Wednesday, January 2, 2013

Mmwanafunzi wa kidato cha pili katika Sekondari ya Kiparang’anda wilayani Mkuranga mkoani Pwani, Ismail Mohamed (15), amefariki baada ya kuchomwa kisu na kijana mwenzake!

Akisimulia tukio hilo, katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani (Maturubai), Mjomba wa Marehemu, Nurdin Mohamed aliliambia Mwananchi, lililoambatana na kikosi cha doria cha Polisi Temeke kuwa mtuhumiwa alimchoma kisu Mohamed kifuani, baada ya kumnyima Sh200.

 hii picha sio halisi

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Sekondari ya Kiparang’anda wilayani Mkuranga mkoani Pwani, Ismail Mohamed (15), amefariki baada ya kuchomwa kisu na kijana mwenzake, Ramadhani Mkamba (19), wakati wa mkesha wa Mwaka Mpya.
Tukio hilo lilitokea saa 5:20, usiku wa mkesha wa mwaka katika eneo la CCM II Mbagala Kiburugwa, maarufu kama Magenge 20, tukio ambalo chanzo chake ni Sh200.
Akisimulia tukio hilo, katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani (Maturubai), Mjomba wa Marehemu, Nurdin Mohamed aliliambia Mwananchi, lililoambatana na kikosi cha doria cha Polisi Temeke kuwa mtuhumiwa alimchoma kisu Mohamed kifuani, baada ya kumnyima Sh200.
Alisema Mohamed ambaye alikuwa amefika nyumbani kwake hapo kwa ajili ya likizo, alikutana na mtuhumiwa huyo wakati akitoka magengeni ambapo walikuwa wakifanya biashara ya kuuza samaki.
Alisema mtuhumiwa alimwomba Mohamed Sh200 lakini alisema hana, mtuhumiwa alimpora simu yenye thamani ya Sh20,000, halafu akamchoma kisu kifuani kisha akakimbia.
Alisema baada ya mtuhumiwa kumchoma kisu Mohamed na kukimbia, yeye alimchukua majeruhi na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani, ili aweze kupata fomu namba 3 ya Polisi kwa ajili ya matibabu, lakini wakati taratibu za kupata fomu hiyo zikiendelea, majeruhi alifariki.
Mtuhumiwa alifuatiliwa na kikosi cha doria ambacho kilifanikiwa kumtia mbaroni na kumfikisha kituoni hapo.
Katika tukio lingine, dereva teksi mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel Magori anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 na 40, amenusurika kifo baada ya kuchomwa kisu tumboni na majambazi na kisha kumpora gari.
Tukio hilo lilitokea kati ya saa 6:15 na saa 6:30, usiku wa kuamkia Mwaka Mpya , katika eneo la Imasko wilayani Temeke.
Baadhi ya wananchi walishauri Watanzania kuwa makini hasa katika nyakati za sikukuu ili kuepuka hali kama hizo.

No comments:

Post a Comment