Kihistoria Mkoa wa Tanga ulitumiwa sana na wakoloni wa Kireno, Kiarabu, Kijerumani na Kiingereza ikiwa lango la biashara na uchumi kwa kuunganisha sehemu za ndani za Afrika Mashariki na Kati na sehemu mbalimbali za Dunia kupitia bahari ya Hindi.
Monday, December 31, 2012
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete Ametangaza Matokeo Ya Sensa Ya Watu Na Makazi Ambapo Watanzania Waongezeka Kutoka Watu Milioni 34.4 Hadi Kufikia Watu Milioni 44.9,Rais Kikwete Awataka Watanzania Kupunguza Kasi Ya Kuzaliana.
Ramani ya Tanzania.
Tanzania bara kuna watu 43.6 milioni na Zanzibar watu 1.3milioni.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja kwenye bango linaloonyesha idadi ya watu Tanzania na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Akizungumza katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa uzinduzi huo, Rais Kikwete ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali wa kitaifa, alisema kuwa matokeo hayo ni ishara kwamba ifikapo mwaka 2016 kuna uwezekano wa idadi hiyo kufikia milioni 51 jambo ambalo linaweza kuwa ni mzigo kwa taifa, jamii na hata katika masuala ya uchumi.
Sensa hii ni ya tano kufanyika tangu Muungano ambapo ya kwanza ilifanyika
mwaka 1967 na idadi ya watu ilikuwa milioni 12,313,469, bara wakiwa milioni
11,958,654 na visiwani 354,400.
Alisema
kuwa sensa ya kwanza ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za mwisho zilifanyika
baada ya Uhuru katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002.
Kulingana
na sensa ya mwisho iliyofanyika Agosti 2002, idadi ya watu nchini ilikuwa
34,443,603.
Sunday, December 30, 2012
Dijitali Kuanzia Dar Pekee,Mwanza, Tanga, Mbeya baadaye
Wananchi wakiwa kwenye foleni ya kununua ving'amuzi vya Startimes eneo
la Bamaga jijini Dar es Salaam jana katika siku za mwisho kabla Mamlaka
ya Mawasiliano nchini (Tcra) kuhamisha matangazo ya televisheni kutoka
mfumo wa Analojia kwenda digitali.Picha na Silvan Kiwale
WAKATI zimebakia saa 24 Tanzania kuungana na nchi nyingine
duniani kuanza kurusha matangazo ya televisheni kwa mfumo wa Dijitali
zikiachana na ule wa Analojia, imebainika kuwa mpango huo utaanzia Mkoa
wa Dar es Salaam pekee.
Habari za ndani kutoka Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), zilizolifikia Mwananchi Jumapili, zinaeleza kuwa Jiji
la Dar es Salaam pekee, ndiyo litakuwa la kwanza kuingia kwenye mfumo
huo kuanzia Januari mosi, 2013 na siyo mikoa mingine nchini.
TCRA, imeshatangaza kuwa itaufunga mfumo wa analojia ifikapo Desemba 31 mwaka huu yaani kesho.
TCRA, imeshatangaza kuwa itaufunga mfumo wa analojia ifikapo Desemba 31 mwaka huu yaani kesho.
Habari hizo zimeeleza kuwa mamlaka hiyo imeamua
kuchukua hatua za tahadhari katika utekelezaji wa mpango huo muhimu, kwa
kuanza na mji mmoja baada ya mwingine, ambapo mwezi mmoja baada ya Dar
es Salaam kuanza kutumia mfumo wa dijitali, utafuatia Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma
alipoulizwa aliliambia gazeti hili jana kwamba mamlaka yake itatoa
ufafanuzi kuhusu suala hilo leo katika mkutano wake na waandishi wa
habari.
“Hatuwezi kukurupuka katika suala hili, tuko
makini, lakini kesho (leo), tutakuwa na mkutano wa wanahabari kwa ajili
ya kueleza mikakati mbalimbali na jinsi tulivyojipanga katika jambo
hili,” alisema Profesa Nkoma.
Tayari TCRA imetaja miji mingine mbali ya Dar es
Salaam ambayo imeshaunganishwa katika mfumo wa dijitali kuwa ni pamoja
na Arusha, Mwanza, Tanga, Mbeya, Moshi na kwa sasa mji wa Morogoro
unajengewa miundombinu husika.
Habari zaidi zilieleza kuwa kwa utaratibu uliopo
sasa itachukua miezi kadhaa kabla ya kuzimwa kwa mfumo wa analojia
katika miji minane ya awali, ambapo pia itachukua muda mrefu zaidi
kuzimwa mfumo huo nchi nzima.
Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU),
limezitaka nchi zote duniani kuhamia kwenye mfumo huo wa kurusha
matangazo ya televisheni wa dijitali kutoka mfumo wa analojia ifikapo
Julai 2015.
Ikiwa nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki (EAC), Tanzania imeanza kutekeleza azimio la nchi hizo
ilizozitaka kufanya hivyo mwaka huu wa 2012, badala ya kusubiri hadi
tarehe ya mwisho iliyowekwa na ITU.
Wakati Tanzania ikiwa mstari wa mbele kuhamia
kwenye mfumo huo wa dijitali, ingawa kwa mtindo wa awamu, nchi nyingine
wanachama wa EAC hasa Kenya na Uganda bado hazijaingia katika mfumo huo.
TCRA imezikabidhi kampuni tatu kufanya kazi ya
usambazaji wa mfumo huo wa dijitali, ambazo ni Basic Transmissions
inayoundwa na Kampuni za IPP Media na Sahara
Communications, Kampuni ya Ting ya Agape Associates na Star Media Tanzania Limited (Startimes) ambayo ina ubia na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Star Communications and Technology ya China.
Communications, Kampuni ya Ting ya Agape Associates na Star Media Tanzania Limited (Startimes) ambayo ina ubia na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Star Communications and Technology ya China.
TCRA imekuwa ikielezea kuwa Tanzania ipo tayari
kujiunga na mfumo huo kwa kuwa asilimia kati ya 22 kati ya 24 ya nchi
ambayo inatumia analojia, tayari imefikiwa na mtandao wa mfumo wa
dijitali, ikijumuisha miji minane ambayo kwa kiasi kikubwa kampuni ya
Startimes imeifikia.
Hata hivyo, utata bado unagubika urushaji huo wa chaneli za bure ambazo ni ITV, Star TV, TBC1, Channel Ten na Eat Africa TV ikielezwa kuwa wamiliki wa vituo hivyo hawataki zionyeshwe bure kwenye kila king’amuzi bali ving’amuzi vyao pekee.

