmoja kwa siku au kukosa kabisa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kwamsisi, Athumani Mwagahazi, alimweleza waziri huyo kuwa, wananchi wengi katika eneo hilo sasa wanaishi kwa kula maembe ya kuchemsha pamoja na majani ya mchunga.
Akizungumzia hali hiyo Dk Kigoda aliwaeleza wananchi hao kwamba, Serikali inatarajia kusambaza chakula kinachotarajiwa kuuzwa kati ya Sh700 hadi Sh850 kwa Mkoa wa Tanga, ambao unatarajiwa kuwafikia wananchi wiki hii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Hassan Mwachibuzi, alisema kwamba wanatarajia kupata tani 150 za unga wiki hii, utakaouzwa Sh750 na 900 kwa kilo moja vijijini katika Mkoa wa Tanga.

 Aina mbalimbali za vyakula
 
Mwachibuzi alisema bei hizo zinatofautiana kutokana na gharama za usafirishaji kutoka Jijini Dar es Salaam na maeneo ya mkoa huo, akisema kwa wilaya ya Handeni ambayo ndiyo iliyopo karibu na jiji hilo, kitauzwa na wafanyabiashara kwa bei ya Sh750.

Mmwanafunzi wa kidato cha pili katika Sekondari ya Kiparang’anda wilayani Mkuranga mkoani Pwani, Ismail Mohamed (15), amefariki baada ya kuchomwa kisu na kijana mwenzake!

Akisimulia tukio hilo, katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani (Maturubai), Mjomba wa Marehemu, Nurdin Mohamed aliliambia Mwananchi, lililoambatana na kikosi cha doria cha Polisi Temeke kuwa mtuhumiwa alimchoma kisu Mohamed kifuani, baada ya kumnyima Sh200.

 hii picha sio halisi

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Sekondari ya Kiparang’anda wilayani Mkuranga mkoani Pwani, Ismail Mohamed (15), amefariki baada ya kuchomwa kisu na kijana mwenzake, Ramadhani Mkamba (19), wakati wa mkesha wa Mwaka Mpya.
Tukio hilo lilitokea saa 5:20, usiku wa mkesha wa mwaka katika eneo la CCM II Mbagala Kiburugwa, maarufu kama Magenge 20, tukio ambalo chanzo chake ni Sh200.
Akisimulia tukio hilo, katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani (Maturubai), Mjomba wa Marehemu, Nurdin Mohamed aliliambia Mwananchi, lililoambatana na kikosi cha doria cha Polisi Temeke kuwa mtuhumiwa alimchoma kisu Mohamed kifuani, baada ya kumnyima Sh200.
Alisema Mohamed ambaye alikuwa amefika nyumbani kwake hapo kwa ajili ya likizo, alikutana na mtuhumiwa huyo wakati akitoka magengeni ambapo walikuwa wakifanya biashara ya kuuza samaki.
Alisema mtuhumiwa alimwomba Mohamed Sh200 lakini alisema hana, mtuhumiwa alimpora simu yenye thamani ya Sh20,000, halafu akamchoma kisu kifuani kisha akakimbia.
Alisema baada ya mtuhumiwa kumchoma kisu Mohamed na kukimbia, yeye alimchukua majeruhi na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani, ili aweze kupata fomu namba 3 ya Polisi kwa ajili ya matibabu, lakini wakati taratibu za kupata fomu hiyo zikiendelea, majeruhi alifariki.
Mtuhumiwa alifuatiliwa na kikosi cha doria ambacho kilifanikiwa kumtia mbaroni na kumfikisha kituoni hapo.
Katika tukio lingine, dereva teksi mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel Magori anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 na 40, amenusurika kifo baada ya kuchomwa kisu tumboni na majambazi na kisha kumpora gari.
Tukio hilo lilitokea kati ya saa 6:15 na saa 6:30, usiku wa kuamkia Mwaka Mpya , katika eneo la Imasko wilayani Temeke.
Baadhi ya wananchi walishauri Watanzania kuwa makini hasa katika nyakati za sikukuu ili kuepuka hali kama hizo.

ewura yashusha bei ya mafuta,kitendawili kilichobaki kwa wananchi ni kwamba JE NAULI NAZO ZITASHUKA? au ndio!!!!!!!!!!!!!

