Enzi za uhai wake marehemu Sajuki kulia akiwa na mkewe Wastara,Kila mmoja alimpenda sana mwenziwe.pumzika kwa amani ndugu yetu Sajuki.
Taarifa za uhakika ni kwamba kweli mwigizaji Sajuki amefariki dunia leo asubuhi (Jan,2 2013) katika hospitali ya Muhimbili.
Alilazwa hapo kwa wiki mbili ambapo alikua anasubiri kupata urahisi wa kusafiri kurudi India kwenye matibabu ambayo alipangiwa kurudi tena december 2012.
Sajuki alikua na tatizo kubwa la kupumua wakati huu ambapo Dinno amethibitisha kwamba upumuaji wake ulikua unabadilika mara kwa mara.
Baada ya kuhangaika sana, dakika za mwisho ndio walikua wamepata ndege ambayo imekubali kutoa huduma ya gesi kwa Sajuki ambapo Shirika la ndege la Emirates ndio lilikua limekubali kutoa huduma hiyo kumsafirisha mpaka India.
Msiba upo Tabata,mazishi ni siku ya ijumaa makaburi ya Kisutu,Mwenyenzi Mungu amlaze mahala pema Sajuki.
Waombolezaji wakiwa kwenye msiba wa Sajuki Tabata jijini Dar es Salaam leo, Januari 2, 2013.
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Sajuki leo wakimfariji mjane Januari 2, 2013.
No comments:
Post a Comment