MKUU wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu, ametangaza kufunga ofisi yake kuanzia Januari 3, mwakani hadi Februari 3, atangaza kuhamia kwa wananchi mwezi mzima
Amesema lengo la hatua ni kusimamia kwa vitendo miradi inayohusu kilimo, elimu na ardhi, lengo ikiwa ni kuwaletea wananchi maendeleo.Muhingo katika mahojiano na simu na gazeti hili jana, alisema atatumia muda huo wa mwezi mmoja kusimamia kazi za maendeleo akianza na suala la kuhakikisha vyumba vya madarasa vinapatikana kwa ajili ya kuchukua wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza na wanaojiunga na kidato cha kwanza. “Nitatembea katika tarafa zote saba za wilaya yetu.Nimemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya anipatie kila idara zinazohusika ofisa wa kuwa naye katika kazi hii. Kwa hiyo, nitakuwa na watu wa elimu, ardhi, kilimo, ufugaji wa nyuki na masuala ya wafugaji na wakulima.“Tunaanza na hili la madarasa kwa sababu sitaki mwanafunzi hata mmoja abaki nyumbani kwa kukosa madarasa ya darasa la kwanza na wale waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza,” alisema Muhingo ambaye kitaaluma ni mwalimu na mwandishi wa habari. Alisema katika kilimo, pia wataanza na shule 10 zilizoteuliwa kwa ajili ya kuendesha kilimo cha kisasa na hapo watatumia vocha 300 walizopewa na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na kila shule itakuwa na ekari 10, hivyo kufanya ekari 100. Alisema vocha hizo ni za mbegu, mbolea ya kupandia na kukuzia.Alisema mbali ya kupanda mahindi, pia shule hizo zitapanda mazao ya jamii ya mikunde na nia itakuwa ni kuhakikisha shule zinajitosheleza kwa chakula kwa ajili ya wanafunzi wake. “Namshukuru Waziri Mkuu na Wizara ya Kilimo kwa kutuletea vocha 300. Zitatusaidia sana. Ninataka Handeni inakuwa mfano katika mapinduzi ya kilimo, tukiamua tunaweza,” alisema Muhingo na kubainisha kuwa katika suala la kilimo, baadaye atakuwa na ziara wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kujifunza kilimo cha mananasi.
Mbowe Amtangaza Dr Slaa Mgombea Urais 2015
KUMEKUCHA CHADEMA,Mbowe Amtangaza Dr Slaa Mgombea Urais 2015
Katika Mkutano Mmoja huko Karatu mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtangaza Dr:W.P.Slaa kama mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA mwaka 2015 .
JK Amtembelea Padri Ambrose Mkenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Padri Ambros Mkenda wa Kanisa
Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi
ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es
salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam jana Jumamosi Dsemba 29, 2012 kukupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii wakati akisubiri kufunguliwa geti la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.

Saturday, December 29, 2012
Maalim Seif Ziarani Tanga,Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF anatarajiwa kuhutubia mikutano mitatu ya hadhara katika viwanja vya Tangamano, Kwadiboma Sokoni na Handeni.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bibi Chiku Galawa akimkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika Mkoa huo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na vikosi vya
ulinzi na usalama pamoja na wananchi wa Mkoa wa Tanga, mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa ndege wa Tanga.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na wananchi
mbali mbali waliojitokeza kumpokea wakati walipowasili katika uwanja wa ndege wa
Tanga kwa ziara ya siku mbili. (Picha na Salmin Said, OMKR)

wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema wananchi
wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya uhifadhi wa mazingira ili waweze kuyalinda
na kuepuka kuyachafua.
Amesema
uchafuzi wa mazingira mara nyingi umekuwa ukisababishwa na wananchi wenyewe,
jambo ambalo linapaswa kupigwa vita kwa wananchi kupatiwa elimu ya mazingira ili
kuepusha uharibifu huo.
Maalim
Seif ameeleza hayo wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga bibi Chiku
Galawa, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga kwa ziara ya siku
mbili.
Amesema
iwapo wananchi wataelimishwa ipasavyo wataweza kujiepusha na uharibifu wa
mazingira, ikiwa ni pamoja na kukata miti kiholela bila ya kuzingatia athari za
kimazingira.
Nae
Mkuu wa Mkoa wa Tanga bibi Chiku Galawa amesema uharibifu wa mazingira ni moja
kati ya changamoto kubwa zinazoukabili Mkoa huo, jambo ambalo linarejesha nyuma
maendeleo ya kiuchumi katika Mkoa huo.
Amesema
Serikali ya Mkoa huo inatafuta njia mbadala ya kutumia nishati nyengine ili
kupunguza matumizi ya kuni ambayo yanachangia ukataji wa miti
kiholela.
“Iwapo
serikali itazuia matumizi ya makaa na kuni, serikali na wananchi watapata nafasi
ya kufikiria nishati mbadala ya kutumia kwa ajili ya kupikia, lakini tukiendelea
kutumia kuni mawazo yetu yatabakia hapo hapo tu na tutaendelea kutumia kuni kila
siku”, alitanabahisha bibi Chiku.
Amesema
ukataji wa miti kiholela katika Mkoa huo umekuwa ukichangia kuwepo kwa athari za
mabadiliko ya tabianchi yanayopelekea kuweko kwa upungufu wa mvua pamoja na
kuongezeka kwa hali ya joto.
Hata
hivyo bibi Chiku amesema Mkoa huo umepiga hatua kimaendeleo, ikiwa ni pamoja na
kuimarika kwa miundombinu ya barabara.
Akiwa
Mkoani Tanga, Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF
anatarajiwa kuhutubia mikutano mitatu ya hadhara katika viwanja vya Tangamano,
Kwadiboma Sokoni na Handeni.
Hassan
Hamad (OMKR)
UTAJIRI WA GESI ASILIA: TUWASIKILIZE WATANZANIA WA MTWARA NA LINDI TUSIPUUZE
Zitto Kabwe
Maandamano
ya amani yaliyofanyika mjini Mtwara siku ya alhamis wiki hii yameibua
hoja mbali mbali kutoka kwa viongozi, wananchi, vyombo vya habari na
mjadala wa siku nzima kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook, twitter
na JamiiForums. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameita waandamanaji wapuuzi na
Waziri wa Nishati na Madini amewaita watu hatari na wahaini. CHADEMA
tumetoa kauli kupitia kwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba
udhaifu wa utendaji serikalini ndio chanzo cha maandamano haya.
Lakini
kuna tatizo kubwa zaidi ambalo linaonekana siyo katika sekta hii tu bali
pia katika sekta nyingine ambapo tunaona matokeo yake katika maisha ya
watu wetu na naweza kusema ni dalili za kushindikana kwa sera za CCM.
Sera hizi ndizo ambazo zimelifikisha taifa hili hadi hapa. Kama hadi
wananchi wa Mtwara ambako kwa muda mrefu imekuwa ni ngombe ya CCM
wanaanza kuhoji matokeo ya sera za chama tawala basi ni dalili kuwa
Watanzania wamefungua macho yao na wanaona.
Wanaona
katika nishati, wanaona katika utawala bora, wanaona katia elimu
(kuanzia ya msingi hadi ya juu kabisa!), wanaona katika afya, wanaona
katika utendaji wa jeshi la polisi wanaona katika madini. Sera za CCM
zimeshindwa. Zimeshindwa kuinua maisha yao na zinaonekana kuendelea
kushindwa.
Mtwara na Lindi wanataka nini?.
Watu wa
Mtwara wanataka gesi isiondoke Mtwara na badala yake viwanda na mitambo
ijengwe Mtwara kisha kama ni umeme au mbolea isafirishwe kupelekwa
sehemu nyingine ya nchi. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba Gesi yote na
mazao yake vibaki Mtwara na Lindi. Wanasema umeme uzalishwe Mtwara
usambazwe nchi nzima. Mbolea izalishwe Mtwara na kusambazwa nchi nzima.
Wanataka Bandari ya Mtwara iboreshwe na kuhudumia mikoa ya Kusini. Watu
wa Mtwara hawasemi kwamba mapato yote ya Gesi yatumike Mtwara tu la
hasha.
