Tuesday, February 5, 2013

kikao kazi cha maafisa habari wa serikali Dodoma

Picha na 1 f90c5Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifungua mkutano wa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine amewataka kufanya kazi  kwa kuzingatia weledi na kutoa taarifa sahihi kwa umma mara kwa mara kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali.


Picha no 8 03ec7
 Mmiliki na muendeshaji wa mtandao wahabari na matukio wa Mjengwa Blog kutoka Iringa Bw. Maggid Mjengwa akitoa mada kwa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali kuhusu Faida na Changamoto za matumizi ya mitandao ya kijamii kwa Mawasiliano Serikalini mjini Dodoma.


Picha na 7 f660a
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi chao kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma.


Picha na 2 5c000
Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi hicho  mjini Dodoma.


Picha na 3 958db
Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabuza Serikali  Sarah Reuben akichangia moja ya mada katika kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma.


hab1 55f16
Baadhi ya maafisa habari wa serikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiAwasilishwa katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Bw. Peter Millanzi mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bw. Midradji Maez, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Bw. Abel Ngapemba, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Shiririka la Maendeleo la Taifa NDC


hab2 6bb7f
. Maafisa Habari kutoka wilaya na Mikoa mbalimbali waliohudhuria kikao kazi cha maafisa habari mjini Dodoma wakiwa katika majadiliano ya pamoja kuhusu mafanikio na changamoto zinzoyakabili maeneo yao ya kazi.


hab3 bf999
Maafisa Habari kutoka wizara mbalimbali waliohudhuria kikao kazi cha maafisa habari mjini Dodoma wakiwa katika majadiliano ya vikundi kuhusu mafanikio na changamoto zinazoyakabili maeneo yao ya kazi wakiongozwa na mwenyekiti wa kikundi hicho Luteni Kanali Juma Sipe, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano.


hab 50c83
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akiwasilisha mada kuhusu mkakati wa Mawasiliano wakati wa Kikao kazi cha maafisa habari wa serikali kinachoendelea mjini Dodoma.

5/2/2013, Dodoma
Kikao kazi cha Maafisa habari wa Serikali kutoka Wizara, taasisi, wakala wa serikali, mashirika ya umma, mikoa na wilaya mbalimbali nchini leo kimeingia siku ya pili mjini Dodoma kwa  maafisa hao kupata fursa ya kujadili changamoto zinazokabili vitengo vya  habari na mawasiliano serikalini na namna ya kuzitatua.
Katika kikao hicho mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo ile ya Mwongozo wa Ofisi za Mawasiliano serikalini iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Msaidizi kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) anayeshughulikia uratibu wa vitengo vya mawasiliano serikalini akitoa msisitizo mkubwa  kwa maafisa habari kuyafahamu vizuri majukumu yao ya kazi kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma ili kuboresha utendaji wa kazi.
 Pia maafisa hao wamepata fursa ya kujifunza namna ya kuboresha  mawasiliano serikalini kupitia mada ya mkakati wa mawasiliano (Communication Strategy) wa kuiwezesha jamii kupata taarifa sahihi kwa muda muafaka ,mada iliyowasilishwa na Meneja mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy.
Katika mada hiyo Bw. Mungy ametoa wito kwa maafisa hao kuzitumia nafasi zao kutoa taarifa kwa umma mara kwa mara ili kuwapa fursa wananchi kufahamu yale yanayofanywa na serikali.
Ametoa wito maafisa hao kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari katika kutekeleza mkakati huo kwa kuhakikisha kuwa wanatoa habari kwa umma kupitia radio, magazeti, televisheni na mitandao ya kijamii ili kuepusha madhara yanayoweza ku.sababishwa na jamii kukosa taarifa sahihi za serikali za utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo

No comments:

Post a Comment