 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei kikomo cha bidhaa za mafuta kinayoonyesha kuwa petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeshuka kuanzia leo.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu imesema bei hizo zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 5, mwaka jana.
“Katika toleo hili, bei za rejareja kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa, zimepungua kwa viwango vifuatavyo: petroli Sh126 kwa lita sawa na asilimia 5.96; dizeli Sh32 kwa lita sawa na asilimia 1.60 na mafuta ya taa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.50,” imeeleza taarifa hiyo.
Kwa punguzo hilo, bei ya rejareja ya petroli katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh1,993, dizeli Sh1,967 na mafuta ya taa Sh1,973. Arusha petroli ni Sh2,077, dizeli Sh2,051 na mafuta ya taa Sh2,057.
Katika jiji la Mbeya petroli itauzwa kwa Sh2,099, dizeli Sh2,074 na mafuta ya taa Sh2,079 na jijini Mwanza, petroli itauzwa kwa Sh2,142, dizeli Sh2,117 na mafuta ya taa Sh2,122.
Taarifa imefafanua kuwa mbali na kupungua bei hiyo katika uuzaji wa rejareja, bei pia imepungua kwa katika uuzaji wa jumla ikilinganishwa na matoleo mawili yaliyopita.
“Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepungua kama ifuatavyo: petroli kwa Sh126.10 kwa lita sawa na asilimia 6.17; dizeli kwa Sh32.48 kwa lita sawa na asilimia 1.69 na mafuta ya taa kwa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.6,” alisema.
Mkurugenzi huyo amesema katika taarifa hiyo kuwa mabadiliko hayo ya bei, yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.
Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli, zitaendelea kupangwa na soko.
“Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuzi wa bidhaa za mafuta,” alisema Masebu.
Hata hivyo, Masebu alisema pamoja na mpango huo wa Ewura kuweka bei ya kikomo, kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa hizo kwa bei ya ushindani, ilimradi ziwe chini ya bei hiyo kikomo.
Alivitaka vituo vya mafuta kuchapisha bei hizo mpya katika mabango yanayoonekana bayana na kuonyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.
“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika,” alisema.
Masebu aliwashauri wanunuzi kuchukua stakabadhi ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita ili itumike baadaye kama kidhibiti endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko ya kikomo au yenye kiwango cha ubora kisichofaa.


Mahakamani kwa kubaka mwanafunzi

 
KADA maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Shafii Yatera (40), ameuanza vibaya mwaka 2013 baada ya kusherehekea Mwaka Mpya akiwa Gereza Kuu la Karanga mjini Moshi.
Yatera  alipandishwa  kizimbani juzi mbele ya Hakimu mkazi, Sophia Masati
akikabiliwa na tuhuma za kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Msasani.
Kada huyo ndiye ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 alichuana na Mbunge wa sasa wa Jimbo la Mwanga ambaye pia ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na kushika nafasi ya pili.
Akimsomea mashtaka yake, Wakili wa Serikali Kanda ya Moshi, Oscar Ngole alidai kuwa Novemba 1,2012, mshtakiwa alimwingilia kimwili mwanafunzi huyo wa Kidato cha Nne kinyume cha sheria.
Wakili huyo alidai kuwa kitendo alichokifanya mtuhumiwa huyo ni kinyume cha kifungu 130 (2) (e) na 131 cha kanuni ya adhabu sura ya 16, adhabu ya kosa hilo ni  kifungo cha miaka 30 jela.  Hata hivyo kada huyo wa Chadema ambaye ni mkazi wa Pasua mjini Moshi alikanusha mashtaka hayo lakini upande wa mashtaka ukaiomba mahakama kuzuia dhamana kwa sababu za kiupelelezi.
Wakili Ngole, alidai kuwa endapo mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana ataathiri uchunguzi wa kesi hiyo kwa kile kinachodaiwa amekuwa akimshawishi mwanafunzi huyo kutokutoa ushirikiano kwa polisi.
Hakimu Masati anayeisikiliza kesi hiyo alilikubali ombi hilo la upande wa mashtaka na kuamuru mshtakiwa apelekwe rumande katika Gereza Kuu la Karanga hadi Januari 14, 2013 kesi hiyo itakapotajwa tena.

Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.

Enzi za uhai wake marehemu Sajuki kulia akiwa na mkewe Wastara,Kila mmoja alimpenda sana mwenziwe.pumzika kwa amani ndugu yetu Sajuki.

Taarifa za uhakika ni kwamba kweli mwigizaji Sajuki amefariki dunia leo asubuhi (Jan,2 2013) katika hospitali ya Muhimbili. Alilazwa hapo kwa wiki mbili ambapo alikua anasubiri kupata urahisi wa kusafiri kurudi India kwenye matibabu ambayo alipangiwa kurudi tena december 2012. Sajuki alikua na tatizo kubwa la kupumua wakati huu ambapo Dinno amethibitisha kwamba upumuaji wake ulikua unabadilika mara kwa mara. Baada ya kuhangaika sana, dakika za mwisho ndio walikua wamepata ndege ambayo imekubali kutoa huduma ya gesi kwa Sajuki ambapo Shirika la ndege la Emirates ndio lilikua limekubali kutoa huduma hiyo kumsafirisha mpaka India.

Msiba upo Tabata,mazishi ni siku ya ijumaa makaburi ya Kisutu,Mwenyenzi Mungu amlaze mahala pema Sajuki.

 Waombolezaji wakiwa kwenye msiba wa Sajuki Tabata jijini Dar es Salaam leo, Januari 2, 2013.


 Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Sajuki leo wakimfariji mjane Januari 2, 2013.