Sio
dhambi hata kidogo kwa watu wa Mtwara kudai masuala haya. Watu wa Mtwara
wamefanya maandamano kwa amani kabisa bila kuharibu mali na kutoa maoni
yao. Kwanini tuwasute na kuwasusubika kwa madai yao haya? Kwa nini
tusiwasikilize? Kosa lao nini kudai viwanda ili wapate ajira? Tumesahau
kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni mikoa masikini kabisa nchini?
Tumesahau
kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ilitumika kwa ukombozi wa kusini mwa
Afrika kiasi cha kuwa katika hatari kabisa? Tumesahau ‘sacrifice’ ya
watu wa Mtwara na Lindi dhidi ya usalama wa nchi yetu? Tumesahau kuwa
Korosho imekuwa zao kubwa la biashara na linaloingiza mapato mengi sana
ya Fedha za kigeni? Waziri Muhongo anasema Mtwara warudishe Fedha za
Mkonge na Kahawa. Mbona hataji fedha za Korosho? Mwaka 2011 Korosho
ilikuwa zao la pili kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni baada ya
Tumbaku.
Lakini
tujiulize, watu wa Mtwara na Lindi walifadi fedha za Mkonge? Walifaidi
fedha za Kahawa? Wamefaidi fedha zao za Korosho? Tumesahau hata Reli
iliyoachwa na Mkoloni ya Nachingwea – Mtwara iling’olewa na Serikali
huru ya Tanzania?
Tujiulize
zaidi, hivi watu wa Nzega wamefaidika vipi na Mgodi wa Resolute pale
Lusu? Mgodi umefungwa ukiwa umezalisha na kuuaza dhahabu ya thamani ya
dola za marekani 3.3 bilioni. Hivi katika uhai wa mgodi huu Serikali Kuu
imekusanya kodi kiasi gani? Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepata
ushuru kiasi gani? Watu wa Mtwara wanayaona haya yaliyotokea Nzega na
yanayotokea Tarime, Biharamulo, Kahama na Geita. Watu wa Mtwara wana
Haki kuandamana kuzuia haya yaliyotokea wenzao yasiwatokee wao kwenye
Gesi asilia.
Magufuli Amteua Prof Ninatubu Lema Kuwa Mwenyekiti Wa Bodi (ERB)
Prof Ninatubu Lema kutoka Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET), kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB)
WAZIRI wa Ujenzi, John Magufuli amemteua
Prof Ninatubu Lema kutoka Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET), kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), uteuzi huo unaanzia
Desemba 20 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya
Magufuli iliyosambazwa kweye vyombo vya habari jijini Dar es Salaam
jana, na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Herbet Mrango, ilieleza
kuwa uteuzi huo, utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu hadi Desemba 20,
2015.
Kwa mujibu wa sheria Na. 15 ya
mwaka 1997 ya mabadiliko madogo ya sehemu ya 3(3) ya kifungu 1(1) (a),
na 1(2), kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 24 ya mwaka 2007, ndiyo
iliyomfanya Waziri afanye uteuzi wa wajumbe wa Bodi hiyo akiwemo
mwenyekiti huyo.
Katika uteuzi huo, Magufuli pia
aliwataja wajumbe wanane wa bodi hiyo ya ERB, kuwa ni pamoja na Fintan
Kilowoko kutoka wizara hiyo, ambapo kwa sasa ni mkurugenzi wa Barabara
za Mikoa, Joseph Malongo, ambaye kwa sasa ni Msajili Msaidizi Huduma za
Usajili na Gemma Modu kutoka Baraza la taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE),
Nuberis Nyange kutoka Chama cha Wahandisi Washauri nchini (ACET).
Wengine ni Sarah Barahamoka,
kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Edwin Ngonyani kutoka
Wizara ya Nishati na Madini, Prof Bakari Mwinyiwiwa; Mhandisi
Mwandamizi, Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET), kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es salaam na Prof. John Kandoro; Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia
Dar es Salaam (DIT).
Waziri alisema kuwa jukumu la
msingi la Bodi hiyo ya Usajili wa Wahandisi ni kusajili wahandisi pamoja
na Kampuni zinazotoa ushauri wa kihandisi, kuendeleza wahandisi
kitaaluma, kuwajengea uwezo wa Wahandisi wa kitanzania.
Serikali Yaombwa Kuongeza Fedha Za Mkopo Wa Vijana
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akipokea taarifa ya SACCOS ya Ibwera iliyopo wilayani Bukoba kutoka kwa Benedicta Peter ambaye ni katibu msaidizi. SACCOS hiyo ilipata mkopo wa shilingi milioni tano kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana na kuvikopesha vikundi mbalimbali vya maendeleo vya vijana.
Na: Anna Nkinda – Maelezo, Kagera
Serikali imeombwa kuongeza kiasi
cha mkopo kinachotoa kwa vijana kupitia mfuko wa maendeleo wa vijana na
Halmashauri za wilaya kwani kiwango kinachotolewa kwa sasa cha shilingi
milioni tano kwa vyama vya Kuweka Akiba na Kukopa (SACCOS) ni kidogo
ukilinganisha na mahitaji ya mkopo huo.
Ombi hilo limetolewa jana na
baadhi ya vijana waliopata mkopo huo kupitia SACCOS ya Ibwera na
halmashauri ya wilaya ya Bukoba wakati wakiongea kwa nyakati tofauti na
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
alipotembelea wilaya hiyo ili kuona jinsi fedha hizo zilivyoweza
kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.
Vijana hao walisema kuwa fedha za
mkopo walizozipata zimewasaidia kujiinua kiuchumi ikiwa ni pamoja na
kuajiri vijana wenzao, kupanua mitaji ya biashara zao, kulipa karo za
shule za watoto wao na kujikwamua kimaisha tofauti na ilvyokuwa awali
kaba hawajapata mkopo na kufanya shughuli za ujasiriamali.
Kwa upande wake mkazi wa kijiji
cha Ibwera Ibrahim Mulokozi ambaye alipata mkopo wa shilingi laki nne
kupitia SACCOS ya kijiji hicho alisema kuwa ameweza kununua matandazo na
kulipa wasaidizi wanaohudumia shamba lake la migimba na kahawa
ambalo ni la mfano kwa vijana na wazee wanaotoka kata ya Ibwera, Mikoni
na Nyakibimbili na kwenda kujifunza na kuchukua miche ya migomba.
Alisema kuwa anakabiliwa na
changamoto za kutokuwa na fedha za kuendeleza shughuli za kilimo, kutoka
na mbolea ya kutosha ya kurutubisha shamba, bei ya miche ya kahawa
kupanda kutoka shilingi 50 hadi 500 kwa mche mmoja, kuendelea kutumia
jembe la mkono, kutokuwa na masoko ya uhakika hasa soko la ndizi na
magonjwa ya migomba.
Naye katibu wa kikundi cha
Msifuni Johanes Joel ambacho kilipata mkopo wa shilingi milioni moja na
laki tano kutoka Halmashauri ya wilaya ya Bukoba alisema kuwa kikundi
chao kinajishughulisha na kazi ya ukulima wa samaki na walianza na
bwawa moja na hivi sasa wana mabwawa matatu na wanampango wa kuhakikisha
kuwa kila mwanakikundi anakuwa na bwawa lake.
“Changamoto zinazotukabili ni
kutokuwa na mtaji wa kutosha, wanachama kutokuwa na elimu ya kuendesha
na kusimamia au kutunza miradi na kufanyiwa hujuma kwa mradi wetu wa
samaki ikiwa ni pamoja na kuibiwa na kuharibiwa kwa mabwawa hasa
nyakati za usiku na watu wasiopenda kufanya kazi za maendeleo”, allisema
Joel.
Kwa upande wake waziri Dk.
Mukangara aliwataka vijana wa kijiji hicho kufanya kazi kwa kujituma na
kujiunga katika vikundi vya maendeleo jambo ambalo litawafanya waweze
kupata mikopo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana na halmashauri ya
wilaya na hivyo kuweza kujishughulisha na kazi za upandaji wa miti,
kilimo cha samaki na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na nyuki.
Dk. Mukangara alisema, “Vijana ni
lazima mfanye kazi na kuachana na tabia ya uvivu, kufanya kazi si
lazima uajiriwe bali unaweza kujiajiri wewe mwenyewe kama hapa Ibwera
kunahali ya hewa nzuri na milima mingi haina miti mnaweza kuwa na mradi
wa kupanda miti na kufuga nyuki ambao watawapatia asali na mkiiuza
mtapata fedha nahivyo kujikwamua kiuchumi”.
Kwa upande wa mafunzo ya
ujasiriamali waziri Dk. Mukangara alisema kuwa wizara yake inavituo vya
kuwajenge uwezo vijana hivyo basi kama wahusika ambao ni vijana watakuwa
tayari kupata mafunzo ya ushirika na mafunzo mengine kama ya uongozi,
stadi za maisha watayapata na yatawasaidia katika maisha yao.
Waziri Dk. Mukangara alikuwa
mkoani Kagera kwa ajili ya kukagua SACCOS na vikundi vya vijana
vilivyopata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana ili kuona fedha
hizo zimewasaidiaje vijana kujikwamua kiuchumi. Katika wilaya ya Bukoba
alilitembelea shamba la mfano la kahawa na migomba, kikundi cha
burudani cha Rugazi na shamba la samaki la kikundi cha Msifuni.
Taarifa Ya Wizara Juu Ya Mafuta Ya Diesel Feki
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SERIKALI YAZUIA KUINGIZWA MAFUTA YA DIESELI YALIYO
CHINI YA KIWANGO NCHINI
Mwezi Novemba 2012, Kampuni ya Addax Energy SA ya Uswisi
ilishinda zabuni ya sita ya kuingiza mafuta kwa pamoja chini ya utaratibu
unaosimamiwa na Kampuni ya uagizaji mafuta kwa Pamoja (PICL).
Zabuni hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya mafuta ya Mwezi Desemba 2012 na
mwanzoni wa Januari 2013.
Utaratibu wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja huzingatia pamoja na
mambo mengine viwango vya ubora wa mafuta kama vinavyoelekezwa na
Shirika la Viwango nchini (TBS). Aidha, TBS hukagua ubora wa mafuta
hayo kabla hayajaingia nchini.
Pamoja na aina nyingine za mafuta, Addax Energy SA ilipaswa kuleta
mafuta ya dieseli yenye ujazo wa MT 100,000 sawa na takriban lita
100,000,000 katika zabuni ya sita. Meli ya AL BURAG iliyobeba mafuta
hayo ilitakiwa kufika hapa nchini na kupakua mafuta kati ya tarehe 17
mpaka 20 Desemba 2012. Hata hivyo, meli hiyo ilifika tarehe 24 Desemba
2012 ikiwa imechelewa kwa siku nne kwa mujibu wa ratiba. Mafuta hayo
yalipimwa na TBS tarehe 26 Desemba 2012 na kugundulika kuwa yako
chini ya viwango vinavyotakiwa kwa Tanzania. Aidha, tarehe hiyo hiyo,
Kampuni binafsi ya Intertek Testing Services iliyoajiriwa na PICL pamoja na
Addax Energy SA ilipima mafuta hayo na kujiridhisha kuwa yalikuwa chini ya viwango vinavyotakiwa.
Kwa kuzingatia hali hiyo Serikali imechukua hatua zifuatazo:
1. Imeiagiza PICL pamoja Addax Energy SA
IYARUDISHWE yalikotoka
2. Imeiagiza EWURA ichukuwe hatua stahiki za KISHERIA dhidi
ya Kampuni ya Addax Energy SA,
3. PICL ichukuwe hatua zinazotakiwa dhidi ya Kampuni ya Addax
Energy SA kulingana na MKATABA, na
4. Imeziagiza PICL pamnoja na EWURA kuhakikisha kuwa hali hii
haijirudii tena hapa nchini.
Aidha, Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuwahakikishia wananchi
kuwa kutopokelewa kwa mafuta hayo yaliyo chini ya viwango
HAKUTAATHIRI upatikanaji wa mafuta ya dieseli nchini kwa kuwa kwa
sasa kuna mafuta ya kutosha.
Katibu Mkuu
Friday, December 28, 2012
Wanataaluma Wa Kiislamu Nchini (Tampro) Kusaidia Wanafunzi Sekondari Za Kata
Tampro ni Jumuiya isiyo ya
kiserikali iliyoanzishwa mwaka 1994 na kusajiliwa rasmi serikalini Agost
22, 1997 ikiwa na malengo mengi na mojawapo ni kufanya tafiti, kutoa
mafunzo na ushauri wa kitaalam katika maeneo mbalimbali ya maendeleo ya
jamii.
JUMUIYA ya wanataaluma wa Kiislamu nchini (Tampro), imesema kwa kushirikiana na taasisi nyingine, inaandaa mpango mkakati wa kuhakikisha inawasaidia vijana wanaosoma katika shule za sekondari za Kata ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho kama sehemu ya jitihada zao kwa jamii ya Watanzania.

Akizungumza kuhusu maazimio ya
mkutano mkuu wa jumuiya hiyo uliomalizika juzi katika hotel ya Lamada
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji Jumuiya hiyo Sadiki Gogo,
alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kuridhika na utafiti ilioufanya na
kubaini kuna haja ya wao kama wanataaluma kutafuta njia ya kuwasaidia
vijana hao kimasomo.
”Tampro kupitia kliniki
yake ya Elimu, iliomba na kupata kibali Wizarani cha kufanya utafiti
katika shule kadhaa za sekondari za kata hapa nchini na kugundua kuwa
zina uwezo wa kufanya vizuri iwapo zitasaidiwa katika baadhi ya nyanja” alisema Gogo
Akifafanua baadhi ya nyanja
hizo, Mkurugenzi huyo, alisema pamoja na kuwapa mafunzo maalum walimu
wa shule hizo na baadae kupeleka walimu wa kujitolea katika baadhi ya
shule zitakazoonekana zina upungufu mkubwa.
Sambamba na mkakati huo ambao
amedai unalenga kuisaidia serikali, Gogo alisema Tampro kupitia mkutano
huo imeazimia kuanzisha vituo vya Elimu maalum pamoja na huduma
nyinginezo kwa watu wenye mahitaji maalum kama vile ya ulemavu.
Aidha Mkutano mkuu huo umeazimia
kushirikiana na wadau wengine nchini kuwekeza katika sekta ya Afya kwa
madai kuwa bila ya kuwa na watu wenye afya zilizoimarika ,ni ngumu Taifa
kufikia maendeleo ya kisiasa na kiuchumi.
Umoja Wa Makanisa Nchini Kuliombea Taifa Disemba 31 Uwanja Wa Taifa
NA : MWANDISHI WA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM
MUUNGANO wa Makanisa nchini
unatarajia kufanya Mkesha wa kuliombea Taifa ili amani na utulivu uliopo
uweze kudumu, ambao unatarajiwa kufanyika Desemba 31 mwaka huu kwenye
viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Godfrey
Malassy , alisema mkesha huo umekuwa ukifanyika kila Desemba 31 ya kila
mwaka, kuukaribisha mwaka mpya.
Alisema lengo la mkesha huo ni
kuliombea Taifa hilo mungu, ili aweze kuliponya na kulinusuru na majanga
mbalimbali, na kudumisha amani miongoni mwa jamii yote nchini.
Malassy aliongeza kuwa Taifa kwa
sasa linapita katika kipindi kigumu hususani kuanzia uelewa, uchumi, na
katika masuala ya usalama wa raia wa ndani na nje ya nchi ambapo kuna
baadhi ya watu wameanza kuichezea amani kwa kusababisha vurugu kwa
kvisingizio vya dini.
Pia alisema kuwa Watanzania
wanapaswa kudumisha amani na utulivu kwani hiyo ni tunu ambaayo
wamepatiwa na mungu hivyo haipaswi kuchezewa na watu wachache wasio na
nia njema.
“Mkesha wa dua hilo, utafanyika
Desemba 31 mwaka huu kuanzia saa 2:00 usiku hadi asubuhi katika viwanja
vya Taifa Dar es Salaam, na tunatarajia Rais Jakaya Kikwete atakuwa
mmoja wa wageni wetu waalikwa” alisema Malassy.
Malassy alibainisha kuwa mkesha
huo wa maombezi utashirikisha mikoa zaidi ya 16 ya Tanzania Bra na
Visiwani, ambapo utakuwa na lengo la kuwaleta Watanzania kuliombea Taifa
kwa ajili ya kudumisha amani, umoja na mshikamano visitetereke.
Maamuzi Ya Baraza La Madaktari Juu Ya Madaktari Waliogoma
Kutokana na mgomo wa madaktari uliotokea kati ya tarehe 23 na 29 mwezi
juni 2012.Wizara iliwasilisha malalamiko kwenye Baraza la madaktari
Tanganyika ili lifanye uchunguzi kuhusu madaktari hao .Idadi ya
madaktari wote waliogoma walikuwa 394, kati yao madaktari 376 walikuwa
ni madaktari walio katika mafunzo kwa vitendo (Interns) kutoka
hospitali za Muhimbili, K.C.M.C. Bugando, Mbeya Rufaa, St.Francis -
Ifakara, Dodoma, Temeke, Mwananyamala, Amana, Haydom na Sekou Toure.
Aidha, Madaktari waajiriwa(Registrar) 18 walishiriki katika mgomo huo
kutoka hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Baraza lilipitia malalamiko yote na limetoa adhabu stahiki kwa kila
daktari aliyethibitishwa kushiriki katika mgomo huo. Adhabu hizo
zilikuwa katika makundi yafuatayo; onyo, onyo kali na kusimamishwa
udaktari kwa muda wa kati ya mwezi mmoja na miezi sita.Vile vile kuna
Madaktari ambao hawakuwa na hatia ya kushiriki katika mgomo na hivyo
walifutiwa mashtaka.
MCHANGANUO WA ADHABU
• Waliofutiwa mashitaka madaktari 49
• Waliopewa onyo madaktari 223
• Waliopewa onyo kali madaktari 66
• Kusimamishwa kwa muda madaktari 30
• Mashitaka yaliyoahirishwa kutokana na wahusika kuhitaji ushauri wa
kisheria madaktari 4
• Mashitaka yasiyosikilizwa kutokana na wahusika kutofika walipoitwa
na Baraza madaktari 22
Wizara inakamilisha taratibu za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni za
Utumishi wa Umma kwa Madaktari wote waajiriwa ambao walipatikana na
hatia mbele ya Baraza la Madaktari. Wizara pia imeridhia kuwapa
Madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo fursa nyingine ya
kuendelea na mafunzo hayo katika hospitali za Umma walizokuwepo kabla
ya kuondolewa. Hata hivyo fursa hii haitawahusu Madaktari wote
waliopewa adhabu za kusimamishwa na Baraza la Madaktari, hadi hapo
watakapomaliza kutumikia adhabu zao.
HITIMISHO
Kwa taarifa hii madaktari wote waliofutiwa mashtaka na wale waliopewa
onyo na onyo kali wanatakiwa kuwasilisha kwa Katibu Mkuu Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii barua kutoka kwa msajili wa Baraza la
Madaktari ikithibitisha kurejeshewa usajili na kuruhusiwa kuendelea
na mafunzo kwa vitendo. Vile vile madaktari waajiriwa(Registrar)
wanatakiwa pia kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya ili kupewa
barua zao kulingana na Adhabu walizopewa. Barua hizi zitatolewa
kuanzia tarehe 2 Januari, 2013.Madaktari wote walio katika mafunzo kwa
vitendo wanatakiwa kuanza kazi katika vituo vyao vya awali ifikapo
tarehe 14 Januari, 2013.Hakuna muda utakaoongezwa kwa kipindi
kilichobakia cha mafunzo kwa vitendo. Kwa wale wote waliopewa adhabu
wataanza kutumikia adhabu hizo kuanzia tarehe ya adhabu hiyo
ilivyotolewa.
Nsachris Mwamwaja
Msemaji
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
27/12/2012

Nguvu Ya Rangi Katika Biashara Zetu
Na: Albert Sanga, Iringa.
Leo nitawapitisha
wajasiriamali katika somo muhimu kuhusu rangi. Je, unafahamu chimbuko la neno
yeboyebo hapa nchini? Twende pamoja. Kampuni moja ya nchini Tanzania miaka
michache iliyopita imewahi kutambulisha bidhaa zake za juisi zilizokuwa
zikifahamika kama “Yebo” Juhudi kubwa iliwekwa katika matangazo kutoa taarifa
kwa watumiaji kuhusu uwepo wa bidhaa hizo.
Juisi ile ilikuwa ni ya rangi ya njano na
katika matangazo ya kwenye televisheni walikuwa wakitumika watu waliokuwa
wamevaa kandambili za plastiki zenye rangi ya njano. Kwa sababu kandambili hizo
ndio kwanza zilikuwa zinaingia sokoni zikabatizwa jina la yebo yebo.
Haikuishia hapo, neno ‘yebo yebo’ likawa linapewa kwa kila kitu chochote kilichoonekana kutumia ama kuwa na rangi ya njano. Timu ya mpira ya Yanga ilikuwa mmoja wa waathirika wa hali hiyo kwani ilibatizwa jina la Yebo yebo!

Yebo yebo likajipatia
urasmi wa ‘kiaina’ kutumika kwa ajili ya kumaanisha kitu kinachopatikana kwa
wingi, kisicho na thamani kubwa na kinachodharaulika. Sina uhakika kampuni
husika ilichukua hatua gani baada ya hapo kujisalimisha na hatari ya bidhaa zao
kuchukuliwa “poa” kutokana na matangazo waliyoyabuni.
Ukifuatilia maarifa katika sayansi ya biashara utabaini kuwa tatizo la kuzuka kwa neno ‘yebo yebo’ halikuwa katika kandambili za plastiki wala halikuwa katika ubora wa bidhaa (kwa maana ya juisi yenyewe ukitoa ufungashaji) bali tatizo lilianzia katika rangi ya njano. Rangi ya njano ilipelekea kuzaliwa kwa dhana ya uyebo yebo kutokana na namna inavyotafsiriwa katika ubongo wa mtu.
Unapoona bidhaa yeyote ikiwa imefungashiwa kwa rangi za aina Fulani basi ujue jambo hilo halifanyiki kwa bahati mbaya bali linabeba maana kwa mtumiaji hata kama mtumiaji hajijui kwa nini anatumia bidhaa za rangi fulani na asitumie za rangi nyingine.
Ukiangalia soda ya
Seven Up kutoka kampuni ya Pepsi pamoja na soda ya Sprite kutoka kampuni ya
CocaCola utaona kuwa soda hizi zina rangi nyeupe lakini zinafungashwa katika
chupa za kijani, kwa nini?
Katika nchi nyingi masikini ikiwemo Tanzania, makampuni na wajasiriamali wengi wamekuwa hawatilii mkazo suala la rangi katika biashara zao. Hii inajumuisha katika bidhaa, mazingira ya huduma pamoja na rangi zitumikazo katika majengo ya kufanyia hizo biashara. Kupuuza suala la umuhimu wa rangi katika biashara kumepelekea wafanyabiashara na makampuni mengi kushindwa kukubalika miongoni mwa watumiaji.
Si kila rangi inafaa kupakwa katika kuta za duka, si kila rangi inafaa kutumika katika kuandika maandishi kwenye vifungashio vya bidhaa. Umakini wa kuzingatia athari za rangi miongoni mwa watumiaji kunatajwa kuwa ni moja ya sababu zinazosababisha bidhaa kutoka nje ya Tanzania kupendwa ukilinganishwa na za hapa nyumbani.
Kimsingi rangi zimethibitishwa kuwa na uwezo wa kushawishi saikolojia pamoja na tabia za watu. Mtaalamu mmoja wa saikolojia, Ward aliwahi kuulizwa njia za kuwezesha wafanyakazi kupunguza misongo wakiwa kazini. Alijibu, “Haihitaji semina wala mafunzo, jambo la msingi ni kupaka rangi sahihi katika kuta za vyumba wanamofanyia kazi, ambayo itaweka hamasiko ama mfifio kwa mabadiliko yanayohitajika”
Kwa mujibu wa mtafiti mwingine wa mambo ya biashara katika masoko, Wexner, anabainisha kuwa rangi nyekundu kwa mfano inatajwa kuwa inaambatana na hisia za kuhamasika, machungwa inaambatana na kukatishwa tamaa na kudharauliwa. Zambarau inaonesha hali ya kuthaminiwa, njano inawakilisha hali ya furaha, mzaha na kicheko na nyeusi inaonesha nguvu, umiliki na uimara.

Makampuni na biashara mbalimbali duniani kila siku zinakazana kutafuta njia za kuwezesha mwonekano na nguvu za nembo zao. Njia thabiti zinapovumbuliwa mikakati ya kimasoko huwekwa ambayo inahakikisha kuwa nembo hizo zinakuwa katika akili na fikra za wateja.
Tofauti za kiutamaduni,
kiuchumi, kijamii na nyinginezo zinaleta changamoto ya ugumu kwa biashara na
makampuni kufahamu kwa usahihi aina moja tu ya nembo ambayo itawaridhisha na
kuwapendezesha wateja wote. Hivyo biashara nyingi hasa za kimataifa zinajikuta kuwa
zinalazimika kuwa na nembo moja katika muundo tofauti tofauti ili kufanikisha
ufikaji wa bidhaa kama ilivyokusudiwa.
Mbinu mojawapo ya kimasoko inayotumika na waendeshaji wa masoko hasa kimataifa bila kujali eneo ama watu gani wanaoenda kutumia bidhaa hizo ni rangi. Rangi ni moja ya vifaa ambavyo mameneja masoko hutumia katika kutengeneza, kuimarisha na kurekebisha mwonekano wa nembo katika ufahamu wa mteja. Umuhimu wa rangi kuwasilisha maana Fulani kwa walengwa kunathibitishwa hata katika taratibu na sheria mbalimbali duniani.
Kwa mfano kule nchini Marekani kuna sheria inayofahamika kama Lanham Act ambayo inalinda rangi za bidhaa kama nembo halali za kibiashara . Rangi zinafahamika kuwa zinabeba chembechembe za kihisia na kisaikolojia.
Maana mbalimbali
zinazoambatana na rangi mbalimbali zinaumaana mkubwa sana kwa watu wanaohusika
na masoko katika bidhaa ama huduma za makampuni mbalimbali, kwa sababu mbinu za
kutangaza bidhaa ndizo huamua ukubalikaji wa bidhaa yenyewe.
Kwa mfano ua la waridi (rose) litabaki kuwa hivyo katika mataifa na tamaduni mbalimbali, lakini rangi za maua hayo zinakuwa na maana tofauti tofauti kutoka utamaduni, taifa moja kwenda jingine. Wajapan wanapendelea maua hayo yenye rangi nyeupe wakati watumiaji kutoka Hong Kong wanapendelea kutumia maua hayo ya rangi nyekundu
Mtu anapotaka kununua gari, rangi inatajwa na wataalamu wa masuala ya biashara kuwa inashika nafasi ya tatu katika orodha ya vigezo vya bei na ubora . Rangi pia ina umuhimu mkubwa sana katika ujenzi wa nembo ikiwemo logo, ufungaji na uonyeshaji .

Mtaalamu na mtafiti wa
mambo ya masoko, Wagner kupitia taasisi yake ya utafiti wa mahusiano ya rangi
na biashara, ijuliakanayo kama Wagner Color Research Institute, alijaribu kuthibitisha
dhana yake maarufu, ‘Colors are associated
with certain images’ (rangi inaambatana na taswira fulani). Wagner alitumia
kampuni inayoendesha migawaha iitwayo Wienerschnitzel yenye matawi zaidi ya 350
katika nchi ya Marekani.
Wagner aliishauri
kampuni hii kuongeza rangi ya njano kidogo katika rangi zinazopamba majengo ya
migahawa yao ili kuwasilisha ujumbe kuwa kampuni hiyo kupitia matawi yake
inauza vyakula vya bei rahisi. Baada ya kubadilisha rangi, kampuni hiyo
iliripoti ongezeko la mauzo kwa asilimia saba.
Kiujumla rangi
zinaambatana na taswira fulani kila
inapoonekana na kufikiriwa katika fikra za mteja. Kwa mfano rangi ya bluu
mahali pengi huambatana na maana na taswira ya utajiri, uaminifu na usalama.
Ndio maana ukifuatilia kwa umakini utagundua kuwa benki nyingi zinapenda
kutumia ama kujumuisha rangi ya bluu katika nembo na machapisho yao.
Hii inaingiza taswira
miongoni mwa wateja wa mabenki hayo kuwa, benki ipo imara (utajiri mkubwa), ina
umaninifu, (hivyo akaunti zake haziwezi kufanyiwa hujuma), na usalama,
(kimbilio sahihi la kutunzia hazina zake). Wakati rangi ya njano inabeba
mwonekano wa kitu cha bei rahisi
Wasimamizi wa masuala ya masoko katika makampuni na biashara wanapaswa kufahamu maana tofauti tofauti zinazoambatana na rangi ambapo maana hizo zitawezesha kugawanya na kupoka fursa mbalimbali za kimasoko kwenye jamii na tamaduni mbalimbali. Muunganiko wa rangi katika kufungasha bidhaa nao una umuhimu mkubwa sana ili kuwateka wateja.
Upo mfano mwingine wa kampuni ya kutengeneza vifaa vya kompyuta ya Apple kupitia bidhaa zake za iMac inafungasha kutumia mwunganiko wa rangi tano ambazo zina maana tofauti tofauti katika mataifa mbalimbali. Rangi hizo ni kijani, dhahabu, nyeupe, bluu na njano. Bidhaa za iMac zinapoingia Taiwan zinatafsiriwa kuwa ni amani, rafiki (kijani), zisizo na madhara (bluu na nyeupe), endelevu (dhahabu), zinazosisimua, zinazofanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi (njano).

Muunganiko huo wa rangi
unapoingia China tafsiri inakuwa ni nyingine kabisa lakini bado tafsiri
inaisaidia na kuiwezesha kampuni kuuza bidhaa zake vizuri. Kule china bidhaa za
iMac huleta maana ya; amani (kijani), nzuri na zinazoleta urembo (njano) wakati
nyeupe huwakilisha vitu vilivyo katika mpangilio na vinavyofafanulika.
Kuna changamoto kubwa inayowakabili wajasiriamali wa Tanzania hasa katika wakati huu ambao tupo katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Namna bidhaa zetu zinavyotengenezwa na kufungashwa zinaamua sana jinsi zinavyoweza kushindana katika masoko ya kimataifa.

Hata wafanyabiashara
wadogo wadogo katika maduka na vibanda vyao ni vema sana wakawa na ufahamu wa
namna ya kupaka rangi zitakazowavutia wateja na kuongeza uhakika wa kushinda
changamoto za kiushindani!
Mwanafunzi Afariki Ndani Ya Chumba Cha Nyumba Ya Kulala Wageni Akitolewa Mimba
MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari ya
Tongoni nje kidogo ya jiji la Tanga, (jina tunalihifadhi) amekutwa
amekufa ndani ya nyumba ya kulala wageni alikopelekwa kutolewa mimba
bila mafanikio.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na
kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe
mwanafunzi huyo alikutwa amekufa juzi katika nyumba ya kulala wageni
iliyopo barabara ya 21 jijini Tanga.
Mmoja wa wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni
ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema kwamba mwanafunzi huyo
aliingia saa 4.00 asubuhi siku ya tukio akiwa ameambatana na kijana
mmoja wakakodi chumba.
“Baadaye alikuja mwanaume mmoja wa makamo ambaye
alituuliza kama wameingia mwanafunzi huyo na mwenzake, tulipomwonyesha
chumba walichoingia naye akakodi chumba cha jirani ndipo tukaona wote
wakijifungia kwenye chumba kimoja,” alisema mhudumu.
Mhudumu huyo alisema baada ya muda wa saa moja,
mvulana na mzee huyo wakaaga kwamba wanatoka huku wakisema kwamba
msichana amebaki chumbani akiwa amepumzika. Akithibitisha habari hizi,
Kamanda Massawe alisema taarifa ya tukio hilo ilitolewa na mhudumu wa
nyumba hiyo ya kulala wageni katika Kituo cha Polisi cha Chumbageni
Jijini Tanga.
“Tatizo ni kwamba nyumba hii ya wageni wahudumu
wake hawakuwapa wageni hao daftari ili waorodheshe majina yao hivyo
inakuwa vigumu kuwafahamu,” alisema Kamanda Massawe na kufafanua kuwa
alifariki akitolewa mimba ya mwezi mmoja.
Kamanda Massawe alisema mpaka sasa hakuna mtu
aliyekamatwa na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini
waliohusika na kifo hicho.Raisa Said, Tanga
Tuesday, December 25, 2012
Sunday, December 23, 2012
JIWE WALILOLIKATAA WAASHI LIMEKUWA JIWE KUU LA PEMBENI
Lema anatisha sana Arusha
HABARI LEO
MTANZANIA
TANZANIA DAIMA
NIPASHE
MWANANCHI
MAJIRA
HABARI LEO
MTANZANIA
TANZANIA DAIMA
NIPASHE
MWANANCHI
MAJIRA
Kontena la kondom mbovu lakamatwa
zimebainika kwamba zipo madukani
Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
wamelazimika kufanya msako mkali kwenye baadhi ya maduka ya dawa jijini
Dar es Salaam baada ya kubainika kwamba tayari kondomu hizo zipo sokoni.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es
Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Leandri Kinabo alizitaja kondomu
hizo kuwa ni aina ya Melt Me zenye thamani ya Sh222.1 milioni
zilizokamatwa tangu Oktoba 23 mwaka huu na kuzuiliwa bandarini hapo kwa
taratibu zaidi za kisheria.
“Jambo lililotushtua ni kwamba zimebainika kwamba
zipo madukani, tukajaribu kufuatilia tena bandarini tukifikiri kuwa
huenda zimetolewa kinyemela licha ya kuzuiliwa ili ziteketezwe au
zirejeshwe nchini India kwa gharama zao wahusika.
Tulipokwenda bandarini tukabaini kwamba bado zipo
katika hali ile ile, kumbe zimeingizwa nchini kwa njia ya panya, kwa
kweli ni mbovu na ndiyo maana tumelazimika kuwajulisha wanahabari ili
muwape taarifa wananchi wawe makini,” alisema Kinabo.
Alifafanua zaidi kwamba kondomu hizo ni mbovu
kwani zimebainika kuwa na vitundu, pia zinapasuka haraka, hazina kabisa
viwango vya ubora wa bidhaa unaotakiwa na Shirika la Viwango la
Kimataifa (ISO).
Kinabo alisema kuwa TBS bado wanaendelea kufanya
mawasiliano na kampuni iliyotengeneza kondomu hizo, lakini kwenye kasha
lake inaonyesha kuwa inaingizwa nchini na kampuni ya Fair Deal Exim ya
Dar es Salaam.
Katibu Bavicha Tanga ‘kukiona’
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Mwenyekiti wa Chadema mkoani humo, Saidi Mbwete alisema kitendo cha
Katibu huyo kumtaka Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa ajiuzulu kwa
kumiliki kadi ya CCM ni cha utovu wa nidhamu.
Mbwete alisema kauli na vitendo vya katibu huyo, vinaonyesha utovu wa nidhamu na kumdhalilisha Dk Slaa.
Alisema mtu anapohama chama kimoja na kujiunga
na kingine, huwa amejitoa moja kwa moja kutoka kwenye chama chake cha
awali.“Kurudisha kadi ya chama cha awali, ni hiari ya mwenye kumiliki
kadi hiyo kwani ni yake kwa sababu ameinunua na kuilipia,” alisema
Mbwete.
“Hata katiba za vyama vingi hazisemi kwamba mwanachama anapokihama chama chake, anatakiwa arudishe kadi,” alisisitiza
Mwenyekiti huyo alisema uongozi wa mkoa wa chama hicho, umekuwa ukifuatilia nyendo za kiongozi huyo wa Bavita na kugundua kuwa anatumiwa na CCM ili aivuruge Chadema.
Mwenyekiti huyo alisema uongozi wa mkoa wa chama hicho, umekuwa ukifuatilia nyendo za kiongozi huyo wa Bavita na kugundua kuwa anatumiwa na CCM ili aivuruge Chadema.
“Tumegundua kuwa huyu si mwenzetu kwa sababu
mawazo yake huwa kwake ni uamuzi ya kikao, ndiyo maana hata tangazo lake
la kumkosoa Dk Slaa halikuwa na baraka za kikao,” alibainisha.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa
wao kimkoa hawana mamlaka ya kumfukuza katika uongozi au uanachama
isipokuwa watapeleka mapendekezo yao kwenye vikao vya ngazi ya juu kwa
uamuzi wa mwisho.
Madai hayo ya kumshughulikia katibu huyo,
yamekuja baada ya kutoa waraka unaomtaka Dk Slaa ajiuzulu kutokana na
kumiliki kadi mbili za vyama vya siasa.
Na Raisa Said, Tanga
Na Raisa Said, Tanga
COAST UNION YA TANGA YAPATA NAFASI YA PILI KOMBE LA UHAI
Azam mabingwa Kombe la Uhai 2012
Wachezaji wa Azam wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Uhai kwa kuifunga Coastal Union kwa penalti 3-1 jana kwenye Uwanja wa Karume. Picha na Michael Matemanga
AZAM imenyakua ubingwa wa Kombe la Uhai kwa kuichapa Coastal Union kwa penalti 3-1, baada timu hizo kutoka sare 2-2 katika dakika 120 kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Shujaa wa Azam alikuwa kipa wao Aishi Manula
aliyeokoa penalti tatu kati ya nne zilizopigwa na Coastal Union na kuipa
ubingwa timu yake.
Kwa ushindi huo Azam wamejinyakulia kitita cha
Sh1.5 milioni, Coastal Union wakiondoka Sh1 milioni, huku mabingwa wa
msimu uliopita Simba wakiondoka na Sh500,000 kama washindi wa tatu.
Katika mchezo huo Azam walianza mchezo huo kwa
kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza katika dakika 11 kupitia,
Samwel Mkomolo, kabla ya Kelvin Friday kupachika bao la pili kwa mkwaju
wa penalti katika dakika 34.
Coastal Union ‘Wagosi Wakaya’ walibadilika kipindi
cha pili na kufanikiwa kupata mabao ya kusawazisha yaliyofungwa kwa
kichwa kwa kupitia Mohamed Miraji katika dakika 61 na Ally Iddi (77) na
kufanya mchezo huo kwenye dakika 30 za nyongeza.
Fainali hiyo ilishudiwa na Rais wa TFF, Leodegar
Tenga, Idd Kipingu na Said Mohamed mwenyekiti wa Azam pamoja na mamia ya
mashabiki waliojitokeza kwenye uwanja huo.
Mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Mzee alinyakua
Sh300,000 tuzo ya ufungaji bora baada ya kufunga mabao sita, huku
mchezaji bora wa mashindano, Joseph Kimwaga wa Azam alipata Sh350,000.
Ruvu Shooting ilitwaa tuzo ya timu yenye nidhamu
itakabidhiwa Sh400,000, wakati kipa bora Mansour Ally wa Coastal Union
alipata Sh300,000.
Kocha bora Bakari Shime wa Coastal Union alizawadiwa Sh300,000 kama ilivyokuwa kwa mwamuzi bora wa michuano hiyo.
Kocha bora Bakari Shime wa Coastal Union alizawadiwa Sh300,000 kama ilivyokuwa kwa mwamuzi bora wa michuano hiyo.
AZAM imenyakua ubingwa wa Kombe la Uhai kwa kuichapa Coastal
Union kwa penalti 3-1, baada timu hizo kutoka sare 2-2 katika dakika 120
kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Shujaa wa Azam alikuwa kipa wao Aishi Manula
aliyeokoa penalti tatu kati ya nne zilizopigwa na Coastal Union na kuipa
ubingwa timu yake.
Kwa ushindi huo Azam wamejinyakulia kitita cha
Sh1.5 milioni, Coastal Union wakiondoka Sh1 milioni, huku mabingwa wa
msimu uliopita Simba wakiondoka na Sh500,000 kama washindi wa tatu.
Katika mchezo huo Azam walianza mchezo huo kwa
kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza katika dakika 11 kupitia,
Samwel Mkomolo, kabla ya Kelvin Friday kupachika bao la pili kwa mkwaju
wa penalti katika dakika 34.
Coastal Union ‘Wagosi Wakaya’ walibadilika kipindi
cha pili na kufanikiwa kupata mabao ya kusawazisha yaliyofungwa kwa
kichwa kwa kupitia Mohamed Miraji katika dakika 61 na Ally Iddi (77) na
kufanya mchezo huo kwenye dakika 30 za nyongeza.
Fainali hiyo ilishudiwa na Rais wa TFF, Leodegar
Tenga, Idd Kipingu na Said Mohamed mwenyekiti wa Azam pamoja na mamia ya
mashabiki waliojitokeza kwenye uwanja huo.
Mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Mzee alinyakua
Sh300,000 tuzo ya ufungaji bora baada ya kufunga mabao sita, huku
mchezaji bora wa mashindano, Joseph Kimwaga wa Azam alipata Sh350,000.
Ruvu Shooting ilitwaa tuzo ya timu yenye nidhamu
itakabidhiwa Sh400,000, wakati kipa bora Mansour Ally wa Coastal Union
alipata Sh300,000.
Kocha bora Bakari Shime wa Coastal Union alizawadiwa Sh300,000 kama ilivyokuwa kwa mwamuzi bora wa michuano hiyo.
Kocha bora Bakari Shime wa Coastal Union alizawadiwa Sh300,000 kama ilivyokuwa kwa mwamuzi bora wa michuano hiyo.
Saturday, December 22, 2012
TAIFA STARS YAWAKANDAMIZA MABINGWA WA AFRIKA 'CHIPOLOPOLO' 1-0 UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM
MATOKEO YA MPIRA WA MIGUU KATI YA TAIFA STARS NA CHIPOLOPOLO LEO MARA BAADA YA DAKIKA TISINI
Hivi ndivyo Usomekavyo Ubao wa Matokeo katika Uwanja huu wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa kipindi cha kwanza cha mchezo katika ta Taifa Stars na Mabingwa wa Afrika,Zambia wana Chipolopolo.kipindi cha kwanza kimemalizika sasa huku Taifa Stars ikiongoza kwa bao moja lililotiwa kimiani na Mrisho Ngassa mnamo dakika 45 ya mchezo kipindi cha kwanza.
Mrisho Ngassa mnamo dakika 45 ya mchezo kipindi cha kwanza akiachia shuti kali lililoizawadia Tanzania ushindi.
Mashabiki wa Timu ya Taifa ya Tanzania wakishangilia Ushindi wa timu yao.
kocha wa Taifa Stars Kim Poulsen akipeana mkono na kocha wa Chipolopolo ambaye alionekana kutofurahishwa na matokeo ya mchezo.
Subscribe to:
Posts (Atom)